Filamu nyingi hazina maadili ya Kitanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Filamu nyingi hazina maadili ya Kitanzania

Discussion in 'Entertainment' started by MziziMkavu, May 4, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 4, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]WIZARA ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kupitia Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza imezuia kuonyeshwa filamu 5 kati ya 45 zilizokaguliwa mwezi Februari na Machi mwaka huu kutokana na kutozingatia maadili ya Kitanzania.

  Filamu zilizozuiwa kuonyeshwa hadharani na kwenye vyombo vya usafiri ni Filamu ya Mtoto wa Mama, Inye, inye Plus, Inye Ndembendembe na Inye Gwedegwede.

  Sababu kubwa ya Bodi ya Filamu na Michezo ya kuigiza kuzuia filamu hizo ni pamoja na filamu hizo kutokuwa na maudhui na maadili ya Kitanzania, ambapo zinaonyesha vitendo vya Ushoga sambamba na kudhalilisha wanawake hasa wanene kwa kugeuza miondoko yao ambayo inaamsha hisia za kingono.

  Tunaipongeza Bodi ya Filamu na Michezo ya kuigiza kwa kuzuia filamu hizo kuonyeshwa, ingawa hatujalidhishwa na utaratibu wanaotumia wa kuruhusu filamu zisizo na maadili ya kitanzania kurekodiwa na kuonyeshwa huku pia wakichelewa kukagua filamu nyingi zinazotengenezwa nchini kwa sababu zimeishasambaa kila kona ya nchini na watu wanazo majumbani kwao.

  Tunasema hivyo kwa sababu watunzi na watengenezaji wa filamu hawatakiwi kutengeneza filamu bila kuwa na kibali cha Waziri mwenye dhamana ya masuala yanayohusu filamu na michezo ya kuigiza na hawatakiwi kuonyesha filamu yoyote bila kukaguliwa na Bodi na kupewa daraja.

  Tunapenda kuishauri Bodi ya Filamu na Michezo ya kuigiza kuwa makini na kuendesha zoezi hilo la ukaguzi kila mwezi ili kuhakikisha filamu zilizo sokoni zinastahili kuangaliwa na watanzania na kuondoa sokoni filamu ambazo hazistahili.

  Tunaamini zipo filamu nyingi ambazo zinatengenezwa bila kibali cha Waziri mwenye dhamana ya masuala yanayohusu filamu na michezo ya kuigiza kwa sababu jinsi zilivyo wazazi hawawezi kukaa na watoto wao na kutazama filamu hizo pamoja.

  Tunaishauri Bodi ya Filamu kutengeneza utaratibu wa kukutana na watunzi na watengenezaji wa filamu ili kupeana miongozo muhimu itakayohakikisha tasnia ya filamu na michezo ya kuigiza inakua na kuzingatia maadili ya kitanzania.

  Ni wazi Bodi ya Filamu wakikutana na watunzi na watengenezaji wa filamu watafundishana kuhusu maadili ya Mtanzania kwa sababu inavyoonekana asilimia kubwa ya watunzi na watengenezaji wa filamu hawajui maadili ya kitanzania na kama wanajua basi wanafanya makusudi kupotosha maadili ya kitanzania, ipo haja ya kufahamu maadili ya kitanzania yapo vipi.

  Chanzo:Gazeti la Mwananchi
   
 2. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #2
  May 4, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,991
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Copy n paste Nigeria mkuu,ubunifu hamna kabisa.Wengi wao ni vilaza kwenye fani.
   
 3. chapaa

  chapaa JF-Expert Member

  #3
  May 5, 2011
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 2,355
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Kama akina nani kaka?tujuze basi.
   
 4. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #4
  May 7, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Nahisi nitamaliza nguvu zangu kuzizungumzia hizi takataka tunazoziita "bongomovie"
   
 5. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #5
  May 8, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,688
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  Maadili ya Mtanzania ni yapi? Inyeeee. Kwani c hata wazungu ktk film zao huwa wanaweka ni kuanzia miaka ipi mtu anayeruhusiwa kuangalia film hiyo
   
 6. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #6
  May 8, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,231
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Tanzania yenyewe imeshindwa kusimamia ama tuseme kabisa imekosa ut amaduni wake ndo maana vijana wa kileo hawaishi kotoga ndimi huku dada zao wakitembea uchi...
   
 7. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #7
  May 8, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Ni watu wengi saana ambao huponda sana hizi Bongo Movies kwa kuzilinganisha na za nchi nyingine. Personally napenda saana kuangalia movies lakini nimewahi angalia za kibongo kama tano, nakumbuka tu moja jina I think it goes something like 14 days or 14 weeks (mtanisamehe sikumbuki vizuri).

  En ways kitu ambacho nilitaka kugusia ni ukweli ulio wazi kua watanzania weengi lugha ya kigeni yani kiingereza kinatusumbua saana. Hivyo basi hio ilipelekea kua Wananchi wachache sana wa Tanzania walikua wakiketi chini na kukaa kama familia kuangalia filamu, hasa hasa wakijitahidi saana ilikua zinachuliwa picha za ngumi ambazo haziihitaji uelewe lugha bali kujua tu sterling kashinda na hajauwawa... (Enzi za Van Damme, Jacky chain, Arnold...)

  Bado naona kiwango cha filamu Tanzania ni kidogo but kweli kwa moyo wa dhati kabisa napongeza wale woote Tanzania walio katika filamu industry kwa kazi wanayofanya kwani ni Wananchi wengi sasa wanoweza kuketi na kuangalia filamu akaelewa lugha na akafurahia. Weakness zao katika hizi picha ni kubwa na nyingi to the extent mtu anae angalia movies toka zamani na kuzoea kuangalia za nje ina kua kazai kweli kuvumili sababu kubwa kwamba movies zetu hazina suspense. I wish ifike a time ambayo hata mimi naenda dukani kutaka movie fulani ya Kitanzania huku nikijua nita enjoy....

  Big up watu wa film industry, someni historia za Movie entertainment Bollywood na most importantly Hollywood then tuta observe nao walianza kwa kuchechemea....
   
 8. H

  HERBERGONER Member

  #8
  Sep 6, 2011
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli!
   
Loading...