First in Africa Boeing 787 Dreamliner ET Unajua trip yake ya kwanza? Kilimanjaro! Ya kwetu?

Maskini nchi yangu Tanzania tumefikia hatua ya kusifia siyo kwa kununua ndege mpya bali kwa kutua kwenye uwanja wetu!!!!!! Lini tutanunua yetu.

Hata hivyo, naomba nimfahamishe Mleta Uzi kwamba Rais Paul Kagame anazo mbili Boeing 787 Deamliner mpya na anasubiri ya tatu. Zote zinatumiwa na Rwandair. Sisi tutaendelea kununua mitumba ya Forker za piston engine na Beoing 737-200 zilizoundwa miaka ya 70 iliyoshindikana kwa wenzetu.

Si kweli mkuu,fanya reseach vizuri utang'amua hili,taarifa ya uhakika toka Boeing ni kwamba kwa sasa ni Ethiopian Airlines na shirika moja la ndege la Japan linaitwa ANA ndio wanamiliki Dreamliner, waethiopia waliweka oda ya Dreamliners kumi na hiyo ndio wamepatiwa ya kwanza imetoka mwezi March,inawezekana Rwandair wameweka oda pia (sina uhakika na hili) lkn bado hawajapata,hapa Africa ni waethiopia tu ndio wenye hiyo ndege
 
Maskini nchi yangu Tanzania tumefikia hatua ya kusifia siyo kwa kununua ndege mpya bali kwa kutua kwenye uwanja wetu!!!!!! Lini tutanunua yetu.

Hata hivyo, naomba nimfahamishe Mleta Uzi kwamba Rais Paul Kagame anazo mbili Boeing 787 Deamliner mpya na anasubiri ya tatu. Zote zinatumiwa na Rwandair. Sisi tutaendelea kununua mitumba ya Forker za piston engine na Beoing 737-200 zilizoundwa miaka ya 70 iliyoshindikana kwa wenzetu.

Aisee kwa Africa Ethiopia ni nchi ya kwanza kumiliki hiyo toleo 787 dreamliner, kwa Asia ni Japan Europe hakuna nchi inayomoliki toleo hili. America ndio watengenezaji. Mkuu fuatilia Rwanda hawana hiyo kitu boeing 787 Dreamliner. najua wana boeing nyingine lakini si hili toleo.
 
AIR TANZANIA[Wings of Kilimanjaro]
mimi huwa sipendi ku-generalize mambo kwani kwa kufanya hivyo nitashindwa kufanya critical analysis ya issue.
Nisingependa kwenda ndani sana kuhusu shirika letu kwani kufanya hivyo inawezekana ni kupoteza muda tu kwani jamvi letu siku hizi limebadilika sana wengi wetu tunapenda kutrivialize au kuingiza siasa na unazi.
Ukiangalia kwenye maelezo ya shirika letu lilivyoanza 1977, tulikuwa na asset kubwa ya 'technical manpower' na ukiacha zile ndege tulizorithi, serikali juu ya ugumu wa uchumi lakini ili invest kiasi kikubwa cha resources kwa ATC. Shirika hili lilipewa base kia ambako kulikuwa na hata nyumba nzuri tuu kwa wafanyakazi.
Katika kipindi kile, kwa vile serikali ilikuwa haina wataalam wa mambo hayo ilikuwa inawasikiliza sana ATC. Kilichotokea ndani ya ATC ni infighting for power between senior guys. kabla ya hapo wakati wa EAA Kulikuwa na Commercial Director ambaye ni mtanzania na ilitazamiwa huyu ndiye angekuwa boss wa shirika jipya lakini hakupewa nafasi hii na walioshinda ni wale waliojipendekeza ili waonekane ni wazalendo halisi ndiyo walifanikiwa.
Pili Tanzania ilikuwa na uhusiano mzuri sana na uholanzi na ilikuwa na mkataba nao wa kifundi. Kupitia shirika la KLM ilipendekezwa kuwe na ushirikiano wa karibu sana na shirika letu. wazo hili serikali yetu ilitaka ushauri toka kwa wataalam wake ambao ni viongozi wa ATC nao kwa vile hawakutaka kuingiliwa walipendekeza serikali ikatae mpango huo kwa vile eti tunajisheleza. [kama tungekubali kuingia nao ubia KLM leo tungekuwa kwenye nafasi ya KQ]
Matatizo yalianzia hapo internal politics ikafanya serikali kujiingiza ndani.
Kosa kubwa ambalo serikali ililifanya ni kusimamisha mafunzo ya technical staff na shirika lisingeweza kuhimili gharama hizo.
Kwa ufupi, tatizo hili lilianza pale ubinafsi ulipoingia ndani ya shirika [kwa bahati mbaya waliokuwa wakijipendekeza serikalini ndiyo waliokuwa wanashinda. Kuna kipindi ATC ilifanya vizuri kiasi likiwa chini ya bw. mwapachu na hata mzee Sanare lakini wakati hao wanaingia it was too late to change the speed towards self destruction.
Nimeandika haya machache nikifahamu kuwa kuna wanajamii wanaofahamu zaidi na kama wakichangia something will come of this ili tupate alternative option how best should we do to make ATC flourish in african skies.
TACHE KULAUMU TUU KWA KWANI HATA CHIZI ANAWEZA KUFANYA HIVYO
 
Tangazo limekaa swanu.

Sisi tukitangaza utaona mtu kamweka mkewe na jisura baya kwenye tangazo,
aidha tangazo linakuwa la kiloko mpaka nchi nzima tunaona aibu.

Si kwamba hatuwezi bali tumewaachia wasiweza watuwezeshe jambo ambalo ni sawa na kujifanyie uhuni sisi wenyewe.

Kweli nimeona kwenye kalenda zao, nimeona aibu kuiweka ofisini, nikaipeleka nyumbani, watoto wakasema walichosema, (wana mtindo wa kuomba mwaka ukiisha wajaladie vitabu na madaftari yao) hakuna aliyeiomba, sikumbuki iko wapi!
 
Hili ni vema likajadiliwa kisiasa, WaEthiopia wamenunua ndege ya kisasa kabisa nje ya Japan na ya kwanza ya aina yake Africa, unaajua trip yake ya kwanza? Kilimanjaro, huwezi kuamini dlegetion ya viongozi na media from all over the world: Angalia hapa:
BBC News - Ethiopia gets first Boeing 787 Dreamliner in Africa

Air Tanzania itanunua lini ndege zake used maana TZ tunaongoza kwa Mitumba! I am not proud of this, but it worth saying.
'PESSIMIST'
 
Leo hii hao hao waliohoji ndiyo wanaponda kwa hoja kwamba ndege haiwezi kuwa kipaumbele nchi hii yenye shida lukuki.

Wabongo ni "undefined walking objects(UWO)". na ili uwaongoze kwa mafanikio unatakiwa kwanza uwa-ignore.
 
Maskini nchi yangu Tanzania tumefikia hatua ya kusifia siyo kwa kununua ndege mpya bali kwa kutua kwenye uwanja wetu!!!!!! Lini tutanunua yetu.

Hata hivyo, naomba nimfahamishe Mleta Uzi kwamba Rais Paul Kagame anazo mbili Boeing 787 Deamliner mpya na anasubiri ya tatu. Zote zinatumiwa na Rwandair. Sisi tutaendelea kununua mitumba ya Forker za piston engine na Beoing 737-200 zilizoundwa miaka ya 70 iliyoshindikana kwa wenzetu.
Leo tumenunua bado mnalalamika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom