filam za bongo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

filam za bongo

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Born Star, Jan 7, 2012.

 1. Born Star

  Born Star JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2012
  Joined: Oct 24, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  jana nimeangalia filam moja ya bongo sio sili inakela yaani nusu saa tu imeisha halafu wanasema niitafute part 2 hivi hii maana yake nini wajameni?
   
 2. Ralphryder

  Ralphryder JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 4,588
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Bado unatazama upupu huo! Mi nilikwisha acha kabisa! Hawana ubunifu,action,wala kumudu camera hawajui! Pole.
   
 3. Amyner

  Amyner JF-Expert Member

  #3
  Jan 7, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 2,404
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  Mtu akishapata umaarufu tu anaigiza... Unategemea kutakuwa na kiwango hapo?
   
 4. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #4
  Jan 7, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  ​kwani bongo wanafanya movie au maigizo?????????
   
 5. mafiakisiwani

  mafiakisiwani JF-Expert Member

  #5
  Jan 7, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 456
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  wamefundishwa biashara na mchina
   
 6. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #6
  Jan 7, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,177
  Trophy Points: 280
  Wananifurahisha na Translation Zao From Swahili to English... na Pia Hawajui Kutune Sauti kwani Mtu akiwa Nje na Ndani hakuna Tofauti Mivumo na Mirindimo mwanzo mwisho
   
 7. mafiakisiwani

  mafiakisiwani JF-Expert Member

  #7
  Jan 7, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 456
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  wape maujuzi ndugu yangu ili na wao wawe njema.
   
 8. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #8
  Jan 7, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,633
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  kuna filamu moja ya nje inaitwa 'The Son of Rambow' pale ni darasa tosha kwa watunzi,waongozaji wa filamu za tz. Inaonyesha watoto wadogo walivyotumia resources kidogo kutengeneza picha kali...hasa ubunifu na muda...
   
 9. mafiakisiwani

  mafiakisiwani JF-Expert Member

  #9
  Jan 7, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 456
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  ngoja nikaitafute
   
 10. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #10
  Jan 7, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,177
  Trophy Points: 280
  Wakubwa hawafundishwi kucheza Mpira.. Kuwafundisha si ndio itakuwa Elimu Mtaani dot Com mnaionaje..
   
 11. matumbo

  matumbo JF-Expert Member

  #11
  Jan 7, 2012
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 7,199
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Ukiangalia lazima uwe na remote control pembeni kudhibiti mfumuko wa sauti.
   
 12. mafiakisiwani

  mafiakisiwani JF-Expert Member

  #12
  Jan 7, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 456
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  sasa utafanyaje ili kuwasaidia?
   
 13. mafiakisiwani

  mafiakisiwani JF-Expert Member

  #13
  Jan 7, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 456
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  ni nini kinafanya hayo yatokee?
   
 14. Raimundo

  Raimundo JF-Expert Member

  #14
  Jan 7, 2012
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 13,552
  Likes Received: 10,940
  Trophy Points: 280
  Kama huzipendi na zinakukera, piga chini. Acha wanaoinjoi waendelee kupata uhondo, na kwa taarifa yako Library zote za muvi zina 60-80% ya Bongo Movies, sasa utajiuliza wepi wanaangalia!

  JF tunajifanya classic sana, hakuna cha ndani tunachosifu hata kimoja, acha kuponda toa maushauri kama kweli wewe ni mjanja sio kulalama tu na kuharibiana biashara.

  NB: Kanumba, Ray et al wana hela zaidi yetu wengi tunaojiita griti thinkas humu JF, wanauza hizo hizo muvi tunazoona choka mbaya.
   
 15. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #15
  Jan 7, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,177
  Trophy Points: 280
  Hata Kikwete asipoendesha Nchi Vizuri tumuache na tukae Kimya kama Vipi Tusepe Nchi zingine? Mkuu Kuna Tuzo huwa zinatolewa za Movie Nzuri na Movie Mbaya zile zilizopigwa ovyo... Movie ni Utamaduni wa USA so usidhanie watu waone Wenzetu wanakosea waachwe tu Hata Original Comedy walipoanza kukosea ikapoteza Watazamaji....
  Taarabu walipozidisha Mipasho ikapoteza Wapenzi..
  Bolingo walipozidisha viuno ikawa Kero ikapotea.
  Sasa Hizi Movie tuzishike tuwasaidie Wawe Juu... wanazicheza ndivyo sivyo huwa zinamuelekeo fresh but zina makosa Mengi

  Mwanzo walipoanza kulikuwa hadi tunaona vivuli vya mike au mpiga picha walisemwa wakajirekebisha Sasa Sauti ndio naona inawakera wengi..
   
 16. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #16
  Jan 7, 2012
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Suala sio kuwa na hela nyingi, kuna majambazi wana hela nyingi kuliko sisi, tuwasifu? Msipokubali kurekebishwa mtabaki hapohapo milele. Kazi kuiga sinema za ki nigeria, sinema hazina uhalisia, kila movie lazima ichezwe kwenye jumba la kifahari.... Picha inapigwa toka mtu anavaa socks, anakunywa chai, anafunguliwa geti, gari inatoka taratibu huku ikiwasha indicator, inasubiri magari yaishe, inaingia main road, inasimama kwenye taa nyekundu eeeh. Hapo shida ni kuonesha eti boss anakwenda kazini.
   
 17. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #17
  Jan 7, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,633
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  Dan Brown(mwandishi wa vitabu kv. DA VINCI CODE n.k) aliwahi kusema hivi: 'katika kila ukurasa mmoja uliopo kwenye kitabu umetanguliwa na kurasa 10 nilizotupa kwenye dust bin...' Maana yake ni nini? jamaa anaandika na kusahihisha,umakini,tafiti,muda,nk...tatizo la hawa wenzetu ni mtindo wa voda fasta! Tumeshindwa kuhakiki Things Fall Apart, Watoto wa Mama Ntilie,leo hii tunaandika script za thriller movies...wapi na wapi bwana!
   
 18. Bosi Michembe

  Bosi Michembe JF-Expert Member

  #18
  Jan 7, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 273
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Safari ya utengenezaji wa filamu bongo bado ni ndefu sio siri.. Ukicheki lazima uone kivuli cha kameraman, reflections kwenye vioo ya crew ya wapiga picha, subtitles kichina, sound haiko mastered kabisa inapanda inashuka, soundtrack ni moja hiyo hiyo mpaka mwisho, hawaheshimu copyright za wenzao (hapa namaanisha na wenyewe ni wezi) wanaweka miziki ya sean paul, rihhana, celine dion bila copyright agreement yoyote (hapa huwa siwaelewi wanapopiga kelele wanaibiwa kazi zao wakati ndani ya filamu yenyewe wameiba story au music ya msanii wa nje "angalia Fake Pastors'' na nyinginezo), story inaweza kuwa ya 1 hour lakini itarefushwa mpaka izae part 1,2 and 3. Tungependa waendelee lakini pia wajifunze zaidi na kurudi shule am sure they are making money waende hata kwenye film masterclasses nje warudi hata na kitu kichwani....
   
 19. chapaa

  chapaa JF-Expert Member

  #19
  Jan 8, 2012
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 2,355
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  wadau mlichokiongea humu ndani ni ukweli mtupu,tatizo letu ni moja huwa hatupendi kukosolewa na ikitokea hivyo mtu anaanza kudai ooh chuki binafsi na kadhalika lakini unakuta mtu anakuwa anatoa ushauri
   
 20. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #20
  Jan 8, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  dont worry guys. Afroasis Films is coming soon to quench your thirsty
   
Loading...