Fireboy, Rema na Joeboy wameibuka kwenye mziki wa Nigeria na wanatamba sana

Pass Master

Member
Sep 18, 2020
94
58
Fireboy DmL,Joe Boy,Rema

Kwa sasa kwenye mziki wa Nigeria kuna Wasanii wameibuka na wanafanya vizuri sana Kama Rema,Joeboy,Fireboy au Mayorkun, N.k

Rema alitamba sana na EP ya Bad Commando ambayo ilipelekea raisi mstaafu Barack Obama kuiitaja ngoma yake ya Iron Man kwenye Playlist yake. Rema anafanya vizuri pia...

Joe Boy mdundo wa Baby umesumbua sana na ngoma nyingine nyingi kama Don't Call me Back akiwa na Mayokurn na zingine nyingi ambazo zimefanya vizuri.

Nimewasikiliza Wengi Lakini huyu Fire Boy DML kwa nionavyo ni zaidi ya wote,Fireboy DmL ni zao la Olamide....Anafanya vizuri mno Alianza kutamba na mkwaju wa Jeaulos.

Album zake mbili zimefanya vizuri Sana.

Album ya Laughter,Tears&Goosebumps Album hii imebeba midundo kama Need You,Vibration,Jeaulos,What if say,King zote ziache kuna mdundo unaitwa Wait and see🙌🙌 N.k

Juzi tu ameachia album ya Apollo kuna midundo kama Champions,Tattoo,Afar ft Olamide,New york city girl...

Dogo anaimba sana pia Lyrics zake ni nzuri......

Nafikiri Fireboy DmL ni zaidi yao Wadau mnaonaje?

Ni muda wa kina Marioo kutafuta Collaboration na watu kama hao.
 

Attachments

  • images.jpeg
    images.jpeg
    17.9 KB · Views: 9
JoeBoy ndio mpango mzima;- ngoma kama 'Baby', 'Call', 'Beginning' na 'Don't call me back' nnaweza nikazisikiliza siku nzima bila kuzichoka. Rema naona kama yuko overrated
 
JoeBoy ndio mpango mzima;- ngoma kama 'Baby', 'Call', 'Beginning' na 'Don't call me back' nnaweza nikazisikiliza siku nzima bila kuzichoka. Rema naona kama yuko overrated
Mfuatilie na Fireboy utakubari,Joe pia yupo fresh.....Mi Rema namuona wakawaida tu...
 
Wakati tunampa point nyingi joeboy tukumbuke vile vile yeye kaingia kwenye game kabla ya hao wadogo zake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom