Fisadi alitaka kujitafutia umaarufu Kenya...

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,792
287,994
...Raila akamtolea nje
Wengine sawa, si Benjamin Mkapa

Jabir Idrissa
Tanzania Daima

SINA tatizo na wajumbe wengine katika kazi ya kupatanisha wanasiasa wa pande mbili wanaovutana nchini Kenya, baada ya moja kupinga matokeo yaliyompa ushindi Mwai Kibaki.
Kibaki anayeongoza Chama cha PNU, anapingwa kama rais na chama cha ODM chini ya Raila Odinga. Msimamo wa ODM kupinga ushindi wa Kibaki, umesababisha hali kuchafuka na kuleta balaa la mauaji na uharibifu mkubwa wa mali.

Kuna kundi la wasuluhishi limeanza kazi ya kuwapatanisha wanasiasa hawa kama jitihada za kimataifa za kutuliza hali mbaya inayoendelea kujiri katika nchi hiyo yenye uchumi mzuri zaidi kwa kanda ya Afrika Mashariki.

Nafahamu ubora wa mstaafu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Koffi Annan. Ana uwezo na uzoefu wa kutosha wa kupatanisha makundi yanayovutana. Amekuwa katika nyanja hii kwa miaka mingi. Ni Muafrika aliyebobea katika uongozi wa masuala ya kimataifa.

Vilevile sina tatizo na ubora wa Graca Machel, mke wa rais wa kwanza wa Afrika Kusini huru, Nelson Mandela aliyerithi mke wa mpigania uhuru maarufu nchini Msumbiji, Samora Machel aliyeuawa kikatili na mkono wa utawala wa Makaburu. Mama huyu ana uwezo, imani na moyo wa upendo juu ya Waafrika.

Tatizo langu kubwa ni huyu Benjamin Mkapa, mstaafu rais wa Tanzania, aliyeongoza kwa miaka 10 kutoka Novemba 1995 hadi Desemba 2005. Simuamini hata kidogo kuwa msuluhishi na kile ninachokijua kuhusu yeye, ndiyo msingi wa mtazamo wangu leo.

Hebu tufahamu kwanza maana halisi ya kupatanisha. Kupatanisha ni kufanya kazi ya kukaribisha watu wanaovutana waelewane.

Kuwaweka karibu watu wanaotofautiana ili wapunguze misimamo mikali juu ya tofauti zao kwa kuzingatia zaidi maslahi ya jamii.

Mpatanishi anatakiwa kuwa mtu mweledi, mwenye fikra pevu za kiutu, mwenye upendo kwa watu na muadilifu kama kiongozi katika jamii. Uadilifu ninaoutaja hapa ni wa kiwango cha juu si cha kubahatisha.

Bila shaka huyu anakuwa ni mtu ambaye katika historia yake ya utumishi wa umma, hususan alipopata nafasi ya kuongoza watu, alitumikia watu hao kwa uadilifu mkubwa.

Kwamba ni mtu aliyeongoza vizuri na kuonyesha hasa ni kiongozi mwenye dhamira ya kweli ya kuwa kioo kwa anaowaongoza.

Mpatanishi, lazima awe mtu msafi kwa maana zote. Kukiwa na dalili hata ndogo za uchafu kwake, huyo hafai kupatanisha wavutanao.

Mpatanishi hawezi kuwa mtu jeuri, mwenye kiburi, mwenye fikra ambazo mara nyingi hazijibainishi wazi. Kwamba wakati anaamini hivi na kutamka hivyo aaminivyo, kumbe utendaji unabadilika. Huyu hawezi kuwa mpatanishi au msuluhishi.

Tanzania tunao watu wachache mno, kwa medani ya wanasiasa, wenye sifa za kuwa wasuluhishi. Ninasema wachache mno kwa sababu harakaharaka, ninawapata wawili, mstaafu Katibu Mkuu wa Umoja wa Afrika (AU), Dk. Salim Ahmed Salim na mstaafu Waziri Mkuu, Joseph Warioba.

Hawa wanafahamika vema katika kuongoza usuluhishi. Ni wasafi na uadilifu wao kama viongozi wa umma hawana shaka ndio maana wanakumbukwa sana na wanaposema leo wanasikilizwa.

Dk. Salim na Jaji Warioba, kutokana na walivyo wanadiplomasia mahiri, wamepata kutumwa na kutumika kama wasuluhishi sehemu mbalimbali barani Afrika na hata nje. Hawa wanaiweza kazi ya upatanishi.

Mkapa ana madoa mengi. Historia yake katika uongozi wa umma imechafuka mno, tena chafu kweli kweli. Zile sifa nilizozitaja za mtu kufuzu kuwa msuluhishi, nyingi hanazo. Ila moja anayo na kwa kiwango kikubwa kisicho shaka, ya ueledi.

Simnyimi haki yake hapa. Ana upeo mkubwa wa kufahamu mambo maana ana akili ya kuzaliwa. Ni mjuzi hasa na hili huenda ndilo jambo lililompatia nafasi ya kuwa katika kamisheni ya kimataifa inayohamasisha kukubalika kwa itikadi mpya ya utandawazi.

Tatizo kwake ni zile sifa nyingine. Upendo kwa watu, fikra pevu za kiutu, usikivu na uadilifu kama kiongozi. Kipimo changu kwa haya ni mambo yaliyotokea nchini kwetu au aliyoyatenda alipokuwa kiongozi wa jamhuri yetu. Haya ndiyo yamemchafua isivyomithilika.

Wakati hapa nchini tuhuma dhidi yake kuhusu ufisadi uliotokea chini ya uongozi wake, hazijatulia - maana mwenyewe hajajitokeza hadharani kujieleza, ameweka kitangulizi kibaya katika historia ya uongozi wa taifa hili linaloendelea kusifika kama kisiwa cha amani.

Amani ya Tanzania ilichafuka mwaka 2001 kwa sababu alishindwa kuwajibika ipasavyo siyo kutuliza hali mbaya ya kisiasa iliyoikumba Zanzibar, bali aliichangia iwe ilivyo.

Mkapa alidharau hata ushauri aliopewa na baadhi yetu tulipoona mambo yanakwenda mrama.

Alijua kwamba asipodhibiti makundi ya vijana wahuni waliopewa jina la ‘Janjaweed' waliokuwa wakidhaminiwa na chama chake, hali itazidi kuwa mbaya.

Vijana hawa walitishia maisha ya wananchi, wakiwadhalilisha mchana kweupe na wakahujumu mali zao.

Vijana hawa walitumia magari ya serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye nyendo zao zote. wakilishwa na viongozi wa CCM au na mamluki waliowatumikia viongozi. Walihutubiwa na kupewa moyo.

Nilipata kumwandikia waraka maalum Mkapa wakati nikifanya kazi kwenye Kampuni ya Habari Corporation Ltd (HCL) ambayo moja ya magazeti inayochapisha ni Rai. Nilimweleza kuwa ni yeye pekee mwenye uwezo wa kuinusuru Zanzibar na balaa hilo.

Yaliyotokea wakati wa kampeni za uchaguzi na yaliyofuatia baada ya upigaji kura, ni mambo ya kupangwa kwa utaratibu makini uliopata baraka ya dola, ambayo ilikuwa chini ya Amiri Jeshi Mkuu aliyeitwa Benjamin William Mkapa.

Na haya yalikuwa ni tamati ya dharau ya Mkapa katika kuhimili na kudhibiti matumizi mabaya ya vyombo vya dola. Alishindwa kudhibiti hali tangu mwaka 2000 ndipo Tanzania ikaingia doa kubwa kihistoria, la mauaji ya kikatili ya Januari 26 na 27 ya wananchi wasio na hatia.

Tanzania ilipata wakimbizi kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi yenyewe kuwa ndiyo kimbilio la wakimbizi wa mataifa jirani yalipokuwa na migogoro ya ndani.

Mkapa alishindwa kuwajibika kama kiongozi wa jamhuri, kwa hivyo alichangia kuwepo kwa migogoro na mauaji yasiyokuwa na lazima yoyote.

Sasa ni wapi mtu aliyeshindwa kudhibiti migogoro iliyosababisha mauaji anateuliwa kuwa msuluhishi? Wengine sawa, si Mkapa katika usuluhishi wa mgogoro na ghasia za kisiasa nchini Kenya.
 
Mkapa anatafuta namna ya kusafisha jina lake kupitia Kenya baada ya kuwa ameliangusha kwenye tope huku Tanzania.

Mkapa hawezi kazi hiyo; alishindwa kwa Mugabe, hataweza kwa Kibaki.
 
Mkapa hadi sasa hivi hapo alipo mikono yake haijakauka damu za innocent people wa Pemba na Mwembechai. Wacha hao masikini wanaokufa vijijini kwa kukosa lishe bora na matibabu kwa sababu za ufisadi wake. Ana tuhuma za kujibu hapa duniani na dhambi za kutosha kabisa kwa Muumba wake Aliye Juu
 
Kama kuna watu wenye roho ngumu hapa duniani, ni pamoja na mr clean aliye badilika na kuwa mr dirty! nashangaa sana anavo stahimili na kuendelea kukaa kimya! Hivi kweli ana roho ya nyama yule? ama roho yake imeumbwa kwa jiwe?? siju1 kwakweli...

Alipo enda Erdorite Na Chissano. yeye hotuba yake aliongea kama ugomvi anawabwatukia wakenya walio hitaji manenno ya Faraja, lakini alipo ongea Chissano pamoja na kiswahili kisicho fasaha.. alishangiliwa sana na alitoa maneno ya ubinadamu ya kufariji!

I doubt Mkapa anamatatizo makubwa sana kuliko tunavodhani!!
 
Duuuh hili ni bonge la DONGO kwa BWM

Na hili dongo alilitengeneza mwenyewe, acha alioge! Tulisema na tutazidi kusema, kwamba demokrasia haiwezi kuzimwa kwa risasi ama vifaru, hivi vyote havina uwezo wa kuzima sauti ya umma!
 
Wakati hapa nchini tuhuma dhidi yake kuhusu ufisadi uliotokea chini ya uongozi wake, hazijatulia - maana mwenyewe hajajitokeza hadharani kujieleza, ameweka kitangulizi kibaya katika historia ya uongozi wa taifa hili linaloendelea kusifika kama kisiwa cha amani.

Aaaah! Huyu si alisema kuwa hataki mambo ya siasa yeye amestaaafu, sasa huko alienda kufanya nini huyu? Yaaani sisi wabongo na huu ujiko! Nani alimuita huko Alienda na watu wanagapi? Waliolipiwa na nani? Na yeye amelipiwa na nani?
 
labda kwa tafsiri ya mku huyu (bwm) upatanishi wa kisiasa sio siasa. nashindwa kushangaa kabisaaa
 
Jamani pengine kateuliwa kwa sababu ya kuongea kiswahili ambayo wengine watakuwa hawaitelewi, lakini anamdhalilisha sana MH ANAN Katika timu yake, Hatahivyo raila inamaana hamjui mkapa kama ni mtu wa aina gani?
 
sasa wakalimani wanafanya nini? mi nadhani mkuu huyu atumie muda wake mwingi kuangalia jinsi gani atatupa watanzania maelezo yanayojitosheleza kuhusu tuhuma zinazomkabili. haya masuala ya ujiko wa kisiasa ayaache kwa sasa na badala yake ajisafishe kwa watanzania.
 
Swali langu ni kuwa, Raila kasema hayo au ni muandishi wa makala anaeleza maoni yake? Maana mtoa mada katika mstari wake wa kabla ya makala anaeleza kuwa Raila kamkataa lakini makala nzima haielezi hivyo hata kwenye mstari mmoja.

Sitaki kuwa hyped up kwamba Raila kamkataa kumbe nimuandika makala tu.
 
mkapa si alisemwa na kikwete kuwa tumuache mzee apumzike kwa amani, kumbe hataki kupumzike basi tumuendee. Maana kama anaweza kwenda kenye, kumbe na mahakamani anaweze. Dr. slaa na Makani mko wapi? huyu bwana hataki kupumzika.
 
Huu ni ushahidi wa wazi juu ya maono yake alipokuwa Rais kuwa Waandishi wa habari wetu wengi ni mbumbumbu ktk medani hiyo,hoja za Jabiri Idrissa zimejipanga uzuri dhidi ya Mh.Ben Mkapa lakini kwanini ujifanye unamnukuu Raila wakati ndani unajifungua kuwa wewe ndie mwenye maoni hayo???!!!!

Pamoja na hayo yote yanayomuandama huyu mzee bado siioni mantiki ya mpemba Jabir kujifanya msemaji wa Raila, mbona anatumia nguvu nyingi kuuangalia upande mmoja wa shilingi kwa namna ya kinyonga angalau ungelituonyesha wasifu wa Litmus pengine tungelijua unathubutu kuona madhaifu ya pande zote.

Ni Mkapa aliyethubutu kuwaambia Wapemba na waunguja waache kurithisha ubaguzi kwa vizazi vijavyo,na alitahadharisha kuwa hayuko tayari kuona hali hiyo inaliangamiza taifa na yuko tayari kutumia mamlaka ya dola kudhibiti aina yoyote ya uangamizi,na alifanya hivyo akiwa amiri jeshi pale wapemba walipojaribu kuitikisa nchi,waswahili wana msemo "Nyundo iligongwa kabla ya Kugonga" Jabiri angalia hilo kwa dhati ikiwa unataka kuwarithisha wazanzibar nchi njema, umemsikia Mh.Balozi Karume, ninadhani wakati umefika wa wewe nawe kujiangalia nafsini mwako kama ni chanzo cha yale ya Zanzibar 2001; Kuhusu Kenya huko nako Mzee Ben amewaambia wakenya kabla hata hajateuliwa na UN kumsaidia Koffi, waache siasa ktk medani za kikabila bali wajiegemeze ktk mawazo chanya yatakayoijenga nchi yao na uwepo wa makabila ubakie ni tunu ya mungu juu yao.Koffi naye juzi baada ya kulikwepa sana hilo amejikuta hana namna zaidi bali kukubaliana na Ben kuwa Ukabila unaitafuna Kenya,hata wao wakenya ukiwauliza si Raila wala Kibaki au Toroitich wanaoweza kukiri bayana kuwa ni ukabila tu.

Baada ya matokeo ya uchaguzi Kenya mwanahabari mwenzio Marin wa TBC aliwataka watanzania wafahamu kuwa kiini cha mgogoro ule ni Ukabila na udini,amethubutu siku ile kurejea kauli ya Kibaki alipokiri kuwa ilimchukua takribani siku kumi kuwaomba wazee wa Kikuyu wamruhusu kukiri kuwa behind his presidency there was a man from Luo who engineered his victory,Loooh ilileta moto kwa Wakenya by then na siku ile kwa wale pannelist pale TBC especially Prof Baregu na Mkamia,hawakukubalina naye.

Please,kama ni uandishi basi ni lazima tuwe wakweli sana,tusiwe wabinafsi na zaidi ya hapo tujiwekee msingi wa kuruthishana ukweli na si fitna.Mkapa amekosea pake na sisi pia tuna mahala tumekosea kama alivyofanya Jabir sasa.
Naomba kutoa hoja
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom