Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,484
- 40,988
Mbona kasha irusha clip Facebook angalieni, nasari anasikika akisema kigoma inaweza kutoa rais baada ya miaka 5,10 au 15 hajasema 2015 ivo walicho kanusha ni kweli Gonga hapa umsikie Alichokisema Mhe. Joshua Nassari-Kigoma - YouTube
Nimeisikiliza hiyo clip.
Tukitaka kuwa wakweli, sidhani kama ni sahihi kumlaumu mwandishi wa gazeti la Mwananchi na Bwana Zitto. Hapa siongelei kama Zitto anafaa kuwa Rais au hapana lakini naongelea juu ya ukweli kama Nasari alitamka au hakutamka kuwa Zitto anafaa kuwa Rais. Japo mwandishi hakunukuu neno kwa neno kama alivyotamka Nasari lakini kwa tafsiri pana inaonesha ndivyo alivyokusudia.
Kwenye hili siwezi kumlaumu mwandishi wa gazeti la mwananchi wala Zitto. Nitamlaumu Zitto kama itadhihirika kuwa Nasari alifanya hivyo kwa kuombwa afanye hivyo na Zitto lakini nayo haitaingilia akilini maana Nasari ni mtu mzima tena mbunge ambaye anaowawakilisha wanaamini ana akili, utashi na busara.
Ningekuwa Nasari, nisingehangaika kukanusha maana tofauti ya alichotamka na kilichoandikwa gazetini ni ndogo sana, hasa katika mtazamo wa kisiasa. Kunaweza kuwa na tofauti kubwa kwenye mtazamo wa kisheria.
Zitto alikuwa sahihi kutamka kuwa hawa watu walitamka ila haieleweki kwa nini wanakanusha. Kwa sababu lile lilikuwa ni tamasha, kuna wengine huenda walikwishapitia Serengeti na safari lager au baada ya kuona umati wa watu, wakatokwa na maneno ambayo baadaye baada ya kurudiwa akili hawakuweza kukumbuka kwa nini waliyasema. Tulihangaika sana kuhakikisha Nasari anaupata ubunge lakini sishawishiki sana kama kweli huyu kijana ni makini na ana hekima ya uongozi maana hata ile kauli yake ya kuasema atatangaza Arusha kuwa nchi ilitutia kinyaa. Leo tena anatamka halafu anakanusha. Tumefanikiwa kuongeza mbunge toka Arumeru Mashariki lakini siamini kama tumeongeza nguvu ya maamuzi ya busara bungeni na nje ya bunge.