Financial Times: Marekani haiwezi kuwalinda marafiki zake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Financial Times: Marekani haiwezi kuwalinda marafiki zake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Feb 8, 2011.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [​IMG]Gazeti maarufu la Financial Times limeandika kuwa, mabadiliko katika nchi za Kiarabu ni jambo lisiloepukika na kwamba Marekani haiwezi kuwasaidia chochote marafiki zake yaani watawala wa nchi za Kiarabu.
  Gazeti hilo limechapisha makala likizilaumu nchini za Magharibi kwa kuwa na misimamo ghalati kuhusiana na ulimwengu wa Kiarabu na huku likiashiria wimbi la mwamko wa Waislamu katika nchi za Kiarabu limeandika: Machafuko yanayoendelea Misri, mapinduzi ya Tunisia, maandamano ya Yemen na hali isiyotabirika ya Iraq yote hayo yanabainisha kuwa Wamagharibi wanakabiliwa na hali ngumu sana hivi sasa kutokana na mahesabu yao mabaya ya kuwapa nguvu watawala wasio na uungaji mkono wa wananchi.
  Makala ya gazeti hilo imeongeza kuwa, kama ambavyo hivi sasa kunakaririwa makosa yale yale yaliyopelekea wananchi kuchoshwa na kuamua kumiminika mitaani kupinga tawala zao, sehemu kubwa ya ulimwengu wa Kiarabu haina chama madhubuti cha kisiasa wala uongozi makini wa kuweza kuunganisha watu na kuondoa hitilafu za kikabila.
  Vile vile limeandika, asilimia kubwa ya wananchi wa nchi za Kiarabu ni vijana, na tawala za nchi zao zinashindwa kuwaandalia nafasi za kazi suala ambalo linazidisha hasira za wananchi.
  Weledi wa mambo wanawalaumu wachambuzi wa nchi za Magharibi wanaojaribu kupotosha wimbi la harakati za kimapinduzi za wananchi Waislamu wa Mashariki ya Kati, wakisema kuwa pamoja na kwamba ugumu wa maisha umechangia kuzuka wimbi hilo, lakini kudhalilishwa mafundisho ya dini yao ya Kiislamu na kitendo cha watawala wa nchi za Kiarabu cha kuwa vibaraka wa Magharibi kinaonekana ndicho kilichotoa msukumo mkubwa wa kuzuka na kuendelea wimbi hilo la mapinduzi.
   
Loading...