Finn’s Facts: Ignore Zitto Kabwe and Dr Idris Rashidi’s pro-Dowans talk | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Finn’s Facts: Ignore Zitto Kabwe and Dr Idris Rashidi’s pro-Dowans talk

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Mar 2, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,780
  Likes Received: 83,135
  Trophy Points: 280
  Finn’s Facts: Ignore Zitto Kabwe and Dr Idris Rashidi’s pro-Dowans talk

  Finnigan Wa Simbeye
  THIS DAY

  KIGOMA North legislator Zitto Kabwe, in a rare move, has decided to join forces with Tanzania Electric Supply Company Managing Director, Dr Idrisa Rashidi, to allegedly pressure the Government into using our vital tax money to buy second hand Dowans Holdings’ turbines at an inflated price of 60bn/-.

  Mr Kabwe who has managed to pull crowds of voters in his favour because of his steadfast arguments and anti-graft stance both in parliament and in public rallies, has joined Dr Rashidi, a former Bank of Tanzania governor and an alleged beneficiary of over 13bn/- radar procurement scandal from BAE Systems.

  Kabwe has gone out of his way in trying to convince the public that Dowans’ turbines are good after all, despite all the scandals and thieving tactics associated with the company and its predecessor, Richmond Development Company.

  The youthful legislator has even suggested that the 2004 Public Procurement Act be amended to allow the Government buy the used Dowans Holdings turbines, which has a capacity of 40 megawatts, because the country is heading towards a spiraling electricity demand.

  Dr Rashidi says currently Tanzania uses 700MW of electricity per annum which is short of the actual demand which he said needs an extra 105MW of energy.

  Annually, argues the man who in some countries would not be in office, the country’s electricity demand increases by between 15 and 20 percent.

  Very convincing arguments by the learned Tanesco boss and his new-found bedfellow, Kigoma North legislator, but certainly not to Parliamentary Energy and Minerals Committee Chairman, William Shelukindo.

  The veteran Bumbuli legislator argues that even if necessary, buying used Dowans turbines is contrary to the 2004 PPA.

  Most of us queue behind Mr Shelukindo and although Kabwe has on several occasions been a public favourite when debating important national issues, this time around he risks losing his grip on the electorate who will question his sincerity in supporting this latest attempt by Dowans to sell us used turbines.

  There is no question that this country needs more power generation which will not necessarily come from Tanesco, bearing in mind that the 2008 Electricity Act deregulated the energy sector which has since seen serious committed private energy companies such as Artumas Tanzania Limited.

  Tanesco’s Rashidi and Chadema’s Kabwe should be encouraging Energy and Minerals Minister, William Ngeleja to speed up the process of drafting regulations to the new energy law so that serious private investors and not greedy businessmen, find their way into the local market and burden consumers.

  Rashidi and Kabwe should be telling Ngeleja and other stakeholders to get down seriously and return Kiwira Coal Mines Limited back to the Government and invest in electricity generation instead of allegedly touting for Dowans’ turbines.

  Rashidi and Kabwe should be advising Dowans to get serious and enter the local energy market which has since been liberalized, other than argue to convince tax payers that our vital money should be used to purchase second hand turbines from a scandalous company contrary to the law.

  For the time being, the public and Government can comfortably ignore the duo and let them do the Dowans touting which is good for their jobs.
   
 2. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Inaonekana Zitto ni secret admirer wa Ngelaja (na wizara yake kwa ujumla). Nakumbuka kuna wakati Zitto msifu sana Ngeleja na akamshauri ahame CCM.
   
  Last edited: Mar 2, 2009
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,780
  Likes Received: 83,135
  Trophy Points: 280
  Utata wa Dowans: Shelukindo asema serikali inatia hofu

  • ASHANGAA SERIKALI KUAMUA MNUNUA MITAMBO

  Exuper Kachenje
  Mwananchi
  Date: 3/1/2009

  SAKATA la ununuzi wa mitambo ya ufuaji umeme wa dharura ya kampuni binafsi ya Dowans Tanzania Limited, jana liliendelea 'kupandisha presha' wakati Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini ilipoeleza hofu kuwa imezungukwa na serikali baada ya suala hilo kuwasilishwa kwenye kamati nyingine ya taasisi hiyo ya kutunga sheria.

  Kamati ya Nishati na Madini iliishauri serikali kuwa isinunue jenereta hizo za kufua umeme kwa kuwa kufanya hivyo ni kukiuka Sheria ya Manunuzi ya Umma, inayozuia kununuliwa kwa mitumba, lakini sasa serikali imewasilisha suala hilo kwenye Kamati ya Bunge ya Mahesabu ya Serikali, kamati inayoonekana kuunga mkono kununuliwa kwa mitambo hiyo.

  Kugeuka huko kwa serikali, ambayo ilishaeleza mwaka jana kuwa haina nia ya kununua mitambo hiyo na ambayo ilivunja mkataba na Dowans Agosti mosi mwaka jana, kumechukuliwa na kamati ya nishati na madini kuwa ni kigeugeu na kuwazunguka wabunge.

  Akizungumza na Mwananchi jana, mwenyekiti wa kamati hiyo ya nishati na madini, William Shelukindo alisema anashangazwa na hatua ya serikali kukimbilia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma katika suala hilo na kwamba kamati yake inajiuliza mazingira yaliyotumika.

  "Nashangaa hatua hiyo ya serikali ya kutumia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma katika kutafuta na kufanya ununuzi wa mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura imekujaje," alisema Shelukindo.

  "Hatuelewi ni katika mazingira gani wanaweza kushughulikia suala hilo kwa kutumia kamati hiyo inayoweza kushughulikia mambo mengine hata kuiacha kamati husika... hili linatia hofu na nalishangaa kwani limefanyika mimi nikiwa nchini Zambia kwa shughuli za kamati."


  Alisema baada ya kurejea jana asubuhi kutoka Zambia, amekuta hali hiyo na kwamba mambo yote yanayohusu hatua za kupata mtambo wa dharura wa kuzalisha umeme ilibidi yapelekwe kwenye kamati yake.

  "Tunajiuliza maswali mengi, kwani awali Tanesco ilikuja kwetu wakaeleza mengi kuhusu mustakabali na azma yao, tukayapokea kama kamati na bunge likatoa mapendekezo kwa serikali, sasa kama kuna lolote inabidi yaletwe kwetu na serikali," alisema Shelukindo ambaye ameonekana kuwa na msimamo katika suala la ununuzi wa mitambo ya Dowans.

  "Hii inaweza kusababisha hisia za kuzungukwa kwani waziri alistahili kurudi kwetu na kutusikia... tungemshauri na kupendekeza nini cha kufanya... kama kuna suala jingine, alete kwetu kuliko kupeleka kwingine. Hii inawachanganya wanachi," alisema Shelukindo.


  Shelukindo, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bumbuli mkoani Tanga, alisema kamati yake ilitaka kujua Tanesco na Dowans wanavyodaiana, suala ambalo kamati yake ilikuwa inasubiri na serikali haijasema wala kueleza lolote iwapo kuna haja ya kurudi katika kamati yake na kushughulikia suala hilo.

  Akizungumzia taarifa zinazodai kuwa mitambo ya Dowans ilishanunuliwa na serikali muda mrefu na kinachofanyika sasa ni taratibu tu za kubariki kitendo hicho, Shelukindo alisema hana hakika na taarifa hizo.

  Hata hivyo, alisema kazi ya kamati yake ni kupokea mambo, kuyajadili na kutoa ushauri na mapendekezo yake kwa serikali, na kwamba haiwezi kuingilia utendaji.

  Shelukindo alisema ataliwasilisha suala hilo leo kwa spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samuel Sitta na kuzungumza naye kuona namna watakavyowaondolea wananchi mkanganyiko huo.

  "Kesho (leo) nitakwenda kwa spika... nitampelekea suala hili, nitazungumza naye tuone namna ya kuwaondolea wananchi mkanganyiko na utata kuhusu hatua hiyo ya serikali," alisema Shelukindo.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali na Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe alikaririwa na Mwananchi Jumapili akisema kuwa "katika suala hili, lazima tuangalie faida na hasara" na kuongeza kwamba wataalamu wa Tanesco wamechunguza na kuona mitambo hiyo inauzwa kwa bei nafuu na kwamba iko katika hali nzuri.

  Katika mahojiano hayo maalum, Zitto alisema kuwa kamati yake imeona umuhimu wa serikali kununua mitambo ya Dowans baada ya kuridhika na maelezo ya Tanesco.

  Alisema kuwa moja ya vigezo vya Tanesco vya kuhalalisha kununua mitambo hiyo ni janga kubwa la ukosefu wa umeme, linalolikabili taifa sasa na hata miaka ijayo. Tanesco imeeleza kuwa mahitaji ya umeme yamekuwa yakiongezeka kwa wastani wa megawati 100 kila mwaka, huku kukiwa na uwezekano wa baadhi ya vyanzo vya nishati hiyo kushindwa kuzalisha umeme.

  Mitambo hiyo ya Dowans ililetwa nchini mwaka 2006 baada ya kampuni iliyopewa tenda hiyo, Richmond Development Company LLC kushindwa kutekeleza jukumu lake la kuleta mitambo ya kufua umeme wa dharura baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili.

  Hata hivyo, serikali ilivunja mkataba na Dowans Julai mwaka jana, ikieleza kuwa taratibu za Sheria ya Manunuzi ya Umma hazikufuatwa wakati wa kuipa Dowans mkataba, ikidai utata wa uhalali wa usajili wa Kampuni ya Richmond na hivyo kuutangaza mkataba wake kuwa batili, hali iliyobatilisha hata mkataba wa Dowans.

  Baada ya habari kuvuja kuwa serikali ilikuwa na mpango wa kuinunua mitambo ya Dowans, watendaji wakuu wa Tanesco na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja walikanusha vikali kuwepo mpango huo, hadi suala hilo lilipoibuka tena mapema mwaka huu wakati waziri na Tanesco walipotoa hoja nzito za umuhimu wa serikali kununua mitambo hiyo.
   
 4. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #4
  Mar 3, 2009
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Katika jambo hili kijana mwenzetu zitto ameamua kuwa mkweli rohoni na hadharani, nimemkubali kwa sababu amekataa kuwa mnafiki mbele ya umma.

  Tumuuunge mkono tu mtumishi huyu wa umma
   
 5. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #5
  Mar 3, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  hapa zitto ndo hoja nafikiri kwa sasa kutokana na msimamo wake. nina wasiwasi sana na wabu nge wa ccm na utendaji wao wa KINAFIKI NA KIGEUGEU. hawana msismamo hata siku moja wao ni USHABIKI TUUUUU. Hili suala TANESCO hawana haja ya kutegemea mawazo potofu ya kamati ya madini na nishati ambayo imejaa vigeugeu na wapenda sifa za muda mfupiii. suala la nishati ni nyeti na naomba siasa ziwekwe pembeni na UTAALAMU UFANYE KAZI YAKE.

  Kama MD wa tanesco anatudanganya basi atawajibika kwa makosa yakee na timu yake.
  Zitto nampongeza ameamua kuwa muwazi kwa masilahi ya taifa. miytambo ya dowans wabunge hao wa kamati ya madini na wapambe wao wanahisi ni ya rostam kwa hiyo serikali ikinunua atafaidi RA.

  kwa hili kwa maono yangu, uwezo wa watendaji wa kisiasa kufikiri na uwezo wa mgt ya tanesco chini ya dk huyo idirisa natumai watavutanaaaa mpaka mgao utukuteeee.
  lazima tuwe na uwezo wa kufanya maamuzi mazito (bold actions) na sio kulialia tuuuu..

  mwakyembe ndo nimemshangaa anadai zitto anaendeleza kampeni sangaraaaaaaaaaa.....lol!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 6. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #6
  Mar 3, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  hapa zitto ndo hoja nafikiri kwa sasa kutokana na msimamo wake. nina wasiwasi sana na wabu nge wa ccm na utendaji wao wa KINAFIKI NA KIGEUGEU. hawana msismamo hata siku moja wao ni USHABIKI TUUUUU. Hili suala TANESCO hawana haja ya kutegemea mawazo potofu ya kamati ya madini na nishati ambayo imejaa vigeugeu na wapenda sifa za muda mfupiii. suala la nishati ni nyeti na naomba siasa ziwekwe pembeni na UTAALAMU UFANYE KAZI YAKE.

  Kama MD wa tanesco anatudanganya basi atawajibika kwa makosa yakee na timu yake.
  Zitto nampongeza ameamua kuwa muwazi kwa masilahi ya taifa. miytambo ya dowans wabunge hao wa kamati ya madini na wapambe wao wanahisi ni ya rostam kwa hiyo serikali ikinunua atafaidi RA.

  kwa hili kwa maono yangu, uwezo wa watendaji wa kisiasa kufikiri na uwezo wa mgt ya tanesco chini ya dk huyo idirisa natumai watavutanaaaa mpaka mgao utukuteeee.
  lazima tuwe na uwezo wa kufanya maamuzi mazito (bold actions) na sio kulialia tuuuu..

  mwakyembe ndo nimemshangaa anadai zitto anaendeleza kampeni sangaraaaaaaaaaa.....lol!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 7. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #7
  Mar 3, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Duu? kweli tuna tofautiana sana... yaani hata kama Zito katokosa tumuunge mkono tu? binafsi kwa hili nasema a big No!, Mh Zito alipaswa kuiasa serikali ifanye maandalizi ya kukabiliana na hali hii ya upungufu wa nishati unao tegemewa, kwa kubuni njia mbadala za solar, wind mills, na hata kurudisha kiwira yetu na kuifanya productive lakini siyo swala la kuchukua 'ndoo yetu pekee ya maji tuliyo baki nayo'tukaimwage tena kwenye bahari ya DOWANS! HAILIPI KABISA!
   
 8. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #8
  Mar 3, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Ni kweli, hata Mkapa na Yona wakati wanajiuzia Kiwira walifanya maaamuzi mazito wakiwa wanafahamu nafasi zao. Pia wote kina Balali na wote walioshiriki kwenye wizi wa epa pamoja na twin towers walifanya maamuzi mazito (BOLD ACTIONS). I wonder how bold should it be for public interests.

  Maamuzi mazito wanafanya watu wengi, vibaka wote na wezi wote wanafanya maamuzi mazito (BOLD DECISIONS) kwani wanajua kuwa ni ama kuishi au kufa.

  Ni kweli maamuzi mazito (BOLD DECIONS) siku zote yanakuwa pale watu wanapopanga jinsi ya kuliibia taifa, km rada, ndege, epa, richmond, na sasa dowans etc!

  Kwanini haya maamuzi mazito yasitumike kuanzisha "scheme za umwagiliaji" tukaondokana na njaa milele?

  Kwanini haya maamuzi mazito yasifanyike katika mfumo wa utawala ili kila mmoja ajue cheo ni dhamana?

  Kwanini haya maamuzi mazito yasifanyike kubadilisha maisha duni ya wananchi wetu vijijini wanaolaziishwa kuchangia shule za voda faster na zahanati zisikowa na vifaa wala waalimu? NI KWELI NI MAAMUZI MAZITO!

  Kwanini hayo maamuzi mazito yasifanyike ili wote wanaohusika na uharamia wa mali ya watanzania wakawajibi kwa mujibu wa sheria

  Kwanini hayo maamuzi mazito yasifanyike nchi iwe na katiba iliyohuru na inayotoa fursa sawa wote?

  Ni mengi unaweza kusema katika hili, ila inashangaza kauli yako "MAAMUZI MAZITO"!
   
 9. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #9
  Mar 3, 2009
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Kwa hili Zitto katokota na kuuonyesha kuwa ni Ma*****ya wa kisiasa na huko mbele ya safari anaweza kufanya maajabu ya kutuliza, maamuzi mazito ambayo watanzania tunayataka ni kusikia kuwa sasa tunalipa pesa kuirudisha Kiwira yetu na kuikarabati wenyewe ili ianze kufanya kazi, Maamuzi mazito tunayotegemea ni kama yale ya mwalimu Nyerere aliposema watanzania fungeni mikanda miezi 18 ya hali ngumu baada ya vita ya nduli Amini, hapa wangesema tufunge mikanda hata miaka 18 lakini serikali iweze kufufua Stieglers gorge project na kuweka bwawa pale Rufiji basin ambalo linaweza kutoa zaidi ya 2000MW kwani feasability studies zilishafanyika ni kuendeleza tu, leo ati Zitto anakuja na maamuzi mazito ya ka turbine kanakotoa 100mw, tena toka kwa mwekezaji aliyetuibia ?kuna uzito gani hapo? au akili zenu ndio nzito kujua kuwa watanzania sasa hivi sio wazito wa kuelewa mambo? Zitto kama ukimkamata mgoni kwa mkeo acha sheria ichukue mkondo wake na sio upatane naye kwa vile una shida au u maskini, ni bora kufa na tai shingoni kuliko kunyanyaswa na huyo Dowarns wenu, kwanza katuibia halafu tena tulipe fedha? jamani tunangoja maamuzi mazito na yawe mazito kweli sio masihara mnayotufanyia, Na wewe Zitto kama ni kupotoka basi rudi kundini kwa maneno mawili tu ya kiungwana "naomba mnisamehe" na hapo kina Shelukindo hawatasema kuwa unajifunzia siasa Bungeni-kubali yaishe mwanawane!!!
   
 10. Tuntu

  Tuntu JF-Expert Member

  #10
  Mar 3, 2009
  Joined: Jan 28, 2009
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa ufuasi wa Upofu namna hii Tanzania Yenye Neema Haitawezekana,kumbuka kuwa nae ni binadamu wenye maslahi yake binafsi.......,unanikumbusha enzi zile za fikra sahihi za mwenyekiti...duuh??
   
 11. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #11
  Mar 3, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,585
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Kwa upande wangu naona uamuzi wa kununua au kutonunua hiyo mitambo ya Dowans iko chini ya MD wa Tanesco. Kwa kuwa Dr. Indris Rashid anahitaji mitambo hiyo ili kulinusuru Taifa kwenye tatizo kubwa la umeme, Serikali yetu inapaswa kufanya utekelezaji.

  Nashangaa kuona ili swala linapelekwa kisiasa zaidi kwa Sababu tu ZITTO ameunga mkono mawazo ya Dr. Idris Rashid, kinachotakiwa ni utekelezaji wa haraka katika mambo ya kiufundi/technical na sio kuleta Siasa kwenye masuala nyeti kama haya.
   
 12. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #12
  Mar 3, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  nashukuru umeelewa kwa mapana maana ya ''bold action''.
  Nakubaliana nawe kwamba maamuzi mazito yanahitajika kila eneo lenye kuleta tija na maendeleo katka maisha ya watanzania. Tatizo la viongozi wetu hawataki kufanya maamuzi hayo kwa kupenda ama ubinafsi au zaidi cheap popularity!!!!

  Kama taifa sasa yabidi tuondokane na kulalamika na kuhamasika kuleta maendeleoo.
  Matatizo ya umeme nchi hii yanajulikana kuanzia ukiritimba mbovu wa tanesco( kuzalisha, kusambaza umeme), uongozi dhaifu, overstaffed, unskilled labour nk.....

  Kiongozi makini lazima afanye maamuzi hapoo kuanzia ya kisera na utendaji.
  Ni ndoto kwa mfumo wa sasa wa tanesco kujiendesha kwa ufanisi na wananchi wengi kupata huduma hiyo muhimu ya nishati. Kumbuka muswada wa kuondoa ukiritimba wa utendaji ulikwama bungeni.....siasa iliwekwa mbelee zaidi ya utaifa..

  Kwa hiyo kwa hili la mitambo ya dowans kama wataalamu wa tanesco wameshauri tununue...je sisi tushauri vipi (hapo zitto ana hoja)
  kwa taarifa tanesco walishamlipa consultancy na ametoa ripoti yake hiyooo

  jamani kama taifa tunahitaji kusonga na maamuzi mazito ni muhimu.
  Ndo maana yalifanyika hapo nyuma na la msingi ni kuyarekebisha kila wakati.
  Mfano ubinafsishaji ni moja ya maamuzi mazito..

  Na kiongozi makini ni yule mwenye kufanya maamuzi hayo bila woga na kukubali makosa yatokanayo nayoooooo....(hapo ben aliweza)
   
 13. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #13
  Mar 3, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Tatizo langu ni uswahiba uliopo baina ya Zitto na huyo anayesadikiwa kuwa mmiliki Richmond na baadaye Dowans -- Rostam. Uswahiba huo haupo bayana lakini upo na anaewaunganisha hao wawili ni mhariri mkuu wa media house yake -- Habari Corporation. Kama siku 10 zilizopita Zitto alifika katika chumba cha habari ya media house hiyo mtaa wa Shekilango -- Sinza na kuongea faragha na mhariri huyo kwa masaa zaidi ya mawili -- ofisini mwake, na baadaye alipopaki shangingi lake. walikuwa wanaongea nini? Siku chache baada tu ya mkutano huo, ndiyo tukasmsikia Zitto kawa kipofu na kuanza kutetea ununuzi wa Dowans.
   
 14. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #14
  Mar 3, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mimi bado sijaona uzito wa uamuzi wa kununua ama kutokununua mitambo ya Dowans. Kama ningekuwa na maamuzi, ningesema outright kuwa tuachane nayo na tutafute mingine haraka sana. Ningeshauri tuachane nayo kwasababu kwanza iliingia TANESCO kwa njia za miujiza miujiza (bila kufuata taratibu wala sheria za manunuzi ya umma), pili TANESCO ina case mahakamani na sasa imeamua kuchukua uamuzi wa kuizuia, tatu ilionekana kuwa bei ya mitambo ile ni kubwa kuliko mitambo kama hiyo kutoka kwa manufacturer (kwa mujibu wa Kamati ya Bunge iliyoongozwa na Mwakyembe). Nne, kama kulikuwa na haja ya kuwa na mitambo kama hiyo, kwa nini haikununuliwa baada ya hii ya DOWANS kuonekana imenunuliwa kimakosa mwaka mmoja uliopita?

  Wakuu, sijasikia popote ambapo maelezo ya kina ya sababu za kuinunua mitambo hii midogo ya 100MW (isiyotosha), iliyonunuliwa bila kufuata sheria zaidi ya kuwa tunategemea upungufu wa umeme na kauli za mabishano za wanasiasa.

  Kinachotakiwa sasa, ni kuangalia kama mitambo hiyo imesafishwa kisheria, na kuwa sasa inaweza kutumiwa na TANESCO bila kukiuka taratibu zozote za manunuzi ya umma. Pia ingekuwa vyema kujua kama ikinunuliwa mingine (mipya) kihalali, itagharimu bei gani hadi kufika nchini na kufungwa, na itachukua muda gani kufika na kufungwa ili iweze kutumika (badala ya hii iliyotumika).

  Haiingii akilini kuona na kusikia viongozi wakishabikia kuvunja sheria ili kukidhi mahitaji yasiyotosheleza haja na yasiyoeleweka vizuri.
   
 15. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #15
  Mar 3, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu shutuma zako kali sana. Unajua unaweza kumsababishia mwanasiasa kijana kupotea kabisa katika ulimwengu wa siasa kama hayo ulioyasema hapo juu yataweza kuthibitishwa?

  Kama uliyosema ni kweli, basi tumekwisha. Maana hata wale ambao wanaomba wananchi wawape nafasi ya kuomba uongozi wakiwa wanafanya vitendo hivyo mapema namna hiyo, basi wananchi hawatakuwa na haja ya kusikia lolote kuhusu upinzani, na na kuhakikishia, upinzani hautapona. Inahitaji wapinzani wachache sana kuonekana mafisadi ili kuumaliza upinzani wote. Mkuu, kama uliyosema ni kweli, basi hatima ya upinzani katika siasa za nchi inakaribia ukingoni. Sitaona jinsi hata mmoja wao atakavyopata kura za kurudi Bungeni.
   
 16. M

  Mugerezi JF-Expert Member

  #16
  Mar 3, 2009
  Joined: Mar 28, 2007
  Messages: 454
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mimi sioni tatizo la Zitto kwani yeye ametoa mawazo yake so ni kazi yetu sisi kuyafanyia kazi na kama ni mazuri tuyachukue lakini kama ni mabaya tuyaache. Jamaa ameshaur kununua mitambo iliyotumika kwa maono yake yeye hiyo ni solution ya haraka lakini pia inabidi tutoe solution kama kununua mitambo mipya au kutangaza tenda ili kampuni nyingine zije. Lakini kumbuka mtu akiumwa na nyoka akiguswa na jani anaruka baada ya makosa yaliyofanyika its like jamaa wanaogopa kurudi kule kule kwani viongozi wetu wao wanaenda na watu wanasemaje au kimeandikwa nini. Pia nikifanya hiki jamaa watasema. Mimi kwa upande wangu zitto simlaumu yeye hayo ndiyo mawazo yake si lazima yafanane na yangu.
   
 17. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #17
  Mar 3, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Kite, maneno mazito hayo umeandika. Nafikiri wahusika wakisoma watafanyia kazi maana kweli heri kusota miezi 18 ila hili tatizo la maji na umeme hatimaye limalizwe kabisa kwenye miji mikubwa. Ni aibu eti swala la energy(umeme) hata nalo linatupa shida, tena MIJINI.
   
 18. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #18
  Mar 3, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Zitto naona uko hapa tena.
  Jamani tafadhali, heri TUSOTE ila muweke mitambo mikubwa na ya maana. Ikiwezekana isiwe miwili mikubwa sana ila iwe walau nane (ya kiwango cha kati) na iwekwe sehemu tofautitofauti ili sehemu moja ikikwama basi nyingine ziendelee kufanya kazi. Nilishawahi kusikia balozi mmoja akilalamika kuwa "hii nchi yenu vipi, miaka 40 ya uhuru na mnashindwa kuwa na umeme wa uhakika". Haya mambo ya dharula yalituletea Richmond. Tangu wakati huo kwa nini hawakujenga mitambo ya uhakika kusolve hili swala? Nafikiri ilitakiwa kurudisha Kiwira, kujenga Rufiji basin, na kuweka hayo mapanga boi hapo Singida. Ikiwezekana basi umeme wa ziada uwepo hata kwa miaka 10 ijayo ili kama kukiongezeka mahitaji ya umeme kwa mfano kumejengwa kiwanda basi kusilete shida yoyote.
  Mie nipo nanyi ili muradi hili tatizo LIISHE MILELE. Hata kama ikibidi kula nyasi, acha tule ili muradi SHIDA YA UMEME IWE HISTORIA. Hii mitambo kwa kweli sina imani nayo sana na naona itakuwa "tunakunywa pombe ili kupoteza mawazo. Tukija amka tutaanza kuona double double". VIongozi hatimaye muwe kama WAZAZI, tena mfano mzuri uwe wa Mzee Joseph Jackson, aliyesotesha sana watoto wake ila leo hii JACKSON FAMILY ni jina kubwa sana dunia hii. YES, WE CAN!!!!!!!
   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  Mar 3, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,780
  Likes Received: 83,135
  Trophy Points: 280
  Sheria zilizotungwa za manunuzi ya mitambo haziruhusu ununuzi wa mitambo michakavu. Hakuna sababu yoyote ya muhimu ya kubadilisha sheria hizo. Sasa hivi serikali kwa kushirikiana na TANESCO waanze taratibu za kununua mitambo mipya badala ya kupoteza muda kutaka kununua mitambo ambayo imegubikwa na ufisadi wa hali ya juu na imelingizia Taifa hasara kubwa sana ambayo sijui kama tutairecover toka kwa hao wenye mitambo yao.
   
 20. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #20
  Mar 3, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Nguvu za Dowans ni kali, zapofua uongozi Tanesco

  2009-03-03 11:01:11
  Na Muhibu Said


  Nguvu za kampuni ya kuzalisha umeme ya Dowans, zimeifumba macho menejimenti ya Shirika la Umeme nchini (Tanesco) kiasi cha uongozi huo kuipuuza Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika hilo la umma, Nipashe imeelezwa.

  Habari za kiuchunguzi na vyanzo vya habari ndani ya Tanesco vimeithibitishia Nipashe kwamba Menejimenti ya shirika hilo pekee na kongwe la kuzalisha nishati ya umeme nchini, ilitangaza mapendekezo yake ya kutaka kununua mitambo ya kufua umeme wa dharura ya Dowans huku ikijua fika Bodi ilikuwa imetoa maelekezo kadhaa ya kuzingatiwa kabla ya tangazo hilo.

  Chanzo chetu cha habari kutoka ndani ya Tanesco kinaeleza kuwa miezi minne iliyopita bodi ilitoa maagizo matatu muhimu kwa menejimenti ya Tanesco, lakini hadi mwezi uliopita uongozi huo uliposema bado unafukuzia mitambo ya Dowans, ulikuwa haujatekeleza hata agizo moja.
  Hatua hiyo ya menejimenti ya Tanesco ambayo imeibua mjadala mkali miongoni mwa Watanzania na kuwagawa wabunge makundi mawili kupitia Kamati za Bunge, inaelezwa kuwa imeishtua Bodi hiyo.

  Kikao cha Bodi kilichofanyika Desemba 12, mwaka jana, kilihitimishwa kwa kwa kuiagiza menejimenti ya Tanesco kuteua wajumbe wawili kutoka Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kwa ajili ya safari ya kwenda Houston, nchini Marekani kuangalia bei ya mitambo kama ile inayomilikiwa na Dowans.

  Ilielezwa kuwa agizo hilo lilitolewa kutokana na taarifa ambazo Bodi inazo, kwamba mitambo kama ile inayomilikiwa na Dowans, inauzwa kwa Dola za Marekani milioni 14 wakati mitambo ya kampuni hiyo, ambayo ni michakavu Tanesco wanataka kuinunua kwa Dola milioni 30, yaani zaidi ya mara mbili ya bei halisi.

  ``Hata hivyo, menejimenti ya Tanesco haikutekeleza agizo hilo,`` kilieleza chanzo chetu ndani ya Tanesco.


  Mbali na agizo hilo, Bodi pia iliitaka menejimenti ya Tanesco kukumbuka ushauri uliotolewa kwake na wanasheria wa shirika hilo kwamba kampuni ya Richmond ni hewa na mkataba na mitambo ya Dowans imetokana na kampuni hiyo, hivyo chochote kinachotokana na Dowans pia kitakuwa na utata.

  Chanzo hicho kimesema kwamba Bodi waliiagiza menejimenti ya Tanesco iwasiliane na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili kupata uhalali wa mitambo ya Dowans, ambayo imeirithi kutoka Richmond, pia waombe marekebisho ya sheria ya manunuzi.

  ``Lakini menejimenti ya Tanesco hawakufanya hivyo, badala yake wakaamua kutoa tangazo kwenye vyombo vya habari kutaka Bodi iidhinishe ununuzi wa hiyo mitambo ya Dowans. Bodi imeshtuka sana,`` kilieleza chanzo hicho.


  Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Adola Mapunda, alipoulizwa na Nipashe jana, alisema hawezi kuzungumza lolote kwa vile suala hilo liko mahakamani.

  Kutokana na kauli ya Mapunda, hata uongozi wa Tanesco haukupaswa kuzungumzia wala kutangaza mipango ya kununua Dowans hadi kesi dhidi ya shirika hilo imalizike.

  Wakati hayo yakijiri, habari zilizopatikana jijini Dar es Salaam jana zinaeleza kuwa Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa leo kukutana na viongozi na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini, ikiwamo menejimenti ya Tanesco na huenda hoja kuhusu Dowans ikawemo katika orodha ya mambo yatakayojadiliwa katika kikao hicho.

  Jumamosi wiki iliyopita, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Dk. Idris Rashid, alitoa taarifa kwenye vyombo vya habari kueleza hali ya umeme katika Gridi ya Taifa pamoja na mambo mengine, akapendekeza kuwa mtambo wote wa Dowans ununuliwe na serikali pamoja na vifaa vyote vya kuunganishia kwenye gridi.

  Hata hivyo, wakati Tanesco ikitoa taarifa hiyo, Mbunge wa Kyela Dk. Harrison Mwakyembe, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, alikaririwa na Nipashe akisema kuwa ni vigumu kununua mitambo ya Dowans kwa sababu licha ya kukiuka Sheria ya Manunuzi ya Umma na maazimio ya Bunge, kampuni hiyo imefungua kesi dhidi ya serikali na Tanesco katika mahakama ya usuluhishi huko Paris, Ufaransa.

  Kutokana na hali hiyo, Dk. Mwakyembe alisema anashangazwa na hatua ya Tanesco kung`ang`ania mitambo ya Dowans, wakati tayari wamiliki wake wamewashtaki serikali na Tanesco huko Ufaransa.

  Wakati Dk. Mwakyembe na kamati yake wakipinga vikali suala hilo, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, wiki iliyopita alikaririwa na vyombo vya habari akibadilisha msimamo wa awali wa serikali wa kutonunua mitambo ya Dowans kwa kusema kwamba, uamuzi huo si ufisadi.


  SOURCE:
  Nipashe

  Duu, yaani Bodi ilimwambia Idris akaangalie mitambo USA na jamaa akagoma na sasa anataka kusema muda hautoshi ili anunue hii mitambo. Kila kitu sasa kiko wazi. Nani anamtunza Idris kwa uzembe wa namna hii? Pinda amuwajibishe au Pinda akatae kazi maana huu sasa ni ........ (sijui niseme neno gani maana zaidi ya tusi, sina jingne). Nafikiri kuna watu wana agenda ya siri. Zitto, huu mradi ni FEKI. Ukiukumbatia basi utakubeba kaburini la kisiasa. Acha mitambo hiyo IOZE hapo na wasipokuja kuichukua mapema, waanze kulipia pesa kwa mitambo yao kukaa hapo Ubungo. Bei iwe nzuri tu kwa upande wetu.
   
Loading...