Fisadi Kinje Mbona Haongelewi

LeoKweli

JF-Expert Member
Apr 23, 2008
335
18
Jamani Mnaona Watoto Wa Wakukubwa Wanvyo Rithi Ufisadi,
Hebu Anagalia Ubungo Terminals Ya Mabasi Ilivyochakaaa , Harafu Cha Kushangangaza Ni Kwamaba Kinje Anakula Kuku Tu, Mbabe Yeye Ukimwambia Kitu Bunduki Mkononi Anatashia Kuku Ditopile

Tuliko kuwa Tunaenda huyu bwana angeweza hata kukuvua nguo kwa kodi zetu

Parking King kinje

Kinje Fichio La Ufisadi
 
leokweli
could you please, break it down with more details then we can pick it up from there?
 
Mimi naamini kweli kuna ufisadi kuhusu hilo swala
1 Tenda ya parking iko chini yao na haikutangazwa na kugombniwa kwa haki...monopoly..tangu wapate je wameendeleza nini hata hawajatengeneza parking space.
2 Kituo cha mabasi kiko chini yao na je tangu wachukue wamekiendeleza vipi?

Ufisadi upo usikatae ndugu yangu...mtu kula kuku kwenye nchi yako ni sawa lakini endeleza basi na jiwekee jina
 
Leokweli karibu sana JF,

........katika maelezo yako naona kuna jambo muhimu ambalo inabidi kujiuliza.....nalo ni MAINTENANCE......nafikir hili neno pale kwetu Tanzania tulishalifuta kabisa

na hivyo basi:

1.Kampuni ya Kinje responsibilities zake ni nini?
2.Nini wajibu wa serikali katika kituo kile.
3.Mkataba wa Kinje ni wa muda gani?

Kuhusu Kinje kupata hiyo Zabuni pengine ungetuwekea information zaidi........je unaweza kuthibitisha kuwa Zabuni haikutangazwa? (hili lisiwe jukumu lako peke yako.....bali hata mtu mwingine ajuaye ukwlei anaweza kutuwekea)

......JF iko kazini.......na kila Jiwe litapinduliwa na kila uvungu JF itachungulia
 
Mimi naomba kuunga mkono hoja iliyotolewa kuhusu hizo kampuni za kina Kinje, kuanzia hiyo iliyopewa tenda ya Ubungo Bus Terminal, na hiyo ya kuegesha magari mjini, Tanzania Parking Services, kama ifuatavyo:

1) Ubungo Bus Terminal ni vurugu tupu. Kuanzia nje hadi ndani, hakuna kinachoeleweka. Hakuna mpango hakika wa huduma kwa wanaotoa huduma na wanaopokea huduma. Hakuna usalama wa uhakika. Nje ya hiyo terminal kumejaa wezi, vibaka na matapeli. Unaweza kurubuniwa - kama wewe si 'mtoto wa mjini' (hehe, mimi hawanipati) - na kuambiwa kuna basi linaondoka 'fasta fasta'. Wewe na haraka zako, ukawafuata wale watu mpaka ndani. Kumbe wameshakula njama na mtu ambaye atakuwa na kitambulisho bandia, kuonesha kwamba yeye ni mkataji tiketi wa hilo basi; tena amevaa sare za kampuni hiyo ili kukupa matumaini na uhakika kwamba 'huingizwi mjini'. Wale ambao ni wafanyakazi halali wa kampuni ya hilo basi, kwa wakati huo, wako kimya, wakikutazama, kwani wanajua kwamba kwenye hizo pesa utakazokatishwa tiketi bandia kuna mgao wao! Unakata tiketi, unakaa kwenye kiti 'chako' ndani ya basi tayari kusubiri safari kuanza. Mara basi linaanza safari yake, anaingia kondakta wa basi na mkaguzi wa tiketi. Anapofika kwako unampa tiketi uliyokatishwa, hapo ndipo kizaa-zaa kinapoanza. Unaambiwa "Tiketi hii si yetu. Tunaomba utulipe fedha zetu au ushuke nje." Nadhani mnajua kinachoendelea baada ya hapo.

Kampuni ya kina Kinje mbona haiweki watu wa kuhakikisha kwamba wanaokata tiketi wanatambuliwa rasmi, kwa mfumo mzuri zaidi wa utambulisho? Mbona haiwajibiki kuweka matangazo kuwatahadharisha wateja kwamba, kwa hali yoyote ile, wasikate tiketi NDANI ya eneo la terminal, ila, wakate tiketi zao kwenye ofisi maalum zilizo kwenye uzio wa terminal hiyo?

2) Tukienda kwenye hawa wanaotoza wenye magari ada ya maegesho ya magari, kule ni tabu tupu. Si tu kwamba haieleweki nani mwenye wajibu wa kutoa huduma za ulinzi wa magari yanayoegeshwa, bali pia, inasadikika kwamba baadhi ya watoza kodi hao hushirikiana na vibaka wanaoiba vifaa kwenye magari, kama vile side mirrors, radio, etc. Hii inatokana na ukweli kwamba watoza kodi hao HAWAAJIRIWI kama wafanyakazi, ila wanaajiriwa kama vibarua, yaani, CASUAL LABOURERS! Pia, wanawekewa viwango maalum (quota) vya makusanyo ya ada za maegesho kwa kila siku na kila wiki. Wasipovifikia (viwango ambavyo, kutokana na hali halisi si rahisi kuvifikia), huachishwa kazi na kufukuzwa kama mbwa. Wapo vijana wengi tu ambao 'wamepitia' ajira za 'wiki moja' kama watoza kodi ya maegesho ya magari jijini Dar, na watakuambia yaliyowasibu! Kiwango kikubwa cha Shs. 30,000/= kwa wiki kufikiwa si rahisi. Kwa wasichana, wengi wao wanalazimika 'kutembea' na mabosi wa kampuni hiyo ili wasifukuzwe kazi, kwani ukweli ni kwamba hali mbaya ya uchumi inawafanya vijana kufanya kazi aina yoyote ile, hata kama kazi hiyo itahatarisha afya zao. Kwa akina dada, wengi wao hulazimishwa kufanya ngono bila kinga, jambo ambalo linachangia kueneza kasi ya maambukizi ya UKIMWI!

Nyie mnaosema hoja hii isijadiliwe hapa mnakosea, kwani kina Kinje na wenzake wanarithishwa na kuendeleza ufisadi! Ufisadi, kwa hali yoyote ile, lazima ujadiliwe, na lazima upingwe!

Wewe unayekataa tusijadili hili suala, basi, mimi binafsi nina mashaka nawe, kwani wewe pia, kwa kukataa hoja hii, moja kwa moja nawe ni FISADI!

Siogopi kusema! Nitasema tu! Mtake msitake! Kwani, kama hujajua bado, Ibara ya 18 (1) na (2) inanipa uhuru wa kutoa maoni yangu. Kwa maoni yangu, mkataa pema pabaya panamwita... unaitwa FISADI kwa kuwa unakataa tusijadili ufisadi huu!

Bora niende kaburini nikitetea haki, kwani walio wengi, wanyonge, wamepokwa haki yao, kuliko kukaa kimya na kuwa mwoga, nikisema, naogopa kufa, au si kazi yangu kusema!

./Mwana wa Haki!
 
Jamani Mnaona Watoto Wa Wakukubwa Wanvyo Rithi Ufisadi,
Hebu Anagalia Ubungo Terminals Ya Mabasi Ilivyochakaaa , Harafu Cha Kushangangaza Ni Kwamaba Kinje Anakula Kuku Tu, Mbabe Yeye Ukimwambia Kitu Bunduki Mkononi Anatashia Kuku Ditopile

Tuliko kuwa Tunaenda huyu bwana angeweza hata kukuvua nguo kwa kodi zetu

Parking King kinje

Kinje Fichio La Ufisadi

Hii mbona imekaa ki-Michuzi-Michuzi.

Lakini,mwandishi pia ungekuwa na facts kidogo zaidi ya hizo.Mfano,kampuni ile sio ya kinje bali ya mama yake,pili walitaka kunyang'anywa tender na watu wa city lakini wakasema wamekopa pesa nyingi kuweka mitambo.Kinje,as Kinje ana kampuni yake ya kukodi magari na ana magari mengi tu
 
Jamani wana JF,

Ukiangalia kwa undani ni jinsi gani nchi yetu inakuwa costed na Project Mpya za kimaendeleo utagundua kwamba hatuwezi kuafford ubadhilifu wa mali za Umma tena.

Sisi sote tunajukumu kama watanzania kulinda mali na rasilimali za Taifa letu na hii ndio inayo nisikitisha mimi kuona kwamba watu wengine wantumia nafasi zao kujinufaisha wenyewe bila kujali hali ya baadae ya rasilimali hizo.

Ubungo Terminal imeicost Jiji fortune of money lakini ukiangali hali yeke kwasasa inahidaji ukarabati ambao unakalibiana na initial investment iliyowekwa pale.

Management Audit imekuwa haifanyiki kwasababu ya Vitisho vya bwana Kinje, kinje kwakutumia Jina la mzee wake kwa miaka Mingi amekuwa akikumbatia Miradi Mingi ambayo haijulikani ameipataje , siajabu hata mikopo anayochukua ndio ile ile isyokuwa na collateral.

Na mtu kama kije kabla haujashituka na tabia hizohizo utasikia ni mbunge, Jamani tuangalieni Mbele, Hatutaki nchi inayorishwa kwa mafisadi tena.

Parking system zimekuwa zikiingiza mamilioni , Htuajawahi kuona report za mapatao yake, Hata hizyo parking haisaiidii hata kazi za kimaendleo zilizo karibu yake.

Ninajua kwamba wana JF mnajua zaidi kuliko mimi, na chunguzeni tu mtajua zaidi kinachoendelea ......

Mwisho hatuwezi kuendelea kuongoza nchi kama tukiachia vitendo vya ubabaishaji viitawale kila sekta
 
we mwaga mambo wala usikatishwe tamaa na hao hapo juu...hapa kazi ni kumkoma nyani giladi kweupee where we dare to talk openly....hakuna cha umbea hapo ni ukweli mtupu labda mnachotakiwa kumwambia mtoa hoja ni viambatanisho vitakavyo tetea hoja yake...otherwise kila mtu anamjua Kinje na ndio maana baadhi ya wanafiki wanaiponda maada hii..
 
Jamani wana JF,

Ukiangalia kwa undani ni jinsi gani nchi yetu inakuwa costed na Project Mpya za kimaendeleo utagundua kwamba hatuwezi kuafford ubadhilifu wa mali za Umma tena.

Sisi sote tunajukumu kama watanzania kulinda mali na rasilimali za Taifa letu na hii ndio inayo nisikitisha mimi kuona kwamba watu wengine wantumia nafasi zao kujinufaisha wenyewe bila kujali hali ya baadae ya rasilimali hizo.

Ubungo Terminal imeicost Jiji fortune of money lakini ukiangali hali yeke kwasasa inahidaji ukarabati ambao unakalibiana na initial investment iliyowekwa pale.

Management Audit imekuwa haifanyiki kwasababu ya Vitisho vya bwana Kinje, kinje kwakutumia Jina la mzee wake kwa miaka Mingi amekuwa akikumbatia Miradi Mingi ambayo haijulikani ameipataje , siajabu hata mikopo anayochukua ndio ile ile isyokuwa na collateral.

Na mtu kama kije kabla haujashituka na tabia hizohizo utasikia ni mbunge, Jamani tuangalieni Mbele, Hatutaki nchi inayorishwa kwa mafisadi tena.

Parking system zimekuwa zikiingiza mamilioni , Htuajawahi kuona report za mapatao yake, Hata hizyo parking haisaiidii hata kazi za kimaendleo zilizo karibu yake.

Ninajua kwamba wana JF mnajua zaidi kuliko mimi, na chunguzeni tu mtajua zaidi kinachoendelea ......

Mwisho hatuwezi kuendelea kuongoza nchi kama tukiachia vitendo vya ubabaishaji viitawale kila sekta

Kinje ameshajizatiti kugombea ubunge, tayari kabisa kumwangusha yule mtoto wa CHADEMA John Mnyika. Kama sehemu ya mkakati mwisho wa mwaka 2007 alifanya shehere kubwa na wakazi wa Kata ya Kibamba na kugawa nyama. Pia ameshafanya hafla nyingine kata ya Kimara iliyohusisha wajumbe wa nyumba kumi. Ni wazi amedhamiria kushinda

PM
 
Nafikiri inatakiwa achukue muda kidogo kuindaa vizuri ili iweze kuchangiwa +ve au -ve kulingana na facts.... ni vema aongeze maelezo kidogo yahusuyo mkataba wa hiyo coy ya Ubungo bus terminal si lazima mkataba mzima bali yaliyomo yahusuyo wajibu na majukumu ya mkandarasi
 
5.jpgHivi huyu jamaa bado anaendelea kukusanya pesa pale 7/7 na kule kwenye kituo cha mabasi ubungo au?
 
Alishanyanganywa!jamaa na mtoto wa daniel yona walifisadi sana rasilimali zetu!hawa ni ma mission town balaa
 
ha ha haaaaaa yaani wewe ulishindwa kuvumilia sio????lol

ule udaku wa the utamu wa kipipi umekukaa mpaka umeuropoka...lol
nimecheka mpaka basi.....lol
hahahahahah unafikiri udaku...angejua sifa yake angejituliza tu!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom