Filikujombe na Msolla wawatolea uvivu mawaziri wa Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Filikujombe na Msolla wawatolea uvivu mawaziri wa Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Dec 21, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Dec 21, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Rais Jakaya Kikwete
  [​IMG] [​IMG]

  Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe kushoto na kulia Mbunge wa Kilolo Profesa Msolla

  MBUNGE FILIKUNJOMBE NA PROF MSOLLA WAWACHARUKIA MAWAZIRI WA JK

  MBUNGE wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe na mbunge wa jimbo la Kilolo mkoani Iringa Profesa Peter Msolla wageuka mbongo katika kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa (RCC) Iringa kwa madai kuwa viongozi wa juu serikali wanamsaliti Rais Jakaya Kikwete .

  Wakati mbunge wa Ludewa akielekeza malalamiko yake kwa waziri wa fedha na Kilimo kwa kushindwa kutimiza ahadi ya rais Kikwete ya kuendelea kununua mahindi ya wakulima wa Ludewa kama alivyoagiza wakati wa ziara yake wilaya ya Ludewa zaidi a mwezi mmoja sasa,mbunge wa Kilolo Profesa Msolla yeye ameimmalamikia waziri wa mambo ya ndani na uongozi wa mkoa wa Iringa kwa kushindwa kutekeleza agizo la Rais la kuhamisha gereza la Kihesa Mgagao Kilolo toka mwaka 2008 alipoagiza.

  Huku mkuu wa wilaya ya Makete Zainab Kukwega akiutaka uongozi wa mkoa kufanya haraka sasa kutekeleza agizo hilo la Rais na kuwa kuendelea kuchelewa kutekeleza ni sawa na kumpuuza Rais .

  Wakizungumza katika kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa (RCC) kilichofanyika leo ukumbi wa St Dominic ,viongozi hao walisema kuwa agizo hilo la Rais lilitolewa toka mwaka 2008 ila hadi sasa hakuna utekelezaji na kuwa kufanya hivyo ni sawa na kumpuuza Rais Kikwete.

  katika maelezo yake mbele ya wajumbe wa RCC Mbunge Prof.Msolla alisema kuwa eneo hilo la gereza la Kihesa Mgagao ni eneo la kihistoria la ukombozi kwa nchi mbali mbali za kusini mwa Tanzania ikiwemo Afrika ya kusini ambapo majeshi ya nchi hizo yalipiga kambi eneo hilo kwa ajili ya kutafuta uhuru wa nchi zao na hivyo ndio sababu ya kuiomba serikali kupitia wizara ya mambo ya ndani kutoendelea kutumia eneo hilo kutesa watu kwa kuwafunga bali eneo hilo kutumika kama shule ili kutoa elimu kwa vijana wazi ambalo Rais alilikubali kwa mikono miwili na kuagiza gereza lihamishwe na eneo hilo ligeuzwe shule ila hadi leo hakuna kilichofanyika.

  Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Ludewa FIlikunjombe alisema kuwa kilio cha wana Ludewa ni juu ya kuendelea kukosekana kwa soko la mahindi katika vituo pamoja na Rais wakati wa ziara yake kuwapa matumaini wananchi kuwa baada ya wiki moja zoezi la kununua mahindi lingeanza katika wilaya ya Ludewa.

  Kwa upande wake mkuu wa mkoa Dr Christina Ishengoma aliahidi kuyafanyia kazi madai ya wabunge hao na kuwa lengo ni kuhakikisha kuwa maagizo mbali mbali yanayotolewa katika vikao kama hivyo na serikali yanatekelezwa kwa wakati.

  Akielezea juu ya wakulima wa Ludewa na mkoa wa Iringa alisema kuwa kuanzia sasa viongozi wa wilaya wasiogope kuwatosa mawakala wa pembejeo ambao wanashindwa kuanza kazi ya kusambaza pembejeo kwa wakulima kwa kisingizio cha kukosa mitaji.

  Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa viongozi wanapaswa kuwabembeleza wakulima kuhusu kuchelewa kwa vocha cha pembejeo ila sio mawakala ambao wanatafuta fedha kwa kazi hiyo na kuwa yule ambaye ameshindwa kusambaza pembejeo kwa nguvu yake basi kazi hiyo imemshinda.
   
Loading...