Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,745
2008-07-02 09:52:45
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Mbunge mmoja ambaye ni miongoni mwa watuhumiwa katika kashfa ya mkataba wa aibu wa Richomond ambayo baadaye ilikabidhi shughuli za kufua umeme wa dharura kwa Dowans ameelezea nia yake ya kung?atuka kwenye siasa kabla ya 2010.
Habari ambazo Nipashe imepata kutoka katika vyanzo vya kuaminika zimedai kwamba mbunge wa CCM (jina linahifadhiwa), ametangaza nia ya kuachia ubunge kabla ya uchaguzi mkuu wa 2010 na kuleta hofu ya uwezekano wa kufanyika uchaguzi mdogo jimboni kwake.
Habari hizo zilisema jana kwamba baada ya mbunge huyo kueleza nia yake ya kujiuzulu, chama chake kimeanza kupanga mikakati ya kuchukua tena jimbo hilo litakalobakia wazi wakati wowote.
Imeelezwa kwamba mbunge huyo ambaye pia ni kada wa kuaminiwa wa chama hicho, pamoja na kuachana na siasa anataka pia kuondoka nchini kutokana na kuchafuliwa na kashfa mbalimbali.
Kwa mujibu wa habari hizo, mbunge huyo, amekuwa akilalamika kwamba kuhusishaa na kashfa ya Richmond kunamfanya ajione kuwa wapiga kura wake na umma hawana imani naye tena.
Kufuatia msimamo wake, habari zimesema kwamba CCM imeanza kujipanga kutafuta wagombea watakaochukua nafasi yake iwapo ataliachia jimbo wakati wowote kuanzia sasa.
Habari zilisema kwamba baadhi ya wakongwe wa CCM wako jimboni kwake wakichunguza na kuandaa mikakati ya kulirudisha jimbo hilo kwa chama tawala iwapo mbunge huyo atashikilia msimamo wake wa kuachia ngazi.
Nipashe jana jioni ilipiga simu ya mbunge huyo ili kusikia kauli yake lakini ilikuwa haipokelewi.
Na ilipowasiliana na Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuph Makamba, simu yake ilipokelewa na msaidizi wake ambaye alijibu kwamba suala hilo anatakiwa kujibu mbunge husika na si ofisi ya Makamba.
Iwapo kiongozi huyo atajiuzulu ubunge atakuwa miongoni mwa wanasiasa wachache waliojiuzulu ubunge ambapo mwaka 1990 aliyekuwa Waziri wa Kazi na Vijana na Mbunge wa Vunjo, Bw. Augustine Mrema, alijiuzulu nyadhifa hizo na kujiunga na upinzani.
Kashfa ya Richmond baada ya kuibuliwa Bungeni kwa sura ya kifisadi na kamati teule ya Bunge hilo iliyoongozwa na Dk. Harrison Mwakyembe, ilisababisha Waziri Mkuu, Edward Lowassa kuachia ngazi.
Pamoja naye, mawaziri wawili waliohusishwa pia na tuhuma za mkataba huo, Dk. Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi waliwajibika pia kujiuzulu nyadhifa zao.
Wiki hii kashfa ya Richmond ilifikia hatua nyingine baada ya TANESCO kukatisha mkataba na kampuni ya Dowans iliyorithi mikataba ya Richmond.
_____________________________
Je ninani huyo au katika walewale ambao wamejiuzulu uwaziri ?