First year wote na tulioko vyuoni soma hii tusije laumiana yakitokea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

First year wote na tulioko vyuoni soma hii tusije laumiana yakitokea

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by MKINDE, Aug 30, 2012.

 1. M

  MKINDE Member

  #1
  Aug 30, 2012
  Joined: Aug 16, 2012
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  USHUHUDA ULIONITOA CHOZI MBELE YA AKADAMNASI.........SOMA ILA USILIE

  NAIKUMBUKA HII SIKU AMBAYO MWANAUME NILITOKWA NA CHOZI BAADA YA KUPATA USHUHUDA HUU KUTOKA KWA MDAU NINAYEMJUA KABISA NA AMBAYE ALIKUWA NI MPIGANAJI NA MWANA HARAKATI WA KUTETEA HAKI ZA WANAFUNZI WENZAKE HAPA CHUONI…..
  Namkumbuka sana mshikaji wangu japokuwa hayupo tena nami hapa duniani, nashindwa ni jinsi gani niilete hii kwenu ila inanibidi niiweke kama stori ya kumbukumbu ya kichwa changu itakavyoniongoza…..
  Namkumbuka jamaa huyu ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa chuo kikuu hapa mlimani miaka ya nyuma kidogo ambaye alishawahi kupata pigo ambalo lilimpeleka kaburini, ishu ilikuwa hviii….
  Jamaa alikuwa ni mwanafunzi wa chuo husika hapo juu ambaye alikuwa akiishi mabibo hostel na alikuwa ni mwongeaji sana na kutokana na kipaji chake hicho alibahatika kupata marafiki wengi kila kona ya chuo hiki kwani kila apitapo wanafunzi wenzake humwita na kutarajia burudani ya stori na vituko kutoka kwake…..
  ….NAMKUMBUKA…
  Nakumbuka zilibaki siku kama tano ili tuanze mitihani ya chuo (UE) kwa ajili ya kumaliza semester ya kwanza ndipo jamaa akapata taarifa kuwa anahitajika na mlezi wa wanafunzi chuoni (dean of student), jamaa alifika mpaka kwenye ofisi ya mlezi huyo na kupewa taarifa ya kwamba hatoweza kufanya mitihani ya semester kwakuwa kuna taarifa mbaya kutoka nyumbani kwao, jamaa alipouliza ni taarifa gani hiyo aliambiwa mama yake mzazi amefariki……..
  ….NAMKUMBUKA…
  Bado namkumbuka,, taarifa ya kifo cha mama yake ilimuathiri sana kisaikolojia huyu jamaa ambapo nikiwa kama shuhuda wa jambo hili mimi ndiye niliyetajwa kama rafiki mkubwa ambaye angependa niongozane nae kwenye msiba japo ilishindikana kutokana na taratibu za chuo…..
  ….NAMKUMBUKA..
  Taarifa ya kifo cha mama yake ilikuja akiwa chuoni lakini pia alipata taarifa ya kifo cha baba yake aliyefariki kwa ugonjwa wa presha alipopata taarifa ya kifo cha mkewe alipokuwa yupo safarini kurudi kwake kutoka katika shughuli zake za kila siku, ni pigo juu ya pigo kwa mshikaji wangu…..
  …NAMKUMBUKA…
  Jamaa baada ya mapito aliyoyapitia alirudi chuoni, kama ulivyo utamaduni wetu wanafunzi tulichangishana ili kuweza kupata rambirambi za mwenzetu kisha maisha yakaendelea, jamaa alipomaliza kufanya mitihani yake ya semester ya kwanza ndani ya semester ya pili aliandaa kama kikao kisha watu tulikusanyika kisha akatoa shukrani zake kwa wanafunzi wa chuo kwa moyo waliouonesha kwake na pia kuwaombea kila la kheri katika masomo yao wawapo hapa chuoni na pia maisha mema popote waendako……
  ….NAMKUMBUKA…
  Hapa ndipo chozi lilipoanza kunidondoka, ndani ya semester ya pili jamaa alibahatika kukutana msichana mmoja kwa jina XXX kisha akajitambulisha kwamba yeye ni mwanafunzi wa chuoni hapo na anasoma BA. ED yaani bachelor of arts education jamaa yeye alikuwa anachukua BSC.ED yaani bachelor of science education hivyo jamaa alifurahi kwani aliamini ya kwamba amepata mtu ambaye wangeweza kushirikiana sana katika masomo ...Maisha ya ushirikiano katika masomo yanaendelea kisha mapenzi nayo yanaingia kati hivyo jamaa na binti XXX wanaanza mahusiano ya mapenzi ambapo kila mmoja hamjui mwenzie historia yake katika suala hilo………
  …NAMKUMBUKA…
  Ni vigumu sana kuweza kuamini ila imemtokea jamaa yangu…, Nakumbuka kipindi jamaa yupo mwaka wa tatu alijitolea kuwa kampeni meneja wa mwanachuo mwenzake aliyekuwa anagombea nafasi ya urais chuoni hapa…. Kutokana na kipaji alichojaaliwa cha kupendwa na kila mwanafunzi hivyo popote alipo simama watu wengi walijitokeza kumsikiliza, mara nyingi alikuwa anatumia sanaa yake ipasavyo hivyo wanafunzi hupata burudani iliyoambatana na kampeni ndani yake…..
  …NAMKUMBUKA…
  Baada ya kampeni kwisha ndipo nafasi ya uchaguzi inapoingia, wanafunzi tunashiriki kupiga kura na hatimaye mshindi anatangazwa, mshindi ni yule aliyekuwa akipigiwa kampeni na rafiki yangu…. Vifijo na nderemo ndivyo vinavyotawala kila kona ya chuo hiki baada ya vifijo na nderemo ndipo simanzi na huzuni inapotawala mara baada ya rafiki yangu kupanda jukwaani na kutoa shukrani zake kwa ushindi walioupata yeye akiwa kama kampeni meneja……..
  …..NAMKUMBUKA….
  Alianza kwa kusema:; Nawashukuru ndugu wanafunzi wenzangu kwa kuelewa na kuweza kumpigia kura nyingi sana kiongozi huyu aliye mbele yetu, kwa upande wangu sina shaka nae na ningependa kumpa ujumbe huu kisha aufanyie kazi…. Kisha alimgeukia rais wa chuo, mkuu tumekuchagua ili uwe daraja kati yetu na utawala wa chuo hiki, tumekuchagua ili utuwasilishie matatizo yetu panapo husika na kupatiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo, nitaonekana nisiye na busara hata kidogo ndani ya chuo hiki kama haya niliyoyaongea hayatotimizwa ndani utawala wako……na,…..( Jamaa alisita kidogo kIsha akawageukia wanafunzi)…….
  ….NAMKUMBUKA….
  Alisema:; Ndugu wanafunzi wenzangu amini ya kwamba ndugu yako ni yule ambaye yupo tayari kujitolea kufa kwa ajili ya tatizo lako na siyo kwa ajili ya tatizo lake, mnafiki hujidhihilisha panapotokea tatizo….(wanafunzi walibaki wameduwaa wasijue jamaa anchomaanisha)… hivi ukitaka kujua kama mimi ni ndugu yako wa dhati ninayestahiki upendo wako wa dhati hapa chuoni na popote utakapo niona ungependa kuona nini kutoka kwangu au labda nikufanyie nini?...(wanafunzi wote walibaki wakiangaliana pasipo kupata jibu)…Jamaa aliuliza hivi ni nani anaye mfahamu XXXX yule msichana mrembo ambaye mara nyingi huwa nipo nae cafeteria na maeneo mengine hapa chuoni? Kila mtu alionesha kumjua msichana huyo anyezungumziwa na jamaa….
  ….NAMKUMBUKA…
  Jamaa aliuliza swali linguine ni nani aliyewahi kukiona kitambulisho chake cha chuo au hata mahali anapoishi hapa chuoni?( Kila mmoja hakuwa na jibu japo alifahamika hapo chuoni) Ndugu zangu wanafunzi kitambulisho chako ndicho kinacho kutambulisha uhalali wako wa kuwepo eneo hili la chuo na mahali popote pale huendeko ukitaka kujua uhalali wa wewe kuishi eneo husika lazima uwe na kitambulisho cha eneo husika….. Nawashukuru sana ndugu zangu wanafunzi kwa kuwa mlionesha upendo wa dhati kabisa kwangu pale nilipo ondokewa na wazazi wangu na kipindi chote niwapo hapa chuoni ila….( Jamaa alisita kidogo kisha machozi yakaanza kumlengalenga kisha akaendelea) kwa sasa mimi sina wazazi na mlezi wangu mkubwa ni bibi yangu aliye kijijini na mara nyingi alikuwa akinihusia mjukuu wake nisome kwa bidii ili niweze kumwokoa na umasikini aliokuwa nao, yeye ndiye aliyekuwa akinitumia pesa mara kwa mara ninapokuwa na upungufu wa pesa hapa chuoni ila…..(Jamaa alisita tena kisha machozi yalionekana kumtiririka dhahiri na hapo ndipo wanafunzi wengine nao wakaanza kulia japo hawajui nini kinachomliza jamaa yangu)…..
  ….NAMKUMBUKA…
  Aliendelea:; Yule msichana ambaye mlikuwa mkiniona nae mara kwa mara siyo mwanafunzi wa chuo hiki na wala sio mwanafunzi wa chuo chochote hapa jijini hapa yule alikuwa na CHANGUDOA alifanikiwa kunilaghai na kuniachia zawadi hii ya ugonjwa hatari wa UKIMWI ambao leo ndiyo imekuwa zawadi ambayo natoka nayo hapa chuoni..( eneo zima lilizizima kwa vilio akiwemo na muhusika wa stori hii, baada ya kama dakika tano hivi ndipo hali ya utulivu ikatawala eneo lile na jamaa akamaliza kwa kusema..) Ndugu zangu wanafunzi KITAMBULISHO CHAKO NDIO UTAMBULISHO WAKO HAPA CHUONI NA MAHALI POPOTE ULIPO kisha jamaa alikaa chini kwa masikitiko makubwa kabisa huku akionesha kujutia kupita kiasi….
  *************************MWISHO WA STORI**************
  *****JAMANI EEEE! UKIMWI UPO KAMA HUAMINI HATA STORI HII NAYO HAIJAKUSAIDIA?******
   
 2. Kurzweil

  Kurzweil JF-Expert Member

  #2
  Aug 31, 2012
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 4,875
  Likes Received: 4,718
  Trophy Points: 280
  Dah good story ingawa ilipofika katikati nikajua mwisho wa story ukoje. Swali kama huyo dada alikua changudoa ilikuaje aache kazi zake huko mitaani aje chuo kikukuu kujifanya mwanafunzi ili apate mgao wa jamaa (boom)
   
 3. k

  king roja Senior Member

  #3
  Aug 31, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 143
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Gud story i love it
   
 4. f

  fidelis zul zorander JF-Expert Member

  #4
  Aug 31, 2012
  Joined: Mar 6, 2012
  Messages: 679
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Dah somo zuri sana mwanangu..tunashukuru sana tumekupata..
   
 5. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #5
  Aug 31, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Umalaya unauwa
   
 6. Babarita

  Babarita JF-Expert Member

  #6
  Aug 31, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 374
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Una kipaji. vp Shigongo bado hajakuona tuuu?
   
 7. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #7
  Aug 31, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  Shigongo @ work.
   
 8. K

  Kibulu Member

  #8
  Aug 31, 2012
  Joined: Aug 17, 2012
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha sana ndugu zangu hasa tunaoenda kuanza vyuo(first year) jamaa katoa picha halisi ya maisha yalivyo huko vyuoni kazi kwetu vjana wenzangu.ukimwi upo na kikulacho ki nguoni mwako. Enjoy your bachelor
   
 9. R

  Rebo's Member

  #9
  Aug 31, 2012
  Joined: Aug 23, 2012
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Vishule vya shuleni!
   
 10. The Don

  The Don JF-Expert Member

  #10
  Aug 31, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 3,455
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Good sms
   
 11. by default

  by default JF-Expert Member

  #11
  Aug 31, 2012
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hata wanafunzi wana ukimwi ahache kusingizia dada poa ,kila mtu atavuna alichopanda uwezi vuna maharage kwenye shamba la mpunga
   
 12. NingaR

  NingaR JF-Expert Member

  #12
  Aug 31, 2012
  Joined: Apr 15, 2012
  Messages: 2,836
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  May GOD guide us and leads our path
   
 13. M

  MKINDE Member

  #13
  Aug 31, 2012
  Joined: Aug 16, 2012
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  wana JF espicial first year jitahidi kumjua mwanachuo mwenzako kwa kutumia kitambulisho chake akileta longo longo kuwa nae makini unaweza ukawa unaishi na kibaka au changudoa ndani ya room yako bila kujua, mimi nilishawahi kushuhudia jamaa akilia baada ya kuibiwa laptop yake na kibaka aliyekuja kulala room kwake akidai yeye ni mwanafunzi wa main compus enzi zileee naishi mabibo hostel. KUWA MAKINI tusije tukajibu kale ka methali ka MAJUTO NI.......
   
 14. K

  Kchibo Member

  #14
  Aug 31, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 72
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Umenianzishia siku na ujumbe mzuri sana, TRUST NOBODY inapobidi vaa boot{kinga}.
   
 15. A

  Apex JF-Expert Member

  #15
  Aug 31, 2012
  Joined: Jul 31, 2012
  Messages: 429
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Somo zuri sana kaka,najua chuon kuna kila aina ya mambo yote so guys take care.
   
 16. majany

  majany JF-Expert Member

  #16
  Aug 31, 2012
  Joined: Sep 30, 2008
  Messages: 1,199
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Na tatizo la wanachuo hupenda kuuza mechi....kuwa makini...AIDS is real...tk cr
   
 17. July Fourth

  July Fourth JF-Expert Member

  #17
  Aug 31, 2012
  Joined: May 2, 2012
  Messages: 2,288
  Likes Received: 546
  Trophy Points: 280
  very touching

   
 18. fanson

  fanson Senior Member

  #18
  Aug 31, 2012
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 181
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Word of truth
   
 19. P

  Prince sax de lizzy Member

  #19
  Aug 31, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  maneno ya dhahabu kwa kweli
   
 20. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #20
  Aug 31, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  ​WORDZ.....................Shigongo hajaiona tu hii utakula bingo
   
Loading...