The Khoisan
JF-Expert Member
- Jun 5, 2007
- 14,927
- 12,222
Filamu ya watoto 'nyoka' wa Mererani yazinduliwa Marekani
Na Harieth Makweta
KUZINDULIWA kwa filamu mpya jijini New York Marekani hivi karibuni inayoonyesha watoto wa Kitanzania wakifanyishwa kazi ngumu kwenye machimbo ya madini ya Mererani mkoani Manyara kunaweza kutoa mwanga kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua za haraka kuingilia kati kuzuia mateso dhidi ya watoto hao.
Filamu hiyo ambayo imepewa jina la Gem Slaves: Tanzanite's child Labour inaonyesha jinsi gani watoto wanavyotumikishwa katika machimbo ya tanzanite Mererani na kushindwa kwenda shule kutokana na muda wao mwingi kuutumia kufanya kibarua kama �nyoka� jina ambalo hutumiwa katika migodi hiyo.
Filamu hiyo inaanza kwa kuwaonyesha watoto wanne wakiwa chini ya migodi wakitafuta mawe.
Wilson Peter, mtoto mwenye umri wa miaka 12 ambaye ndiye anayeonekana kuwa kinara wa filamu hiyo anaeleza kwa undani jinsi watoto hao wanavyokabiliana na ugumu na hatari ya kufanya kazi ngumu kwenye machimbo ya madini.
�Tunateremka mgodini, tukifika chini tunaanza kuchekecha mchanga, wakati mwingine hatupati madini njaa inatuuma hata tunalazimika kurudi nyumbani,� anaeleza Peter.
Anaongeza: �Tukishamaliza kula tunarudi tena kuchekecha mchanga mitaani, ukifika muda wa saa kumi na mbili jioni tunarudi nyumbani.�
�Muda wa jioni ukifika, tunabadilisha nguo tunavaa za nyumbani badala ya kuendelea na zile ambazo tulivaa wakati wa kuchekecha mchanga, tunakwenda kuchota maji ya kutumia nyumbani, na kisha tunamsaidia mama kazi. Usiku ukifika tunakwenda kulala.�
Filamu hiyo inaelezea mazingira halisi ya namna watoto wanaojishughulisha na shughuli za utafutaji madini katika machimbo ya madini jinsi wanavyotaabika kwa kufanya kazi nyingi na ngumu kulinganisha na umri wao.
Machimbo ya madini ya Mererani ndiyo pekee duniani yanakopatikana madini ya tanzanite. Kila mwaka madini hayo huingiza fedha nyingi sawa na dola za Marekani milioni 300 lakini watoto hao hawafaidiki na mapato hayo.
Hata wazazi wao ambao nao wanaizunguka migodi hiyo bado wanaishi katika maisha ya umaskini wa chini ya dola moja kwa siku.
Filamu hiyo inaendelea kuelezea kwamba kila mwaka maelfu ya watoto huenda Mererani kutafuta madini na watoto hao ndio wanaofanya kazi kubwa migodini.
Kwa mujibu wa filamu hiyo, zaidi ya wachimbaji 30,000 huenda chini zaidi ya mita 300 bila vyombo vyovyote vya usalama na bila mshahara wa uhakika.
Kila siku wachimbaji wadogo 4,000 wa miaka kati ya 14-24 huhatarisha maisha yao katika migodi hiyo isiyo na vyombo madhubuti, huku watoto hao wakipewa mlo mmoja tu kwa siku.
�Watu wanapoona tanzanite madukani wanaiona imependeza sana ila hawajui inapatikana vipi mpaka ikafikia rangi na mng�aro mzuri ilionao,� inaeleza sehemu ya filamu hiyo.
Mtoto Wilson anaeleza: �Kama nikiwa Rais wa Tanzania sitaruhusu watoto kwenda kufanya kazi migodini na wale ambao watakamatwa wakitumikisha watoto migodini watahukumiwa kifungo.�
Hata hivyo, japo anajua kuwa kuna hatari anapokuwa ndani ya migodi ambako anaweza kuangukiwa na miamba mikubwa, hana budi kuendelea kuifanya kazi hiyo kwa vile ndiyo inayompatia riziki.
Mbali ya hatari ya kuangukiwa na mawe makubwa, athari nyingine ni pamoja na uwezekano wa kupata ugonjwa wa kifua au kuteleza na kuanguka kwenye mashimo yaliyo na kina kirefu cha kutisha.
Mtoto huyo anasema haoni busara kwa watoto kufanya kazi migodini kwa sababu huwa wanatumwa tumwa ovyo kwenda nje ya shimo, kuleta soda, kuchukua tindo ya umeme (jack hummer) na yeye bado ni mtoto.
Mtoto mwingine, Mutasi anasema yeye alikuwa akifanya kazi kama nyoka, akaacha kutokana na ugonjwa alioupata wa kifua na siku nyingine hushindwa kula chakula cha mchana.
Aliacha peke yake huku wenzake zaidi ya 50 wakiendelea kufanya kazi hiyo mpaka sasa.
Anasimulia kuwa alikutana na fundi mmoja aliyekuja katika mgodi huo kutengeneza mashine naye akapata kumueleza tatizo lake.
Baada ya kujifunza kazi ya kutengeneza magari sasa anajifunza kazi za karakana na baadaye akishakuwa mkubwa anategemea kufungua karakana yake na kufundisha watoto wenzake kama yeye alivyofundishwa.
Katika filamu hiyo msichana aliyeigiza kama mama mzazi wa mtoto Wilson anaelezea masikitiko yake na kuongeza kuwa umaskini ndicho chanzo kikuu cha wazazi kushindwa kuwazuia watoto wao kutofanya kazi migodini.
�Kwa kweli hatuifurahii hata kidogo kazi ya kuchekecha mchanga huko migodini ni shida iliyopo hapa ndiyo inayotulazimu kuwaacha watoto wetu wahangaike,� anaeleza.
Anaongeza: �Maana watakapopata Sh200 au 300 wanaleta nyumbani, wananitupia hapa nami inaniwezesha kuendelea kuwalea, na mimi nikihangaika kuuza mboga inawasaidia kuendelea kuishi,� anaeleza.
�Ndio maana tunawaruhusu, wakisema wanakwenda kuchekecha hatuwanyimi maana kila mtoto ana bahati yake. Kwa kweli wanavyohangaika tunawahurumia lakini kutokana na shida tuliyonayo hapa inabidi tuwavumilie, tuwalee katika hali hii mbaya, anaeleza mama Peter.�
http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=4029