Filikunjombe azuia halmashauri kuwatumikisha wananchi kujenga barabara za mwenge Ludewa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Filikunjombe azuia halmashauri kuwatumikisha wananchi kujenga barabara za mwenge Ludewa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, May 19, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  MBUNGE wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe(pichani) amepinga vikali uamuzi wa mhandisi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Baraka Mkuya kuwatumikisha wananchi wa kijiji cha Masimbwe katika ujenzi wa barabara ya Halmashauri kwa ajili ya mbio za mwenge.

  Mbunge Filikunjombe alifikia uamuzi huo wa kuzuia wananchi kuendelea kutumikishwa kazi za ujenzi wa barabara za wilaya bila malipojuzi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo baada ya wananchi kuhoji sababu za kutumikishwa kujenga barabara za wilaya bila malipo huku shughuli nyingine za uzalishaji mali zikiendelea kusimama.

  Wakizungumza katika mkutano huo wananchi hao walisema kuwa pamoja na jitihada zinazofanywa na mbunge wao kupambana na vitendo vya ufisadi kwa ngazi ya Taifa ila bado kuna ufisadi wa kutisha ambao umekuwa ukifanywa katika ngazi ya vijiji ambao umekuwa ukiwatesa wananchi na kujiona kama ni watumwa katika nchi yao ukiwemo huo wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa kuwatumia wananchi kujenga barabara za wilaya ambazo kimsingi zinatengewa bajeti .

  Mkazi wa kijiji hicho Jonh Mwasanga alisema kuwa katika kijiji hicho wananchi wamekuwa wakishindwa kufanya kazi zao za kilimo kutokana na kila siku kutakiwa kwenda kutengeneza barabara ya wilaya kwa ajili ya mbio za mwenge na kumtaka mbunge wao Filikunjombe kutolea ufafanuzi .

  Mkazi huyo alisema pamoja na kuchangiswa michango kwa ajili ya mbio hizo za mwenge ila bado wananchi wamekuwa wakitakiwa kushiriki katika ujenzi wa barabara hiyo jambo ambalo wamedai kuwa ni kunyanyaswa na uongozi wa wilaya ya Ludewa .


  Afisa mtendaji wa kata ya Mlangali Edward Makamba akizungumzia suala hilo alisema kuwa maeneo mbali mbali ya vijiji wananchi wamekuwa wakitumika kujenga barabara za wilaya . Hivyo alisema kuwa kwa kuwa maofisa watendaji wa vijiji na kata ni watekelezaji wa maagizo ya mkurugenzi wa wilaya hivyo walikuwa hawajui kama kuwatumikisha wananchi katika ujenzi wa barabara ni kosa.

  Mbunge Filikunjombe akijibu madai ya wananchi hao alisema kuwa ni kinyume na utaratibu kwa wananchi kutumikishwa kutengeneza barabara za wilaya na kuwa utaratibu uliopo ni wananchi kutengeneza barabara za vijijini na sio za wilaya ambazo zinatengewa bajeti.

  Hivyo alisema suala hilo atalifuatilia kwa kina hata ikiwezekana kwenda kuonana na mkurugenzi ama waziri wa wizara hiyo John Magufuli.

  Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Monica Mchiro alipoulizwa juu ya suala hilo alisema kuwa atalifanyia kazi zaidi ili kujua ni bajeti kiasi gani ilitengwa kwa ajili ya barabara hiyo ya wilaya .


  Sura ya mandhari ya Ludewa

  [​IMG]

  Nimekuwa najaribu kupata picha ya hali ya wilaya ya Ludewa ilivyo, nikaambiwa ni ya milimamilima kana nchi ya Uswis vile. Hapa nimebahatika kupata picha moja wapo wadau wanaweza kupata picha ya madhari ya wilaya hiyo yenye utajiri wa malia asili ilivyo.

  [​IMG]

  HIVI NI VILELE VIWILI MOJAWAPO......VYA MWAMBA WA CHUMA "Iron Ore" Ni mojawapo kati ya Utajiri usiooza wa LIGANGA - Wilaya ya Ludewa, Mkoa mpya wa Njombe, wilaya iliyopo ukingoni kabisa mwa Ziwa Nyasa.


   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  May 19, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Anapingana na serikali ya Chama chake wanaotembeza mwenge kuchangisha pesa kwa wananchi.

  Mwenge ulikuwa alama ya ukombozi barani Afrika. Sasa bara zima limekombolewa sasa mwenge huo kazi yake nini kuendelea kutembezwa nchini? Upelekwe kwenye jumba la makumbusho mambo ya kale.
   
 3. N

  Njele JF-Expert Member

  #3
  May 19, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Imekuwaje wanavijiji wasafishe barabara kuu ya wilaya kwa ajili ya kupita mwenge wa CCM? Na wasio wanaCCM wanalazimika kuandaa mapito ya mrija huu wa CCM unaoitwa mwenge kuchangisha mafuta ya mwenge na michango mingine inayoishia kwenye makao ya CCM?
   
 4. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #4
  May 19, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Mambo ya kipuuzi kabisa haya. Mwenge kazi yake nini. Pongezi kwako Deo.
   
 5. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #5
  May 19, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Deo yuko sahihi,ila subiri atakavyoshughulikiwa.
   
 6. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #6
  May 19, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,060
  Likes Received: 3,089
  Trophy Points: 280
  Huu nao ni ubazazi wa hatari sana kwenye dunia ya leo bado tunahangaika na mwenge badala ya kusimamia shughuri za msingi za maendeleo? mwenge unampa mtu dawa?mwenge unampa mtu sabuni ya kuoga?mwenge ndo yamegeuka maji safi ya watu kunywa?Utopian!
   
 7. M

  Mkekuu JF-Expert Member

  #7
  May 19, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Deo hama chama watakuharibia karibu sn chadema.
   
 8. M

  Mkekuu JF-Expert Member

  #8
  May 19, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Magamba hovyo kabisa,wananchi wananjaa iliyosabishwa na wenyewe au siyo,tena bado wanataka kuwatumikisha bure.wampe kazi hiyo rejao,riz,tuntemeke,na yuleee tume ya katiba.
   
 9. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #9
  May 19, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kama nimemwelewa Filikunjombe vizuri, Tatizo ni kwamba wananchi wa Ludewa mwaka jana walichangishwa michango ya mwenge. Mwenge wenyewe haukwenda Ludewa. Pesa zikaliwa. Wananchi hawakupata mrejesho wowote. Kilichomkera Filikunjombe ni kuona kwamba mwaka huu tena watu wake wanachangishwa mchango mwingine wa mwenge ili hali fedha za mwaka jana haijulikani zmekwenda wapi. Isitoshe wakawa wanalimishwa bara bara kwaaajiliya mwenge wakati ile bara bara ni mali ya halmashauri ya wilaya si ya kijiji na ina bajeti yake. Filikunjombe alisema hii si haki. Wanalimishwa bara bara na michango ya mwenge inaliwa.
   
 10. IKHOIKHOI

  IKHOIKHOI JF-Expert Member

  #10
  May 19, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 366
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  si atoke tu huko aliko kwa magamba? Naona ni mtu safi, anayejenga hoja sahihi lakini akiwa katika chama kibovu
   
 11. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #11
  May 20, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kitu kimoja nimejifunza siku hizi hasa katika siasa za leo, ile hewala hewala ya watwana imekoma. Lakini wanaojiona watwa bado wangali na fikra mgando wa kuwaona wananchi bado ni wale wale wa hewalahewala na kuimbiwa nyimbo za kuwasifia wakubwa kama miungu mtu na kuambiwa zidumu fikra sahihi za Mwenyekiti wetu.

  Baadhi walio katika mfumo huo wa uongozi wamefunguka akili na mioyo yao, badala ya kujitazama wenyewe sasa wanageukia wapiga kura wao kuwaona walivyo na wanavyonyanyasika kwa kulimishwa barabara na kuchangishwa pesa za mwenge. Hao waongoza msafara wa mwenge ni mradi maana mwisho wa msafara ni kulala maskini na kuamka tajiri.

  Huko kukimbiza mwenge kuzunguka mikoa yote kuna maana gani zaidi ya kuwapotezea watu muda wao wa kufanya maendeleo? Pamoja na hali ngumu ya maisha bado wananchi wanabebeshwa zigo la kuacha kazi zao za maendeleo na hivyo kuchanga pesa za mwenge na kushika majembe kulima barabara itakayopita mwenge. Huu si wakati wa kufanya mambo ya miaka ya 1960 wakati tunapeperusha bendera ya taifa hilo kwa mara ya kwanza.
   
 12. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #12
  May 20, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe amekabidhi maada wa dawa katika kituo cha afya Mlangali ili kusaidia kupunguza kero ya wagonjwa kukosa dawa katika kituo hicho.
   
 13. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #13
  May 20, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Polepole, siku na saa ikifika ataamua wapi kwa kwenda atakapoamua kuwaachia magamba yao CCM.
   
 14. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #14
  May 20, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Mandhari ya milima na mabonde ni dalili tosha ya nchi kuwa na rutuba, hawa wakiwezeshwa wanaweza kuwa mojawapo ya source kubwa ya kiuchumi katika nchi yetu.
   
 15. kimbangu

  kimbangu Member

  #15
  May 20, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 66
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 25
  Deo filikunjombe ni zaidi ya jembe namkubali sana jamaa na naweza mfananisha na mtu mmoja tu ndani ya chdm nae ni godbless lema,hhawa watu hakuna mtu mwingine yeyote wa kuwafananisha nao kimsimamo na kuteteaa wanyonge
   
 16. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #16
  May 20, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Sijui hata tunaelekea wapi? Yaani mbunge ndio ananunua dawa kwa ajili ya vituo vya afya? Kazi za mbunge hata hazijulikani.
   
 17. Arvin sloane

  Arvin sloane JF-Expert Member

  #17
  May 20, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 963
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Saafi sana deo ni mfano wa kuigwa na wabunge wenzako.
   
 18. b

  bdo JF-Expert Member

  #18
  May 20, 2012
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,712
  Likes Received: 1,611
  Trophy Points: 280
  ukombozi bado, mpaka CCM ya Filikunjombe isiweze kushika hata kijiti cha nchi hii
   
 19. M

  Mohamed Ngwasu JF-Expert Member

  #19
  May 20, 2012
  Joined: May 11, 2011
  Messages: 304
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimependa taarifa yako candid scope unaonesha uko karibu sana na mh sasa ebu mwambie akomae pale halmashauri kuna afisa utumishi mmoja mlevi mlevi hivi hana nidhamu ana dharau sana aangalie anaweza akmwadabisha vipi.
   
 20. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #20
  May 20, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Yule jamaa mlevi mlevi, dallu, Filikunjombe keshamchakachua. Ndo aliyeanza naye. Amehamishiwa dodoma.
   
Loading...