Filikunjombe azuia halmashauri kuwatumikisha wananchi kujenga barabara za mwenge Ludewa

Hii misafara ya kukimbiza mwenge kwa jicho la upembuzi shamrashamra zake huhitimishwa kwa baadhi ya watu kujamihiana kiholela hasa unapokuwa mkesha wa mwenge katika kituo fulani, na hivyo kusababisha maambukizi ya gonjwa hatari la ukimwi.
 
Nimependa taarifa yako candid scope unaonesha uko karibu sana na mh sasa ebu mwambie akomae pale halmashauri kuna afisa utumishi mmoja mlevi mlevi hivi hana nidhamu ana dharau sana aangalie anaweza akmwadabisha vipi.

Mbona huyo alishamlipua mbele ya waziri alipotembelea huko na kahamishiwa mkoa mwingine.
 
Sijui hata tunaelekea wapi? Yaani mbunge ndio ananunua dawa kwa ajili ya vituo vya afya? Kazi za mbunge hata hazijulikani.

Kwa haraka haraka hata mie ningefikiri hivyo, lakini tukiangalia kazi za wamisionani na mashirika ya dini tungesema kwa mtazamo wako kwamba mbona kazi yao ni kuhubiri dini, iweje wanaendesha shule na vyuo mbalimbali, iweje wanavituo vya afya na hospitali mbalimbali, iweje wana miradi ya kujenga vituo vya umeme kwa ajili ya kusambaza huduma vijijini ambako serikali imewasahau.

Kwa mazingira yetu ya leo na vijiji vyetu ukiangalia maisha yao yanatia uchungu, hivyo mbunge anaona kidogo alicho nacho bora awasaidie watu wake ni sawa na baba anavyomjali mwanaye kuliko kusubiria serikali ambayo inafanya usanii na dhihaka kwa wananchi katika kutoa huduma kwa ahadi za maneno vila vitendo.

Vibabaja alivyoahidi Kikwete viko wapi? Ambulance aliyotoa Filikunjombe ndiyo inayosaidia akina mama wajawazito kuwapeleka vituo vya afya. Tungesema wananchi hao wasubiri vibabaja vya Kikwete matokeo yake majibu unayo mwenyewe.
 
Sijui hata tunaelekea wapi? Yaani mbunge ndio ananunua dawa kwa ajili ya vituo vya afya? Kazi za mbunge hata hazijulikani.

Ukisema hivyo utaharibu maana ya utendaji uliotukuka na kuashiria kuendekeza mfumo wa mchakacho unaendelea uliozoeleka. Zito alivyojitoa mhanga kuiadabisha serikali na hatimaye mawaziri nane kung'olewa, utasema hiyo siyo kazi ya Zito aliyotumwa bungeni, bali kutunga sheria.
 
safi yule jamaa ashawahi kunitukana siku moja usiku kwenye hotel moja pale ludewa nilikuwa pale mjini kikazi hotel ipo karibu na nmb kwa vile ilikuwa ni usiku nikamchunia asubuhi nikawapa kibano wahudumu pale hotelini wakaniambia ni nani ndipo nikamfuata huko halmashauri alikoma.
 
safi yule jamaa ashawahi kunitukana siku moja usiku kwenye hotel moja pale ludewa nilikuwa pale mjini kikazi hotel ipo karibu na nmb kwa vile ilikuwa ni usiku nikamchunia asubuhi nikawapa kibano wahudumu pale hotelini wakaniambia ni nani ndipo nikamfuata huko halmashauri alikoma.

Ulifanya vema, bora ulituliza mzuka usiku ule pale hotelini na kisha kwa busara kesho yake ukamfuata kazini kwake kumwadabisha kitu ambacho kama ana akili timamu aliaibika kwa wafanyakazi wenzake kufanya jambo isivyo busara kwa mtu asiyemjua.
 
Back
Top Bottom