Filikunjombe@ work: Apiga STOP halmashauri kuwatumikisha wananchi kujenga barabara za Mwenge! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Filikunjombe@ work: Apiga STOP halmashauri kuwatumikisha wananchi kujenga barabara za Mwenge!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kiganyi, May 18, 2012.

 1. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  MBUNGE wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe(pichani) amepinga vikali uamuzi wa mhandisi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Baraka Mkuya kuwatumikisha wananchi wa kijiji cha Masimbwe katika ujenzi wa barabara ya Halmashauri kwa ajili ya mbio za mwenge.

  Mbunge Filikunjombe alifikia uamuzi huo wa kuzuia wananchi kuendelea kutumikishwa kazi za ujenzi wa barabara za wilaya bila malipojuzi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo baada ya wananchi kuhoji sababu za kutumikishwa kujenga barabara za wilaya bila malipo huku shughuli nyingine za uzalishaji mali zikiendelea kusimama.

  Wakizungumza katika mkutano huo wananchi hao walisema kuwa pamoja na jitihada zinazofanywa na mbunge wao kupambana na vitendo vya ufisadi kwa ngazi ya Taifa ila bado kuna ufisadi wa kutisha ambao umekuwa ukifanywa katika ngazi ya vijiji ambao umekuwa ukiwatesa wananchi na kujiona kama ni watumwa katika nchi yao ukiwemo huo wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa kuwatumia wananchi kujenga barabara za wilaya ambazo kimsingi zinatengewa bajeti .

  Mkazi wa kijiji hicho Jonh Mwasanga alisema kuwa katika kijiji hicho wananchi wamekuwa wakishindwa kufanya kazi zao za kilimo kutokana na kila siku kutakiwa kwenda kutengeneza barabara ya wilaya kwa ajili ya mbio za mwenge na kumtaka mbunge wao Filikunjombe kutolea ufafanuzi .

  Mkazi huyo alisema pamoja na kuchangiswa michango kwa ajili ya mbio hizo za mwenge ila bado wananchi wamekuwa wakitakiwa kushiriki katika ujenzi wa barabara hiyo jambo ambalo wamedai kuwa ni kunyanyaswa na uongozi wa wilaya ya Ludewa .


  Afisa mtendaji wa kata ya Mlangali Edward Makamba akizungumzia suala hilo alisema kuwa maeneo mbali mbali ya vijiji wananchi wamekuwa wakitumika kujenga barabara za wilaya .

  Hivyo alisema kuwa kwa kuwa maofisa watendaji wa vijiji na kata ni watekelezaji wa maagizo ya mkurugenzi wa wilaya hivyo walikuwa hawajui kama kuwatumikisha wananchi katika ujenzi wa barabara ni kosa.

  Mbunge Filikunjombe akijibu madai ya wananchi hao alisema kuwa ni kinyume na utaratibu kwa wananchi kutumikishwa kutengeneza barabara za wilaya na kuwa utaratibu uliopo ni wananchi kutengeneza barabara za vijijini na sio za wilaya ambazo zinatengewa bajeti.

  Hivyo alisema suala hilo atalifuatilia kwa kina hata ikiwezekana kwenda kuonana na mkurugenzi ama waziri wa wizara hiyo John Magufuli.

  Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Monica Mchiro alipoulizwa juu ya suala hilo alisema kuwa atalifanyia kazi zaidi ili kujua ni bajeti kiasi gani ilitengwa kwa ajili ya barabara hiyo ya wilaya .


  SOSI; Fransis Godwin!
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  Safi sana Deo H.F
   
 3. B

  Bob G JF Bronze Member

  #3
  May 21, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Tabia hii ya kutumikisha wananchi imekua nikawaida coz wakubwa wanakula hela ya barabara na kulazimisha wananchi kujenga kwa lazima. Kweli nimeamini. NCHI INAJENGWA NA WENYE MOYO NA KULIWA NA WACHACHE WENYE MENO
   
 4. kinya

  kinya JF-Expert Member

  #4
  May 21, 2012
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 482
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Safi sana jembe japo upo kwenye worse timu!
   
 5. O

  One Man Army JF-Expert Member

  #5
  May 21, 2012
  Joined: Dec 27, 2011
  Messages: 238
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  welcome chadema bwana deo filikunjombe...
   
 6. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #6
  May 21, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Huu ujinga wa wananchi kutumikwisha na kuchangishwa michango isiyo pua na mdomo ilisha kwisha kwenye jimbo la Mh. Tundu Lissu. Deo learn from Tundu Lissu, it is unconstitutional! Tetea wapiga kura wako, wewe ni Mbunge tofauti na wabunge wengi wa magamba.
   
 7. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #7
  May 21, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,990
  Likes Received: 2,649
  Trophy Points: 280
  Huyu jamaa ndio mbunge pekee wa CCM mwenye akiri,haogopi ubazazi wa magamba maana ni watu wa vitisho sana,hongera sana Deo.
   
 8. agatony8l

  agatony8l JF-Expert Member

  #8
  May 21, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hakika Deo wale waliokuwa wakifikiri sahihi ya kutokuwa na imani na WM ilikuwa utapeli hawakujui vizuri keep it up! Mapambano ni popote! Wakitaka kukuletea zao njoo M4C
   
Loading...