Filikunjombe: Sikwenda Kigoma kumsafishia yeyote njia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Filikunjombe: Sikwenda Kigoma kumsafishia yeyote njia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Muke Ya Muzungu, Jul 25, 2012.

 1. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2012
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Mh. Mh. Deo Filikunjombe amestushwa sana na swala la yeye kumsafishia Zitto njia ya Urais. 'Hayo ya Zitto ni ya kupikwa, something wrong somewhere" Anashangaa kwa nini kawekewa maneno mdomoni ambayo namna au nyingine imemdhalilisha kwa wapiga kura wake na kuonekana kama kibaraka fulani?

  Atazungumza na waandishi wa Habari/atatoa tamko lake hivi karibuni. Mh. Jembe Mh. Deo Filikunjombe anasema kwamba ametumwa na watu wake kuwawakilisha na siyo kuzungumzia mambo yasiyo na msingi tena ya kuropokwa.hakwenda kigoma mumsafishia yeyote njia... Stay tuned.

  source mshirika wa Mheshimiwa
   
 2. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #2
  Jul 25, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,250
  Likes Received: 3,863
  Trophy Points: 280
  Haya sasa, mimi binafsi bila kumung'unya maneno nilishasema na nitasema daima (mpaka siku ABADILIKE) kuwa Zitto Kabwe ni MNAFIKI, na ni kijana hatari kwa mstakabali wa taifa letu kidemokrasia!

  Sipingi wazo/ndoto yake ya kuwa rais bali njia anazotumia kuifikia ndoto hiyo ni ya kipuuzi na haikubaliki tuikemee na kuipinga, italiingiza taifa hili kwenye machafuko,

  Atambue kuwa yeye amebeba dhamana ya tumaini la vijana wengi tena wakware wa fikra machipuko ambao ni hatari zaidi hasa walishwapo hata uongo tu!

  Propaganda zake na ccm za kuivuruga chadema zimekuwa zikimulikwa usiku na mchana na kila hatua ya unyayo wake inahesabiwa kwa umakini mkubwa!

  Wenzake ndani ya chadema wapo kila kona ya Tz wakikijenga chama (M4C) tena kwakujitolea wakila kwa mama ntilie, lakini yeye hata siku moja hajahudhuria mikutano ya chadema tangu alipoenda Songea na Mwanza kuipiga kampeni za udiwani mwezi wa pili kama si kosei! Amekuwa ni mtu wa ziara binafsi tu kila wiki yupo kwenye ndege, hana tofauti sasa na Rais wetu kwa ziara zilivyo:

  Hivyo arejee kwenye mikingamo huru ya chama na tafakuri sahihi za ukombozi mororo bila kutumia mbinyo wa kuligawa taifa kwa makundi ya vijana, wazee na watoto!

  Tunataka taifa lisimame pamoja, liongee lugha moja na litamalaki pamoja, huku tukijisifu uwepo wa uongozi safi wa kijana mwenzetu Zitto Zuberi Kabwe!!
   
 3. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #3
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sema juu ya hayo mambo mie siyajui, ila lisemwalo lipo.....
   
 4. y

  ycam JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2012
  Joined: Mar 17, 2012
  Messages: 757
  Likes Received: 748
  Trophy Points: 180
  Naona kama Zitto anahukumiwa haraka mno kabla ukweli wote haujajulikana. Tusubiri tuone na kuisikia hiyo video ya tukio zima, kisha tutajua nani anasema uongo.
   
 5. Collins

  Collins Senior Member

  #5
  Jul 25, 2012
  Joined: Jul 19, 2012
  Messages: 145
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zitto bila kuleta video uliyoahidi basi inaonekana live umenunua front page ya gazeti
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #6
  Jul 25, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,250
  Likes Received: 3,863
  Trophy Points: 280
  Hivi unaamini watu watatu tena wawili wa chama chake na mmoja wa chama kinge wote wamkane mtu mmoja?

  Duuuh una roho ngumu wewe! Haya suri videmo za pinako zilizochakachuliwa kuhalalisha uongo! Wenzio wapo studio mida hii
   
 7. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #7
  Jul 25, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,250
  Likes Received: 3,863
  Trophy Points: 280
  Bado ipo studio inafanyiwa mavocaling kuingiza sauti tuzitakazo!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. Collins

  Collins Senior Member

  #8
  Jul 25, 2012
  Joined: Jul 19, 2012
  Messages: 145
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  alisema ataweka kwenye blog lake.....nashangaa kule kwenye blog lake kuna video za tamasha iliyofanyika na ameupload tar 19/07/2012.......sasa hii video yake ya hawa wabunge walisema haya maneno kwanini haikuwekwa.
   
 9. F

  FJM JF-Expert Member

  #9
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hivi hata akileta video hali itatuwama?

  Akikaka kimya watu watatafsiri kuwa alinunua waandishi wa habari, na akileta video si tu atakuwa anakubaliana na waliyosema wabunge vijana kuhusu urais wake, lakini pia atakuwa ameleta hali ya mvurugano ndani ya vyama viwili, CCM na CHADEMA. Maana hao wabunge watakuwa wameenda kumpigia campign mtu nje ya utaratibu wa vyama vyao. Very unfortunate!
   
 10. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #10
  Jul 25, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,250
  Likes Received: 3,863
  Trophy Points: 280
  Hapo ndipo utata, mimi namshauri atulie afanye kama "ni upepo tu hali itatulia"!
   
 11. Collins

  Collins Senior Member

  #11
  Jul 25, 2012
  Joined: Jul 19, 2012
  Messages: 145
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Video zikichakachuliwa utaona hawa wengine wanakuja kukanusha tena.,,,,safari bado ndefu
   
 12. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #12
  Jul 25, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,250
  Likes Received: 3,863
  Trophy Points: 280
  Haahaaaha duuuh lakini mwisho wa siku ataatikana mshindi, lakini mpaka hapa misheni ya ZK imeshafeli sasa aangalie plan B
   
 13. M

  Mbozib JF-Expert Member

  #13
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Zito kabwe tulia acha papara urais si mchezo muone mwenzako jk anavyo umbuka.
   
 14. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #14
  Jul 25, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Zitto Kabwe Kumbe ana nia ya kuiua CDM huyu kijana ana tamaa ya hela sana Chama kilichochukua miaka 20 kukijenga anataka afanye kukivunja kwa masaa mawili huyu kijana wa ccm ni hatari sana CDM wanatakiwa wamuweke under surverlance muda wote
   
 15. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #15
  Jul 25, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
 16. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #16
  Jul 25, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Kidemokrasia Zitto ni positive change Tanzania. Anahamasisha vijana kuwa huru katika kuenjoy haki zao za kikatiba. Sijaona mahali Zitto akikataza watu kuexercise their freedom. Zitto anatuma ujumbe kwa wapenda demokrasia kuwa CHADEMA haina de facto mgombea wa urais na mgombea atapatikana baada ya mchakato maalum unaoheshimu katiba ya chama. Asiyekubali hilo ndio "hatari kwa mstakabali wa taifa letu kidemokrasia!".
   
 17. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #17
  Jul 25, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Kwa bahati nzuri wenzie wameshamjuwa na wanakula na kipofu...hata sisi wananchi wa kawaida wenye uwezo wa kufanya hesabu za kujumlisha na kutoa tayari tuliishaconclude kwani misimamo na affiliation zake zinaonekana wazi....maslahi binafsi kwanza CDM baadaye.
   
 18. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #18
  Jul 25, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Kwa nafasi yake kwenye chama na mategemeo tuliyokuwa nayo kwake si wakati muafaka wa kufanya haya kwa sasa....ni kuhamisha attention za watu toka kwenye kukijenga chama. Ni haki yake muda ukifika.... chochote kilicho mahali pasipostahili ni uchafu.....
   
 19. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #19
  Jul 25, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Hiyo ingekuwa sahihi ingekuwa equillibrium imetulia, lakini hali haiko hivyo. Mijadala ya ndani na nje ya chama imeelekezwa kwenye kumkubali Dr. Slaa kama ndio de facto mgombea 2015. Sasa kuwaambia wengine wakae kimya na kumpigia debe Slaa kuendelee ni kinyume cha demokrasia. Dr. Slaa na washabiki wake wanapaswa kujua kuwa uchaguzi wa 2010 UMEKWISHA, uchaguzi wa 2015 ukianza ni mchakato mpya.
   
 20. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #20
  Jul 25, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,689
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Mkirua,
  Kinachozungumziwa humu ni wabunge kumsafishia njia Zitto. Wabunge wamekana, na wana-JF (baadhi) wame postulate kuwa hii habari Mwananchi wameandikiwa na Zitto (They have their own reasons).

  Zitto naye amesema hajaandika au shurutisha mtu aandike hayo. On top of that, hakutaka kudanganya akasema anayo tape ya wabunge wakiongea kama ilivyonukuliwa na gazeti la Mwananchi.

  Ninavyojua mimi, documentaries huwa zina vi-process fulani kabla hazijawa published, it may take a minute.
  Tusubiri, ila naona wengi wanaenda nje ya mada.
   
Loading...