Fisadi Asababisha kigugumizi kwa Kikwete. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fisadi Asababisha kigugumizi kwa Kikwete.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Indume Yene, Jan 12, 2009.

 1. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #1
  Jan 12, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Katika hali isiyotegemewa, Rais Jakaya Kikwete amekumbwa na kigugumizi cha utoaji vyeti kwa wale waliosaidia kuchangia ununuzi wa pikipiki kwa makada wa SISIEMU. Fisadi huyo ni Japhet Lema anayejulikana zaidi kwa jina la NJAKE.

  Pikipiki hizo zenye thamani ya millioni 24.5 zilikuwa zigaiwe kwa Makatibu wa Chama wilayani Arusha. Mgeni wa heshima katika utoaji huo Rais Kikwete alichezwa na machale ya kuzigawa hizo pikipiki pamoja na vyeti baada ya kugundua kuwa Fisadi Njake ni mmoja wa wadhamini waliochangia ununuzi huo. Hivyo aliutupa huo mpira kwa viongozi wa chama hicho wilayani ili waweze kujigawia.

  Hata hivyo danadana ilianza baada ya viongozi wa wilaya nao kuanza kurushiana mpira.

  Hii inatia aibu sana, kwa nini Mwenyekiti wa SISIEMU(T) ambaye ni Rais wa JMT asiamuru kurudishwa kwa fedha alizotoa fisadi kununua hizo pikipiki badala ya kurushiana mpira? Bado hizo pikipiki zitatumiwa na SISIEMU, kwa hiyo JK kuruka viunzi na kuchomoa kugawa pikipiki kwa makada wake bado hakuleti unafuu wowote. Hizo ni baadhi ya pesa za wizi zilizonunua hizo pikipiki kwa ajili ya usafiri wa makada wa SISIEMU.
   
 2. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #2
  Jan 12, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Jakya kukataa kugawa hizo pikipiki hakuwaondolei sifa hawa CCM kuwa ni mafisadi; mbona walipokea shilingi milioni 400 kufadhili mkutano wa vijana mchana kweupe zilizotolewa ma fasadi Somaia ambaye tunajua fika kuwa alihusika na kutuibia kwenye dili ya radar!! Huu wote ni usanii wa muungwana.
   
 3. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #3
  Jan 12, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Labda JK hakujua kipindi hicho kuwa Somaia ni fisadi vilevile kwa njia moja au nyingine. Zitawatokea matakoni tu muda ukifika. Wananchi bado wanaendelea na ANALYSIS zao.
   
 4. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #4
  Jan 12, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Ndiyo maana nasema tuzidi kuwapigia kelele hawa mafisadi. Kelele zetu baada ya JK kupokea shs. 400,000,000/-, zimemfanya aogope kupokea hizo piki piki - si picha zingepigwa ? Kidogo kidogo tutafika na aibu zao zitawafanya angalau wawe waoga lakini kamwe hauwasafishi kwenye ufisadi - huo ni mfumo wa maisha ndani ya CCM.
   
 5. J

  JokaKuu Platinum Member

  #5
  Jan 12, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,769
  Likes Received: 4,982
  Trophy Points: 280
  wandugu,

  ..hizo pikipiki zimetolewa na mafisadi ambao hawako kundi moja na Raisi Kikwete.

  ..zingetolewa na wale mafisadi wanaomuunga mkono basi angetoa baraka zake na kuzikabidhi kwa wanachama.

  ..Sophia Simba amechaguliwa kwa kutumia rushwa ya fedha za mafisadi walioko ktk kundi la Raisi Kikwete. hiyo ndiyo sababu iliyomfanya Raisi aivumilie rushwa ktk uchaguzi wa mwenyekiti wa UWT.

  NB:

  ..ukitaka ufanikiwe ktk masuala ya ufisadi inabidi uwe ktk kundi linamuunga mkono Raisi Kikwete ndani ya CCM.

  ..kujifanyia ufisadi kivyako-vyako kama Mramba,Yona,na Mgonja, is too risky these days.
   
Loading...