VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Uzuri wa runinga ya nchi hii,haikosi filamu zitiazo hamu. Ni mwendo wa bandika-bandua kabla haijaungua. Baada ya kutajwatajwa kwa haja kwa Said Lugumi na kampuni yake,sasa ni zamu ya Dr. Tulia Ackson na uongozi wake Bungeni.
Tatizo kubwa la runinga yetu ya kinchi na mbonyezaji wake ni kuwa filamu hazifiki mwisho. Zinakatishwa. Na hata hazirudiwi. Zimeshakatishwa filamu za Richmond, EPA,Escrow,Tokomeza,Kimbunga,Kuuzwa kwa Oysterbay Polisi,Nyumba za Serikali,Kivuko cha Bagamoyo,Lugumi na kadhalika. Filamu kali tupu.
Ni kama ilivyoandikwa kwenye kibao pale Luguruni,Kinondoni karibu na Chuo Kikuu cha Mtakatifu Yosefu: "Dr. Tulia Ackson Avenue". Ni muda wa filamu yake adimu. Itazimwa muda si mrefu ili iwashwe nyingine. Watazamaji hatuachi wala kuchoka!
Mzee Tupatupa wa 'Ulevini' Lumumba,Dar es Salaam