Finally naanza upya maisha ya kujitegemea nikiwa mfukoni nina laki 8 tuu

Negative people are more dangerous than snakes. Mkuu kikubwa uwe na maono, plan kwa utulivu na kisha kua na nidhamu ya plan zako.. hakuna lisiloshindikana. Ng'ang'ana, mwombe mungu na usikubali kukatishwa tamaa. Mwaka mmoja uliopita nilikua katika hali mkanganyo yako chamtoto tofauti kabisa na nilipo leo. Na kila nilipokua nnajaribu kuwashirikisha watu juu ya plan zangu na kile nilichonacho mkononi nilipokea sumu za kutosha na wachache walinitia nguvu. Kama ilivyo mguu wako ndio unakupangia size ya kiatu na si kiatu kupanga size ya mguu, kile kilicho akilini mwako ni muhimu katika safari yako kuliko kilicho mawazoni mwa watu juu yako. Kila laheri Soja
 
Ngoja nikupe ramani

Kuna dogo mmoja juzi Kati katokea huko usukumani kapita hapa kwetu tumepa hii ramani hapo dar ana miezi Kama 7 hivi anakomaa na mji haombi hata dala ya kula

Asubuhi Sana anaibukia pale soko la ilala sio karume naaminisha ilala wanapoanza fungua zile balo za nguo anachagua zake zile Kali .

Anazipunguza kwa saizi ya wastani anaenda home anazifua na kupiga pasi saafi (mashati na suruali)

Anatembeza mitaa ya K/Koo yote

Dogo kapanga mbagala dar live kule analipa Kodi 25 na maji na umeme jumla Kama 40 hivi

Mtaji wa dogo buku 50 tu

Huo mji ukijifanya brazameni unakufa njaa
 
Awe na kazi asiwe na kazi kitendo cha kupewa 8kilos kwa mtu anaejitambua anatoboa,but I can see hajazoea huyu kaka maisha ya kujitafutia kazoea kupewa kila kitu bamkubwa anamfunza maisha anaona anaonewa loooh!!!
Kuna watu wametoka home kwao hawana senti Leo wako mbaali.
Dogo ajipange sana
Mkuu mtu mwenye miaka 35 unaweza kumuita Dogo?
 
Pole na hongera.
Hiyo laki nane si hela nyingi.

1: Usikimbile suala la kuoa

2: Nusu ya hiyo hela ichukulie kama mtaji. Angalia kwa eneo ulilopo, unaweza kufanya nini kikakuingizia pesa kidogokidogo. Jifunze kwa yeyote anaefanya vizuri. Weka mtaji wako nusu 200,000/=, wakati hiyo nyingine 200, 000/= ukiangalia mwenendo wa kazi yako. Ukiona inakwenda vyema, utaongeza mtaji kwa kadri.

3: Hiyo 400,000/=, 150,000/= nunua mahitaji mhimu ya maisha. Hasa chakula, luku na maji kama ni ya kulipia ili vitoshe kwa miezi mitatu hata minne. 50,000/= vitu vidogovidogo utakavyohitaji kwa kila siku.
200,000/= iweke kama akiba yako. Utaipunguza pale ambapo kuna suala la muhimu kweli.

4: Kuwa na nidhamu ya matumizi ya hela uliyonayo kama vile ukijua kuna siku ngumu zinakuja mbele. Nunua kitu ambacho ni muhimu na kinahitajika kweli kwenye maisha yako.

5: Weka kumbukumbu ya kila unachokifanya kwa pesa yako.

6: Ukipita kwa kiasi humo, kufeli au kufanikiwa kwako hautaulaumu sana utendaji wako binafsi.

7: Tafakali kwa kina na tahadhali kwa kila utapohitaji kutumia hela yako.
Ushauri mzuri sana juu ya matumizi mazuri ya pesa!
 
Tayari umelipiwa kodi miezi 6 (nusu mwaka)
Umepewa cash Tshs 800,000/=
Kama ulivyosema anza kuchukua hatua Mkuu

Usisubiri kutiwa moyo!! Huna sababu ya kukata tamaa bado.

Acaha kuseek emotional support mkuu huwa haisidii...
Tuendelee kupambana Mkuu
 
Back
Top Bottom