Filamu za kutangaza utalii wa Tanzania kuonyeshwa kwenye ndege 300 duniani

Makanyaga

JF-Expert Member
Sep 28, 2007
10,327
6,849
Dar es Salaam.Balozi wa Indonesia nchini Malaysia, Rusdi Kirana amekubali kuonyesha filamu za kutangaza za utalii wa Tanzania kwenye ndege 300 zinazofanya safari kwenye zaidi ya nchi 50 duniani.
Balozi Kirana ambaye pia ni mfanyabiashara mkubwa anayemiliki mashirika ya ndege ya Lions Group, Batik na Malindo ambapo mashirika hayo yana ndege zaidi ya 300 amefikia uamuzi huo baada ya kuombwa na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dk Ramadhani Dau.

Mashirika hayo yanahudumia abiria 60 milioni kwa mwaka yanatoa huduma za safari kwenye zaidi ya nchi 50 duniani.

Makubaliano hayo yamefanyika leo Alhamisi Januari 30, 2020 baada ya mabalozi hao wawili kufanya mazungumzo juu ya ya kutangaza utalii wa Tanzania kwenye ndege kupitia inflight entertainment.

Baada ya makubaliano, Dk Dau ambaye pia anawakilisha Tanzania nchini Indonesia alimkabidhi balozi Kirana filamu hizo ambazo zitaoneshwa kwenye ndege bila malipo yoyote kutoka ya Serikali ya Tanzania.
Mabalozi hao wawili pia wamekubaliana umuhimu wa kutangaza utalii katika ukanda wa Kusini Mashariki ya Asia ambapo balozi Kirana ameahidi kuanzisha safari za ndege kwenda Tanzania baada ya kufanya mazungumzo na mawakala wa utalii wa Tanzania.

Balozi Kirana ameonesha utayari wake wa kukutana na kujadiliana na mawakala hao wakati wa Kongamano la Uwekezaji baina ya Tanzania na Indonesia (Tanzania/Indonesia Investment Forum) litakalofanyika Jijini Jakarta Indonesia Septemba 24 hadi 26, 2020.

Balozi Kirana ameahidi kutembelea Tanzania katikati ya mwezi Septemba 2020 baada ya kualikwa na Dk Dau.


Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dk

Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dk Ramadhani Dau akimkabidhi Balozi wa Indonesia nchini Malaysia, Rusdi Kirana filamu za kutangaza utalii wa Tanzania.

============

Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom