Fisadi kamandoo

Shetemba

JF-Expert Member
Jan 20, 2018
872
871
Kamandoo wa jeshi ni mtu ambaye ana uwezo wa hali ya juu wa kupambana katika hali zote masika na kiangazi,mjini au vichakani.

Mmiliki wa kampuni ya UDA ni bonge la
Komandoo, big up popote alipo kwa majanga yote aliyoyafanya na mpaka sasa hivi bado anapeta kwenye game hakika
Namuaminia.
Kwanza aliinunua kampuni ya UDA kama shati alichofanya alimwekea mzee Iddi simba hela kwenye akaunti yake kilichofuata akamweka sawa marehemu Masaburi na wenzake mchezo kwisha .

Hakina Kubenea na mnyika walijaribu kupiga kelele wee sasa hivi kimya
Mashilawadu wanadai walilambishwa mpunga pale karimjee ,wale wa CCM Abas Mtemvu na Zungu waliambiwa wanatumia makalio kufikiria: sasa hivi cd ya UDA imeskrachi;
Sasa hivi singo mpya inaitwa UDART
Katoka alikotoka ametua kwenye huo mradi watu wa Kimara na Mbezi wanalia mateso wanayoyapata kutokana na huyo bwana kuwarundika kwenye mabasi yake kama ngombe lakini serikali imekaa
kimya
Je kwa awamu hii ya kutumbua majipu angekuwa ni mtu mwingine angesalimika kweli si angekwisha tumbuka zamani.
 
Acha walundikwe tu
Kwanza wameshazoea
Pili ni mazoezi tosha
Tatu wameshazoea kupumuliana
DSM hoyeeee.

images
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom