Fisadi hassanoo kisutu tena!

Hute

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,537
6,458
BAADA YA KUWA NA KESI YA WIZI WA CONTENA LA MADINI YA SHABA, YALIYOKUWA YANASAFIRISHWA TOKA ZAMBIA KWENDA BANDARI YA DSM, sasa mwenyekiti wa mpira Kibaha HASSANOO amefikishwa na leo tena kwa kushiriki kutenda kosa la wizi na uuzaji wa meno ya tembo yaliyosafirishwa na kukamatwa huko Hong Kong. kesi yao imetajwa leo huko kisutu.....

TAFAKARI: ukiona wenzio wanaendesha magari mazuri, usifikiri yote ni ya kihalali. nchnji hii inaliwa na wenye meno.
 
wana JF NILIWAHI sema hapa kuwa huyu jamaa,dewji,pinda wanafanya biashara hii!bado kuna wachina wapo ubungo mil bus park
 
wapigwe risasiii..hizi sheria zetu vipi jamanii ziko dhaifu sanaaa akifungwa hapo 3yrs or 2yrs
 
hizi si ni tuhuma, au jamaa amepatikana na hatia ? kama ni tuhuma tusubiri hukumu, nafahamu huyu bwana ana kampuni yake ya clearing and fowarding hivyo tusimuhukumu ,polisi wakusanye ushahidi wa kutosha , mahakama itoe hukumu ya haki ,jamii imuite jina sahihi hivi sasa tunamuonea .
 
Hassanoo anakila na wakubwa!! Kesi itarindima weeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee mwisho hautaisikia tena!!! Labda iwe amepindisha deal ndipo atapata kibano!! Changa la macho!! Ukiwa na hela Tz kufungwa si rahisi sana, labda kuwe na big shot nyumba ya kesi yako!!
 
ni rahisi kwa ngamia kupenya katika tundu la sindano kuliko tajiri kuurithi ufalme wa Mbinguni
 
Back
Top Bottom