First class travel for spouse of retired prime minister and assistant | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

First class travel for spouse of retired prime minister and assistant

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KALABASH, Dec 13, 2011.

 1. K

  KALABASH JF-Expert Member

  #1
  Dec 13, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 465
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Nikiwa napitia "THE POLITICAL SERVICE RETIREMENT BENEFITS ACT 1999" nimekutana na vifungu vingi lakini kifungu kifuatacho imebidi nikilete jamvini kupata maoni yenu:

  SECTION 14(4): "If the former Prime is requested by the Government to travel outside the united Republic the appropriate authority shall meet all FIRST CLASS travelling expenses which shall cover expenses for his spouse and one assistant."

  Kwa Rais mstaafu ni spouse na two assistants. Kwa Makamu wa Rais mstaafu ni spouse na one assistant. Wana JF mna maoni gani kuhusu hili mkizingatia kuwa hivi karibuni TANZANIA tume -graduate kuwa namba tatu katika kundi la mataifa OMBA OMBA(Saidia maskini baba!) duniani?
   
 2. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #2
  Dec 13, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ni vizuri kuwaenzi wetu waliolitumikia taifa kwa utendaji uliotukuka. Bila wao Tanzania isingeongoza kwa kuwa mabwana wengi wanaotupenda na kutupa misaada. Wao ndiyo wanaopaka wanja na kupendeza hadi kina CAMERON wanalegea na kutudondoshea misaada kama mvua.
   
 3. T

  Topical JF-Expert Member

  #3
  Dec 13, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hii sheria ina upendeleo sana..

  Besides hawa jamaa hawajawahi kuchangia kwenye mifuko ya ustawi wa jamii halafu wanapata all this amount..

  sijui tunatoa wapi pesa za mchezo hivi
   
 4. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #4
  Dec 13, 2011
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Kuna umuhimu wa kureview sheria ya mafao ya viongozi kwani wako wengi mno na mzigo wa kuwalea umeishakuwa mzito kwa sisi tunaopata mlo mmoja kwa sikui. Moreover hii sheria inawalinda hata viongozi walioachia madaraka kwa kashfa!!
   
 5. p

  politiki JF-Expert Member

  #5
  Dec 13, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Haya ni matumizi mabaya ya fedha za wananchi ktk nchi maskini kama Tanzania lakini inaonekana kama matumizi haya yatafanyika tu endapo kiongozi huyo atakuwa requested na serikali kusafiri nje ya nchi kwahiyo kinachoitajika kufanyika ni kujaribu kuzuia uhitaji huo wa kiongozi kusafiri kwenda nje unless ni safari ambayo ina manufaa makubwa kwa nchi yetu.
  kulingana na kipengele cha hapo juu kwa maoni huyo kiongozi anastahili kulipiwa vitu hivyo endapo serikali yenyewe inataka
  kumtumia badala ya yeye kufanya kazi zake nyingine kwani yeye ni prvate citizen ana majukumu yake mengine pia hilo swala
  la wasaidizi wake labda lingeitaji mabadiliko kulingana na umuhimu wao.
   
 6. p

  politiki JF-Expert Member

  #6
  Dec 13, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  kwako kalabash,
  asante sana kwa info. naomba kujua kama hizo info. zinapatikana online naomba na link please nataka niangalie sheria inasemaje kwa
  kiongozi wa zamani aliyetoka madarakani kwa kuhujumu nchi kama Lowassa ni sheria inasemaje kwamba pamoja na kuisababishia nchi hasara kubwa bado tu tunapaswa kumpa mafao yake pamoja na kwamba ameujumu nchi mpaka akalazimika kuwa kicked out.
  sheria inasemaje endapo kiongozi wa zamani ataitia nchi yetu aibu let say kwa wizi au ubakaji je sheria inasemaje nchi itaendelea kumlipa pamoja na kwamba ameipaka mavi nchi yetu ??
   
 7. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #7
  Dec 13, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,318
  Likes Received: 610
  Trophy Points: 280
  Ni upon request by the govt, lakini unawezakuta hata ziara za Lowasa kwa yule nabii wake Nigeria tunazilipia sisi.
   
 8. K

  KALABASH JF-Expert Member

  #8
  Dec 13, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 465
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mkuu Mwita25
  umefanikiwa kuigeuza hoja nzito kuwa nyepesi! Sawa Waziri mku mstaafu kusafiri FIRST CLASS ingawa hao MABWANA unaowataja wenyewe hawasafiri kwa daraja hilo! Je na mke na msaidizi wa mstaafu vilevile? Nipe justification badala ya kuzungumzia mambo ya kupaka wanja
   
 9. K

  KALABASH JF-Expert Member

  #9
  Dec 13, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 465
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Nashukuru sana Politiki kwa kuonyesha interest katika hoja hii niliyoiombea maoni/michango. Kwa bahati mbaya nimekwisha toka ofisini ambako nilikuwa nachambua Act yenyewe ikiwa in book form. Nitajitahidi kesho kuisoma zaidi na kukutaarifu. Hata hivyo jaribu ku google under THE POLITICAL SERVICE BENEFITS ACT 1999 huenda ukaikuta.
   
 10. p

  politiki JF-Expert Member

  #10
  Dec 13, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  kwa mtu yeyote ambaye yuko interested link ya habari hii ni Eastern African Centre for Constitutional Development - Home ni ajabu Rais wa Tanzania ana benefit package
  nzuri kuliko Rais wa USA . the law is silence in what happened when the leader has been removed from the office like in case of Lowassa
  or anyone who has been convicted of crime after leaving the office ?
   
Loading...