Fisadi anataka kukimbia na kutoroka Nchini

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
2008-07-02 09:52:45
Na Mwandishi Wetu, Dodoma


Mbunge mmoja ambaye ni miongoni mwa watuhumiwa katika kashfa ya mkataba wa aibu wa Richomond ambayo baadaye ilikabidhi shughuli za kufua umeme wa dharura kwa Dowans ameelezea nia yake ya kung?atuka kwenye siasa kabla ya 2010.

Habari ambazo Nipashe imepata kutoka katika vyanzo vya kuaminika zimedai kwamba mbunge wa CCM (jina linahifadhiwa), ametangaza nia ya kuachia ubunge kabla ya uchaguzi mkuu wa 2010 na kuleta hofu ya uwezekano wa kufanyika uchaguzi mdogo jimboni kwake.

Habari hizo zilisema jana kwamba baada ya mbunge huyo kueleza nia yake ya kujiuzulu, chama chake kimeanza kupanga mikakati ya kuchukua tena jimbo hilo litakalobakia wazi wakati wowote.

Imeelezwa kwamba mbunge huyo ambaye pia ni kada wa kuaminiwa wa chama hicho, pamoja na kuachana na siasa anataka pia kuondoka nchini kutokana na kuchafuliwa na kashfa mbalimbali.

Kwa mujibu wa habari hizo, mbunge huyo, amekuwa akilalamika kwamba kuhusishaa na kashfa ya Richmond kunamfanya ajione kuwa wapiga kura wake na umma hawana imani naye tena.

Kufuatia msimamo wake, habari zimesema kwamba CCM imeanza kujipanga kutafuta wagombea watakaochukua nafasi yake iwapo ataliachia jimbo wakati wowote kuanzia sasa.

Habari zilisema kwamba baadhi ya wakongwe wa CCM wako jimboni kwake wakichunguza na kuandaa mikakati ya kulirudisha jimbo hilo kwa chama tawala iwapo mbunge huyo atashikilia msimamo wake wa kuachia ngazi.

Nipashe jana jioni ilipiga simu ya mbunge huyo ili kusikia kauli yake lakini ilikuwa haipokelewi.

Na ilipowasiliana na Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuph Makamba, simu yake ilipokelewa na msaidizi wake ambaye alijibu kwamba suala hilo anatakiwa kujibu mbunge husika na si ofisi ya Makamba.

Iwapo kiongozi huyo atajiuzulu ubunge atakuwa miongoni mwa wanasiasa wachache waliojiuzulu ubunge ambapo mwaka 1990 aliyekuwa Waziri wa Kazi na Vijana na Mbunge wa Vunjo, Bw. Augustine Mrema, alijiuzulu nyadhifa hizo na kujiunga na upinzani.

Kashfa ya Richmond baada ya kuibuliwa Bungeni kwa sura ya kifisadi na kamati teule ya Bunge hilo iliyoongozwa na Dk. Harrison Mwakyembe, ilisababisha Waziri Mkuu, Edward Lowassa kuachia ngazi.

Pamoja naye, mawaziri wawili waliohusishwa pia na tuhuma za mkataba huo, Dk. Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi waliwajibika pia kujiuzulu nyadhifa zao.

Wiki hii kashfa ya Richmond ilifikia hatua nyingine baada ya TANESCO kukatisha mkataba na kampuni ya Dowans iliyorithi mikataba ya Richmond.
_____________________________

Je ninani huyo au katika walewale ambao wamejiuzulu uwaziri ?
 
I smell fisadi Rostam anataka kuachia ngazi....suala sio kuchafuliwa jina..ukweli ni kuwa ametuibia ana hela ya kutosha kuishi peponi Canada, USA au UK.
 
Ingekuwa kuna uadilifu wa uongozi Tanzania basi huyo fisadi angefilisiwa mali zake kabla hajaondoka akaanze upya huko aendako. Lakini si Tanzania ile hii ya sasa ni nchi ya Wanzania inayotawaliwa na viongozi ambao baadhi yao ni mafisadi.
 
Fisadi akisha ondoka wataanzisha tume kungalia nani haswa alisajiri na kuleta Dowans Tanzania na kuangalia hasara gani zilipatikana kutokana na uwekezaji huo.
 
Haya yote ni matokeo ya viongozi ambao si wazalendo na tena wamegeuza kazi ya kuongoza nchi kama vile biashara. Basi tuige viongozi wa nchi zilizoendelea. Ufisadi hufanywa na mameneja wa makampuni lakini si viongozi wa serikali au "sirikali". hope Mungu anatufunulia. I real pray for him to resign so that his/her weakness can reveal the reality that he/she is the FISADI.
 
ROSTAM...keshaiba vya kutosha...baadaye tuhuma zikianza...atapotelea sayari nyingine then atabadilisha living tag kuwa deceased ,then ataishi huko for the rest of his life...Just like Balali...
 
ROSTAM...keshaiba vya kutosha...baadaye tuhuma zikianza...atapotelea sayari nyingine then atabadilisha living tag kuwa deceased ,then ataishi huko for the rest of his life...Just like Balali...
 
Fisadi akisha ondoka wataanzisha tume kungalia nani haswa alisajiri na kuleta Dowans Tanzania na kuangalia hasara gani zilipatikana kutokana na uwekezaji huo.

Af Mkullo ataenda kumtafuta aliko, na serikali haitakuwa na shida nae ikuwa na shida nae itamtafuta, af mara gafla atakufa na snema imeishia hapo....
 
Wanaanchi waamshwe sasa kwani wakati wa kulindana umepita lakini CCM wanauendeleza Tagi ya mapambano sasa ni CCM mwisho wake 2010 ,Piga ua galagaza mafisadi ondokeni serikalini.
 
mmh magazeti ya TAnzania bwana sasa mnaogopa nini kumtaja kuwa ni RA??atakufungia wewe MENGI au mnakula nae?kwa nini hamjamtaja?
member tu wa hapa JF wanajua ni RA je wananchi watajuaje?Kama si kupitia kwenye vyombo vya habari..angalia sasa vyombo vya habari vyenyewe vinaandika habari nusu nusu na kimafumbo mafumbo namna hii.
 
na ni serikali hiyo hiyo ndio itakayo mtorosha.... mtaona...

Baada ya kutoroshwa huyu RA usishangae serikali yako ya ccm itakapokutangazia kuwa haimuhitaji kwa lolote..... then amekufa na maiti imechomwa moto na majivu yake yamezikwa baharini huko Canada.........!
 

Kuna kitu cha ajabu sana si tu kinachofanywa na vyombo vya habari kama magazeti na redio bali na waandishi. Kitu hicho ni uwajibikaji, ni waandishi wachache sana wenye ujasiri wa kuita sepetu, sepetu .Hapa naongelea sana kuhusu habari za uchunguzi, media na wanaofanya uandishi nadhani vyuo walivyosoma hawafundishwi kuhusu kutafuta habari kwa undani.

Mara zote tizama taarifa za habari zote zinakuwa na ile 'fulani kasema bla blah na akadabla za kufa mtu'. Sishangazwi na 'mwandishi wetu' lakini kwanini kila habari inakuwa kama nilivyotaja hapo juu. hivi kweli tuliache gazeti moja tu ama mawili ndo yaandike habari za uchunguzi (ambazo nashukuru sana kuwa zote zinaanzia JF).

Nafikiri ni muda wa waandishi wetu kuacha woga na kufanya kazi yao na kuzingatia maadili ya kazi husika.

Kama ni ufisadi basi uandikwe kwa ukweli mweupe (naked truth) na sio kuita uma, kijiko.



Taaluma itakulinda ukiiheshimu
 

Kuna kitu cha ajabu sana si tu kinachofanywa na vyombo vya habari kama magazeti na redio bali na waandishi. Kitu hicho ni uwajibikaji, ni waandishi wachache sana wenye ujasiri wa kuita sepetu, sepetu .Hapa naongelea sana kuhusu habari za uchunguzi, media na wanaofanya uandishi nadhani vyuo walivyosoma hawafundishwi kuhusu kutafuta habari kwa undani.

Mara zote tizama taarifa za habari zote zinakuwa na ile 'fulani kasema bla blah na akadabla za kufa mtu'. Sishangazwi na 'mwandishi wetu' lakini kwanini kila habari inakuwa kama nilivyotaja hapo juu. hivi kweli tuliache gazeti moja tu ama mawili ndo yaandike habari za uchunguzi (ambazo nashukuru sana kuwa zote zinaanzia JF).

Nafikiri ni muda wa waandishi wetu kuacha woga na kufanya kazi yao na kuzingatia maadili ya kazi husika.

Kama ni ufisadi basi uandikwe kwa ukweli mweupe (naked truth) na sio kuita uma, kijiko.

Ndio maana huwa nasema Tanzania hakuna press.

Hakuna habari inaandikwa Bongo imekamilika. Ukiiona tafadhali nitumie PM.
 
ROSTAM...keshaiba vya kutosha...baadaye tuhuma zikianza...atapotelea sayari nyingine then atabadilisha living tag kuwa deceased ,then ataishi huko for the rest of his life...Just like Balali...

Wamwache aondoke mikono mitupu. Mali zake zote zibaki Tanzania na kufanyiwa uchunguzi kama alizipata kihalali, kama alizipata kiharamu basi zifilisiwe.
 
Taarifa hii ilianzia jimboni Igunga kwani alifanya mikutano ya hadhara na akawa anatoa ujumbe huo kuwa anangatuka.

Kwa wale mnaokumbuka baada ya kusema maneno hayo mara gazeti la majira likajitokeza na kusema kuwa CHADEMA NA CCM wapinga Rostam Azizi kungatuka.

Fumbo mfumbie mjinga mwerevu..................

Hii story haikuwa na umuhimu kiasi hicho na kuwekwa front page kwani iliwahi kuwepo na sio ya kiuchunguzi .
 
Ushauri wangu ni wananchi waanze kuwa makini...Inawezekana mambo yana wa tight.
Sasa MWEMA na wenzake wahakikishe kuwa hawa watu wako nchini hadi Kikwete atakaporudi kwani tuna maswali mengi ambayo ni JK mwenyewe anayetakiwa kutupasha kiunaga ubaga!
Mwema anaweza akawaachia watoroke kwani Rais mwenyewe hajawaambia cha kufanya kuhusiana na ripoti yao!
Hao watu WAKAMATWE MARA MOJA.
 
Wamwache aondoke mikono mitupu. Mali zake zote zibaki Tanzania na kufanyiwa uchunguzi kama alizipata kihalali, kama alizipata kiharamu basi zifilisiwe.


ataondoka mikono mitupu, lakini kiukweli mwenzio alishahamishia huko aendako vijisenti vya kutosha, na ndio anavifuata; hivyo atakavyoviacha Tz vitamfuata huko huko afterwards.
 
ushauri Wangu Ni Wananchi Waanze Kuwa Makini...inawezekana Mambo Yana Wa Tight.
Sasa Mwema Na Wenzake Wahakikishe Kuwa Hawa Watu Wako Nchini Hadi Kikwete Atakaporudi Kwani Tuna Maswali Mengi Ambayo Ni Jk Mwenyewe Anayetakiwa Kutupasha Kiunaga Ubaga!
Mwema Anaweza Akawaachia Watoroke Kwani Rais Mwenyewe Hajawaambia Cha Kufanya Kuhusiana Na Ripoti Yao!
Hao Watu Wakamatwe Mara Moja.

Mwema Amkamate Rostam Azizi? Thubutu, Huyu Ndiye Mwajiri Wao Wote Kuanznia Kikwete, Makamba, Mkapa Nk. Atajiondokea Taratibu Na Atakuwa Anaingoza Serikali Akiwa Kanada
 
Richmond: Vigogo hatarini kudakwa

2008-07-02 17:06:55
Na Mwandishi Wetu, Jijini


Kuna taarifa kuwa lile sakata la mkataba tata baina ya Serikali na kampuni ya kuzalisha umeme ya Richmond limechukua sura mpya baada ya baadhi ya vigogo maarufu kuanza kuliwa mingo ili wadakwe kabla ya kuchukua hatua zozote za kutimkia nje ya nchi.

Taarifa za uhakika toka kwenye chanzo chetu zinadai kuwa hivi sasa, kuna makachero waliojipanga kila kona wanapokuwa vigogo hao ili kuhakikisha hakuna yeyote atakayeweza kutimka nchini kirahisi, ili kukwepa mkondo wa sheria kutokana na `dili` hilo lililozaa kashfa ya malipo ya kifisadi ya zaidi ya Sh. Milioni 180, yanayolipwa na Serikali kila siku.

Taarifa hizo zinadai kuwa kujiandaa kwa makachero wa Jeshi la Polisi na wale wa Usalama wa Taifa katika kuwawinda vigogo husika, zinatokana na taarifa zilizowafikia kuwa kuna mmoja yuko kwenye mipango ya kujiandaa kuikimbia nchi baada ya mambo kuwa mazito.

``Hakuna aliye juu ya sheria...hata huyo uliyemtaja, hawezi kuchomoka kwa namna yoyote...Wana usalama wanazo taarifa zote na wamejiweka tayari kumfuatilia ili akijaribu tu, wamtie mbaroni,`` kimedai chanzo chetu.

``Mimi nakuambia, kwa vyovyote vile, kigogo huyo hawezi kutekeleza mpango wake huo wa kuikimbia nchi kwa sababu Serikali imejipanga vilivyo katika kuzuia jaribio la aina hiyo,`` chanzo chetu kikaongeza.

Kashfa ya mkataba wa Richmond imekuwa gumzo kubwa nchini, hasa baada ya kuanikwa kwa ripoti ya Kamati ya Bunge iliyoongozwa na Mhe. Harisson Mwakyembe kuonyesha kuwa Serikali iliingizwa mkenge kwa kuingia mkataba wa kuzalisha umeme na kampuni hiyo iliyoelezwa kuwa ni ya kitapeli.

Hata hivyo, Richmond waliuhamishia mkataba wao kwa kampuni nyingine ya Dowans, ambayo hadi sasa inadaiwa kuwa inalipwa na Serikali zaidi ya Sh. Milioni 150 kwa siku, huku Tanesco ikitoa tamko kuwa itasitisha kuhusika na kampuni hiyo mwezi ujao.

Katika taarifa hiyo, vigogo kadhaa walitajwa kuhusika kwa namna moja au nyingine na hatua kadhaa zikapendekezwa kuchukuliwa dhidi yao.

Kufuatia mapendekezo ya kamati hiyo ya Dk. Mwakyembe, mbunge wa Kibaha Vijijini ambaye alikuwa Waziri wa Afrika Mashariki, Dk. Ibrahim Msabaha alilazimika kujiuzulu uwaziri wake, kama ilivyokuwa kwa mbunge wa Bukoba Vijijini Mhe. Nazir Karamagi, (pichani ukurasa wa mbele) ambaye aliitema nafasi aliyokuwa nayo ya uwaziri wa Nishati na Madini.

Aidha, Mbunge wa Monduli Bw. Edward Lowassa, naye alilazimika kujiuzulu nafasi ya kuwa Uwaziri Mkuu na kupelekea kuvunjwa kwa baraza zima la mawaziri.

Baadhi ya waliotajwa katika ripoti hiyo ya Dk. Mwakyembe, kwamba wanahusika na Richmond kwa namna mbalimbali ni pamoja na Mbunge wa Igunga (CCM), Mhe. Rostam Aziz, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Johnson Mwanyika na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa , Dk. Edward Hosea.
  • SOURCE: Alasiri
 
Back
Top Bottom