T14 Armata
JF-Expert Member
- Mar 7, 2017
- 10,650
- 34,926
Mojawapo ya sababu za kuvunjika kwa USSR ni Waarabu. Marekani ilihakikisha OPEC wanazalisha mafuta mengi kwenye soko la dunia, mafuta yakawa mengi bei ikaporomoka, Soviet Union iliyotegemea mafuta na gesi kwenye uchumi wake ikapungua mapato. Kule Afghanistan kulianzishwa Mujahideen wapigane na USSR, Marekani kuona hivyo ikawapa silaha hasa MANPADS wapige helicopters za Urusi. Mwishowe wakaondoka Afghanistan na miaka michache wakavunja muungano wao.ikifika muda mtamkosoa tu Putin , km mzungu alifungua Afrika ili kutimiza mahitaji yao , amin hawawez kukosa solution kwenye hili , solution ikipatikana itakuwa ni mwendo wa kumsusia Urusi , waarabu wakipata akili tu basi Urusi hana chake
Waarabu walikuwa watu muhimu kwa USSR hata silaha waliuziwa nyingi, kina Hafez al Assad (baba yake Bashar) na Saddam Hussein wakawa wanazitumia wanafeli ila USSR inasema tungekuwa nazo sisi wenyewe tungeshinda, nyinyi hamfanyi training ipasavyo. Leo hii pale Ukraine vifaru vya Urusi vinashiriki kwenye turret throwing championship.
Kwa sasa kina UAE wananunua Rafales kutoka Ufaransa, Qatar inanunua F-16 za Marekani, Saudi Arabia ndio kabisa ina kila kitu kutoka Marekani. Kidogo Egypt ndio inapenda silaha za Urusi ila nayo mwaka huu imefanya cancellation ya jets. Waarabu wanapunguza kuitegemea Russia