Filam Ya Vikaragosi (Cartoon) Ya Kiswahili Kwa jina la Manzese | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Filam Ya Vikaragosi (Cartoon) Ya Kiswahili Kwa jina la Manzese

Discussion in 'Entertainment' started by X-PASTER, Apr 22, 2011.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Apr 22, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Filam Ya Vikaragosi (Cartoon) Ya Kiswahili Kwa jina la Manzese


  Hii ni kazi ya Dr. Boniface Mhella, mjumbe wa Jumuiya ya Watanzania Roma, ambaye tayari amekamilisha filamu yake yenye mandhali ya kikatuni, inayokwenda kwa jina la "Manzese".

  Dr. Boniface yupo kwenye harakati za kutafuta wasambazaji wanaoeleweka watakao fanya nae kazi.

  Maelezo:
  Filamu hii ni ya kutungwa na ni yenye kufurahisha, kusikitisha na vile vile kuleta matumaini. Inamuhusu mwanamume aitwae Kindunde. Kwa kifupi tu ni kwamba, Kindunde baada ya kuchoshwa na hali ya umasikini na ya maisha duni ya Manzese, aliamua kuangalia uwezekano wa kuitengeneza Manzese kuwa mji mpya.

  *****

  Goofy:
  Kwenye filam hii kuna hitirafu ambazo mtengenezaji angeweza kuzirekebisha, na filam yake ikaleta uhalisia. Kwa mfano, ametumia sauti ya mwanaume sehemu ambayo alipaswa kuwekwa mwanamke.

  Kitu kingine nilicho kigundua ni kuwa sauti zote zilizomo kwenye filam hii ni za mtu mmoja. Amejaribu kubadilisha badilisha uzungumzaji tu.

  Vile vile speed au mwendo kasi wa filam ni mdogo sana, sina uhakika kama waliseti PAL/SECAM 24/25 FPS (frames per second). Hivi ni vitu ambavyo vilipaswa kusetiwa kabla ya kuanza kuchukuwa picha au kutengeneza hivi vigaragosi (Cartoon).

  Wasiliana Naye:
  Wasiliana naye kwa email hii: bonn-j@hotmail.com ili muweze kushauriana nae.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2011
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Nimewahi kuisikia hii filmu ya vikatuni ilipoanza kutengenezwa. Hongera Dr. Boniface kwa kukamilisha kazi hii na bila shaka kabla ya kuisambaza utatilia maanani ushauri wa mleta hoja hapa.

  Tiba
   
 3. D

  Dr Mhella Member

  #3
  Apr 24, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dear JF Senior Expert Member
  Naomba nijibu baadhi ya comments hapa.
  1) Kwenye filam hii kuna hitirafu ambazo mtengenezaji angeweza kuzirekebisha, na filam yake ikaleta uhalisia. Kwa mfano, ametumia sauti ya mwanaume sehemu ambayo alipaswa kuwekwa mwanamke.
  Jawabu langu: Je ni haki kuwaandikia watengenezaji wa Vikaragosi vya SIMPSON na kuwaambia wanawake wote wawe na sauti nyororo za kike? Naamini kama wao watawasikilizeni basi na mimi nitakuwa mtu wa ajabu kutowasikiliza. Lakini kama watawaacheni kama mlivyo basi na mimi nawaacha kama mlivyo. Natumaini kile cha muhimu hapa ni kuchambua charactors kama mtayarishaji wa filamu anavyowaletea. Kuna charactors mtakazozipenda na zipo ambazo mtazichukia. Lakini charactors zote zipo kama zilivyo. Wachambuzi wa filamu huwa hawamwandami mwandaaji abadilishe charactors. wakifanya hivyo basi wanamtangazia mwandaaji ushindi kuwa ameweza kufikisha ujumbe kwa jamii.
  Kitu kingine nilicho kigundua ni kuwa sauti zote zilizomo kwenye filam hii ni za mtu mmoja. Amejaribu kubadilisha badilisha uzungumzaji tu.

  Dunia inayokuja ni dunia ambayo mtu mmoja ataweza kutengeneza movie mzima. Sijui mnalijua hilo? Kuhusu sauti kuwa ya kwangu ni kwa sababu bado wataalamu wa sinema wanahaha kutengeneza software ambazo zitaweza kubadilisha sauti ya kiume kuwa ya kike au ya kama ya mtoto. Nilizijaribu na mimi nakubaliana na ninyi kuwa bado wapo nyuma. Ndo maana mmeweza kuliona hilo. Tuombe huko mbele waweze kufanikiwa kwa hilo au kama kuna mtu anayejua software nyingine basi aniambie ili niweze kuitumia. Ntamshukuru mara mia!

  Vile vile speed au mwendo kasi wa filam ni mdogo sana, sina uhakika kama waliseti PAL/SECAM 24/25 FPS (frames per second). Hivi ni vitu ambavyo vilipaswa kusetiwa kabla ya kuanza kuchukuwa picha au kutengeneza hivi vigaragosi (Cartoon).
  Hili swali aliyeuliza inaonesha hajui hata kidogo mambo ya animation.
  1) Sikutumia physical camera hata moja. Camera ipo ndani ya software na mtu anaiset baada ya animation. na hata ukiiset hakuna kitu kama PAL au NTSC. Hapa tunazungumza lugha tofauti.
  2) Napenda kukuhakikishia kuwa spidi ya movie pale inapokwenda slow ni kwa sababu mimi nimeamua hivyo bila ya kubahatisha. I did it intentionally. Kama haikutakiwa kwenda slow basi it is an intensional error. Wachangiaji wanakosea pale wanapofikiri kuwa spidi ya scene ni ndogo kwa sababu ya kutojua ninachofanya. NO NO NO AND NO. Nashauri uangalie movie nzima ili uone wapi na wapi spidi ilikuwa ndogo. Faida moja wapo ya High Definition ndo hiyo. A scene can go slowly bila blur. Sasa wewe bado upo kwenye mambo ya PAL and SECAM? Rendering yangu ilikuwa HD.

  Kwa sasa hivi naishia hapa. Nitajibu zaidi kama maswali yatakuwa kwenye lugha ya kujibika...
  Asanteni sana
  Boniface
   
 4. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #4
  Apr 24, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mkuu naona majibu yako ni kama mtu ambaye ukupendezwa na uchambuzi wa filam yako....! Utakuwa mtu wa ajabu sana kama utakuwa umekasilikia maoni ambayo mimi binafsi ndio niliye yatoa na kuweka hapa ilo bandiko.

  Maoni niliyoyatoa nilitegemea ni ya kukujenga na si kukudhalilisha kama unavyo fikiria, mimi ni mmoja wa waangaliaji sana wa filamu, na haswa uvutiwa na wale wote wenye kufanya jitihada za kutengeneza kitu kipya kwenye tasnia ya filam haswa za kwetu Bongo. Najuwa sana umejitahidi kwa uwezo wako....! Lakini pale ambapo kuna makosa tutasema ili kesho na kesho kutwa ufanye jitihada zaidi ili siku nyingine utoe filamu iliyo bora zaidi.

  Ulipaswa kwanza kufurahia na pengine kushukuru kwa filam yako kuwekwa hapa na kupata watu wa kuangalia japo kipande kidogo.

  Unapotaka kujilinganisha na watengenezaji wa vikatuni wa Simson, utapotea sana, wale wapo mbali sana kitekinolojia na wana uzowefu mkubwa sana wa utengenezaji wa filamu za vikaragosi, licha ya utaalam wao ulio bobea lakini hawana 3D, bado wanatengeneza vigaragosi vyao in 2D.

  Ninaposema kuwa flame rate hipo too slow namaanisha hivyo kuwa hipo slow, na hata mazungumzo yake yapo very slow yaani kama mtu anayejifunza kuzungumza Kiswahili. Mazungumzo hayana uhalisia wa kimazungumzo kabisa, kiasi unaweza kumchosha muangaliaji. Slow motion unayo izungumzia wewe ni tofauti na kile mimi ninacho kizungumza.

  Kaka nilikuwa sijui kama kwenye HD hakuna kiti kama Pal/secam, basi mimi naweza kuwa nipo nyuma sana kiteknolojia...! Ila ninavyojuwa mimi hata hizo HD zipo kwenye hizo hizo Pal au secam, na uko ndiko kwenye hizo flame rate.

  Haya Dr, nisikuchoshe sana, ila huo ndio mtazamo wangu na ndio maoni yangu binafsi...!

  Naomba nichukue nafasi hii kukukaribisha JF kaka, karibu sana sana tupo pamoja na wacha hasira, tupo hapa kujenga na si kubomoa...! Nimeipenda kazi yako ila penye makosa sitasita kusema.

  Keep it up.
   
 5. JohnShaaban

  JohnShaaban JF-Expert Member

  #5
  Apr 24, 2011
  Joined: Aug 23, 2007
  Messages: 465
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  IMHO, kiwango ambacho X-paster amekionesha ktk kubandika hii habari ni cha KIUNGWANA sana hasa ukizingatia kuwa ameibandika kwa ihari yake na kuongeza na maoni yake! Haiyumkini uelewa wangu mdogo, sijaona mahali ambapo X-paster amemwandama mwandaaji kuhusu kubadili "charactor", nilichoelewa ni kwamba amejaribu kutoa dukuduku la sehemu ambazo "charactors" hawajavaa uhalisia. Nilitegemea jibu lenye mtazamo wa kuelimisha kuhusu uandaaji wa filamu za vikaragosi maana ni wachache wenye uelewa huo.

  Tunashukuru kwa kutuelewesha maana hata hili tulikuwa hatulijui... japokuwa tumelishuhudia kwenye filamu kama "Coming to America", tuliyoiona miaka ya mwisho wa 1980's!

  Tunashukuru pia kwa kututambulisha teknolojia mpya maana Tanzania bado tunajikongoja na hizi za zamani... LAKINI sina hakika "audience" yako ni hipi?

  Kwa sababu sijaiona hii filamu ya vikaragosi, naomba niwe muungwana kwamba nimechangia kutokana na maelezo ya awali ya X-paster na Dr. Mhella. Nategemea walio kwenye nafasi za kutuwekea "clips" watafanya hivyo ili tuweze kuona kazi ya Mtanzania mwenzetu maana tumekuwa na kiu kuona mafanikio yetu... hongera Dr. Mhella kwa filamu hii.
   
 6. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #6
  Apr 24, 2011
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nimeitazama clip hapo juu. Nimesoma pia maoni ya X-PASTER na "Majibu" ya Dr. Mhella. Maoni yangu:

  PONGEZI

  1. Nakupongeza Dr, kwa kazi kubwa. Naiita kubwa kwa kuwa nafahamu uzito wa kufanya ulichokifanya (Character animation). Mimi ni mdau katika mambo haya japo kwa character animation bado niko chini sana, tena sana, maybe in a year ntakuwa nina kiwango ambacho ninakitaka, ila kwa non-character animation naridhika na kiwango changu. Nakupongeza tena.
  MAONI YA X-PASTER

  1. Nadhani maoni ya X-PASTER hayana tatizo (Na ni sahihi pia) kwa maana ya Observation labda tatizo liko katika "technical" explanation ya kile alichokiona. Mambo ya SECAM, MESECAM, PAL, NTSC, DVD huwa determined na media itakayotumika kuplay hiyo video kama VHS, DVD, BluRay pamoja na Maeneo ya Mabara. Kwenye kutengeneza animation hakuna kitu kama hiki, ila ukishamaliza ukataka kutengeneza DVD basi masuala ya PAL na NTSC au HD huja (Hata wakati wa kuexport/rendering pia waweza kuspecify na kwa kawaida tunafanya hivi). Pia si lazima kuwa kitu kikiwa slow basi framerate nayo iko chini. Sikusudii kulichambua suala hili kwa undani, naishia hapa.
  2. Kwa clip niliyoiona hapo juu, iko slow. Iko slow kwa maana ya movements na responses za characters pamoja na uzungumzaji wao. Kuna kiwango cha speed ambacho binadamu wa kawaida huona ndiyo sahihi. Huenda wewe umefanya intentionally kuwa slow hivyo lakini nini sababu ya wewe kuamua hivyo? Kuna wakati slow motion huwekwa ili kuweka emphasis kama katika kurudia goli au faulo katika TV lakini mpira ukiwa unaendelea huwa na kasi ya kawaida. Sinema za Charlie Charplin (Hata za akina Joti) kuna wakati hupelekwa kasi wanapokimbia "kutia chumvi" ya ukimbiaji lakini kwa clip yako matukio yaliyomo yalistahili kuwa ya "kasi ya kawaida" na si "intentional" slow performance.
  SAUTI NA MAZUNGUMZO

  1. Ni kweli kuwa sinema inaweza kutengenezwa na mtu mmoja kama unavyosema hasa kama sinema hiyo ni fupi sana na haina matukio mengi kwa wakati mmoja. Sinema kama Avatar, Pirates of the Carribean etc ni almost impossible kwa mtu mmoja kuitengeneza ndani ya muda ambao ni reasonable labda kama unataka kuitengeneza kwa 7 years. Najua unajua. Pamoja na changamoto ya sauti inayoikabili teknolojia lakini similarity katika characters wako imekuwa kubwa sana. Sijui umejaribu software zipi. Kwa mfano kutengeneza sauti ikakaribia kuwa ya kitoto unaweza kuongeza pitch kwenye Adobe Audition bila kubadili Tempo (haimaanishi itakuwa perfect lakini angalau). Kama trial tu hebu jaribu kuplay wimbo wowote kwa Jet Audio then cheki option ya kubadili pitch uone ambavyo hata wewe unaweza kuipotea sauti yako mwenyewe (Jet Audio inaplay tu na si ku-convert, convertion fanya kwa Adobe Audition). Kutoka sauti ya kiume kwenda ya kike ni kazi yenye kutoa jasho, kui-achieve kwa Adobe Audition inahitaji mchaka mchaka kweli lakini atleast inaweza kukaribiwa baada ya majaribio kadhaa. Ni rahisi zaidi kubadili sauti ya kike kuwa ya kiume kwa kuipunguzia pitch. Jet Audio yaweza kusaidia kufanya majaribio kwa maana ya kuplay tu.
  SANAA

  1. Fanyia kazi modelling beauty na vigour/vibrance ya characters
  2. Success ya sanaa huwa ni namna watazamaji watakavyoipokea hata kama tumeweka/hatukuweka efforts kiasi gani. Tukumbuke pia watazamaji wengi ni non-technical lakini wanajua binadamu wa kawaida ana mikono miwili na ni mdogo kwa umbile ukilinganisha na tembo. They have the "Observation" but they may not have the "Explanation."
  MWISHO
  Nakupongeza kwa kazi nzito na uthubutu. Character animation si lelemama.

  @X-PASTER

  Una maana gani kuwa wazungu hawana 3D za vikaragosi? Shrek, SharkTale, Finding Nemo (hata Avatar) ni nini? Au unazungumzia 3D Stereoscopy, ambayo nayo pia inafanyika?
   
 7. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #7
  Apr 24, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kaka ahsante sana kwa maoni yako, ni matumaini yangu mtengenezaji wa filam hii, atayachukulia kwa uzito wake.

  Kuhusu utengenezajiwa 3D, nadhani ukunielewa...! Hapo nilikuwa nazungumzia kuhusu vigaragosi vya Simpson, ambavyo mtengenezaji alivitolea mfano na si hao kina Shrek na wengine.

   
 8. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #8
  Apr 24, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mkuu clip hipo hapo juu, unaweza kuicheza.
   
 9. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #9
  Apr 24, 2011
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Dr. Mhella karibu JF. Naona umeamua kujiunga ili kutupa upande wa pili wa shilingi na hivyo kutupa hata sisi tusiokuwa na ufahamu mkubwa wa masuala ya utengenezaji wa filamu mwanga kidogo.

  Karibu
   
 10. D

  Dr Mhella Member

  #10
  Apr 25, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakuu na wana harakati wa JF

  Inaonekama jamii forum ni tamu. sema sijaelewa bado discussion hii inataka kwenda mpaka wapi? yaani mwishoni tunatakiwa tuwe tumefanikiwa nini?

  Pili naomba moderator wa discussion hii anitumie email kwenye bonn-j@hotmail.com ili nimtumie DVD aone film mzima. Hii itasaidia kuweka balance kwenye maswali. nitumie address yako.

  Tatu, Je, kama ningeweka kwenye michuzi scene hii

  [video]http://youtu.be/LrZwfAFSlK0[/video]

  unafikiri kungekuwa na maswali yale yale au maswali yangebadilika?

  Nawashukuru sana wote kwa maoni na wala sijakasirika.

  Kuna mdau amegusia adobe audition. Yes I tried to use it. Actually I used various plug in za adobe audition ili kupata sauti mbali mbali. Kwa mfano sauti ya polisi alipogonga mlango ni product ya adobe audition. Sema hata adobe audition wapo nyuma sana kwenye kubadilisha sauti kutoka za kiume kwenda za kike. Movie ijayo ntatafuta mtu mwenye kipaji hicho. Hilo nimewaelewa na nalikubali. I also use a cubase. Ugekuwa umeiona movie nzima ningekuambia kila charactor na software niliyotumia.

  Pasaka njema wote.
  Bon
   
 11. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #11
  Apr 25, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160


  Mkuu nimeangalia hiyo clip, maoni yangu binafsi yanabakia kuwa yale yale.
  Ukiweza kurekebisha jinsi characters wako wanavyo zungumza na kutembea utakuwa umepiga hatua kubwa sana kwenye tasnia hii ya vikatuni.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #12
  Apr 25, 2011
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Karibu tena Bon,

  1. Kuhusu tunachotakiwa tuwe tumefanikiwa baada ya hii discussion ni suala lako mwenyewe. Lakini kubwa ni kuwa kama filamu yako ingekuwa katika development stages basi ungefanyia kazi mapendekezo waliyotoa wadau hapa, nadhani kuna baadhi ya mambo ambayo umekiri utayafanyia kazi. Hujaona kuwa hii tayari ni achievement?
  2. Actually hakuna moderator special wa discussion hii, ila kuna moderators (Mods) wa discussions zote kwa jumla, waweza kuwasiliana nao kupitia: support@jamiiforums.com
  3. Kuhusu watu wa blog ya Michuzi, ni vigumu na "hatari" kubashiri watakuwa na maoni au maswali gani, ungeweza weka link ya video zako huko ujioonee mwenyewe, lakini nikijuacho kuhusu JamiiForums (JF) ni kuwa kuna watu wanafahamu mambo hivyo expect challenges. You are lucky watu kutoa comments kwa kazi yako, mimi niliwahi weka thread yangu hapa wadau wakanyamaza tu bila kusema kitu wakati mimi nilitaka hata negative comments, the thread was:
  https://www.jamiiforums.com/sports-and-entertainment-forum/123854-nifanyieni-tathmini.html

  Pia kwa kuwa umesema utafanyia kazi suala la sauti basi sina neno tena. Mwanzoni nilidhani umefanya "compositing" ya characters differently na environment lakini nimeona environment nayo ni CG. Kilichonifanya nifikiri hivyo ni jinsi ambavyo suurroundings zinaswing tofauti na characters hasa ambapo tunaweza kuona miguu ikiwa imekanyaga ardhi. Angalia dakika ya nne na sekunde tatu(00:04:03); na dakika ya nne na sekunde ya 11 -12 (00:04:11-12) ya clip yako ya kwanza hapo juu (aliyoiweka X-PASTER mwanzo) ambapo nyumba ina-move tofauti na ardhi. Nadhani ni errors katika kuunga clips during compositing (if you did this in an external composting package like Ad AftrFx).

  I hope you will correct them in future. Otherwise, a nice try.
   
 13. D

  Dr Mhella Member

  #13
  Apr 25, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  It is nice to see the way ppo have responded. Dhumuni ya kuiweka scene ile izungumzwe ni kuona jinsi watu watakavyopokea wazo la kuwa na moviez za 3D animation hapa Tanzania. Naamini hakuna mtu atakayeweza kuicriticize movie yangu kama mimi mwenyewe kwani mimi ndo najua niliitengenezaje na kwa kutumia utundu gani. Hilo nalijua zaidi kuliko mtu mwingine yoyote yule.

  Labda tu nifafanue zaidi.

  Zaidi ya mimi mwenyewe kuact, ku-direct, kuandika script, etc etc. bado nilikuwa na tatizo moja la kuwa na miundombinu ya kisasa. Computer yangu ni PC ya kawaida kabisa tena ni microsoft windows 7 Home. Si professional. Ina RAM ya chini sana ambayo hata robo ya film nisingeweza kuisave ndani bila kuicompress. Ukicompress kitu inamaanisha unapoteza quality yake. baadhi la rangi zinaoverlap na nyingine hazionekani kabisa.
  Kama hilo tatizo halitoshi, nilikuwa na tatizo lingine ambalo nadhani ndo kikwazo kikubwa kwa watu wengine hasa hasa watanzania kushindwa kutengeneza film kama hizi. Sijui unajua in a professional movies kama hiyo ya avatar ingenichukua zaidi ya wiki moja ku-render kipisi cha nusu dakika? yaani baada ya kupoteza muda kwenye kuanimate na kutengeneza scene, ingenibidi kwa muda wa wiki moja niiache tu computer yangu bila kuitimia ili ifanye kazi ya kurender kipisi kidogo cha nusu dakika mpaka dakika moja. Hii inamaana mpaka movie ya saa moja na nusu iishe ningechukua zaidi ya miaka mitatu kwenye kuset rendering na kurender tu. Hapo bado ujazungumzia kuingiza sauti, na kama umekosea inabidi baada ya wiki moja ya kusubiri , mzee mzima unaanza upya kuedit kanusu dakika ambako katakuchukua wiki nyingine hivi hivi. JE, UNGEKUWA WEWE SI UNGEKATA TAMAA? Mimi sikukata tamaa. Akili ni nywele, nami ninazo:
  1) nilieliminate shades zote na kutengeneza artificial shading kwenye adobe premier. Kitu ambacho ni ubunifu mkubwa sana. kwa wale wanaojua animation na wanaotumia 3D max studio will be surprised how did I do that.
  2) Rendering was done in a preview setting. This means that all lighting effects was poor. Kwa anayejua 3D works ataelewa nilipoteza kiasi gani cha real effects. Hapa ndo unakuta mambo yote ya poor reflection na reflaction of materials yanaonekana. Lakini nilijaribu kutengeneza artificially.
  3) all heavy textures were eliminated at the same time I invested heavily in UV mapping. Hapa pia ilikuwa kazi sana kwani unapotoa shades na kurender kwa kutumia preview setting most materials textures zinatokea vibaya sana. UV setting was a problem kiasi cha kwamba sehemu nyingine ilinibidi nirender kwenye blue or green screen. This means that I had an extra job to do with Adobe premier and adobe photoshop to create 'artifical' materials and texture to bring into reality a clip.
  all in all, after 6 months I had a movie. Isn't it great?

  Ningeweza kuelezea mambo mengine mengi sema heri niishie hapa. Hizi criticism ambazo watu wamezitoa mimi nazichukulia kama a reflection of what I went through and what I finally have in the eyes of people. Kama unavyosema it is better to have criticism kuliko kupigiwa makofi ya kubeza wakati hata mwenyewe naona kuwa production was not easy. Sema tafuta FILM yote uiangalie ili uelewe ujanja wa mtu masikini aliyetengeneza movie ya kiswahili kwa kutumia MCHANGANYIKO ya softwares mbalimbali.
  All in all, I think it is something. kibongo bongo hivyo hivyo tumeingia kwenye 3D world. Na wengine wafuate nyao... Si mpaka mpate computer zenye nguvu sana kuweza kutegeneza 3D movies. Ni mahesabu tu ya kucheza na image... Akili ni nywele....

  Bon
   
 14. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #14
  Apr 26, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Well said mkuu, Kazi iliyobaki ni ya muhusika na mtengenezaji wa hiyo filam, kuzingatia au kutoyazingatia maoni yenu ni juu yake.
   
 15. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #15
  Apr 26, 2011
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Bon suala la Rendering ni kazi nzito. Labda kwa faida ya wengine niseme tu kuwa storage capacity ya Avatar ni takriban 1 Petabyte ambayo ni GB milioni, utanunua hard disk ngapi? Studios zilizoshirikiana kuitengeneza zinazidi 10 kuanzia New Zealand, US, Canada, UK etc. Hata animation yake imebebwa na Motion Capture technology ndo maana iko kama real kwenye movements. Rendering yake inahitaji render farms. Hapa mimi bado nahangaika na Duo Core PC, 3GB RAM, kasheshe nalipata. Kuna wakati nilitengeneza environment ya 3D ambayo ilikuwa na majani (grass) mengi, acha kabisa, frame moja (still picture moja) ilichukua karibu 5 hours kurender. Nimejaribu programu ya Cornucopia Vue XStream pamoja na Terragen, rendering inachukua muda mrefu sana. Inabidi tupate computers kama HP Z800 au MacPro ya processor 12, angalau. Tatizo bei.

  Kurender kwa Preview quality ni jambo la risk sana kwa sababu uzuri wa textures wote unapotea. Hata ufanye modelling nzuri kiasi gani, kuachieve photorealism ni lazima texturing nayo isaidie, sasa kama ulirender kwa preview quality, duh, its a great quality loss. Hata hivyo planning nzuri inaweza kuokoa kulazimika kurender kwa preview quality kama kuhakikisha hautumii texture za high resolution kwa characters au objects ambazo hazitakuwa karibu na camera. Kingine ni kuwa na multiple versions za characters na objects ambazo zina polygons chache (Low poly) ili kwa scene ya mbali na camera uzitumie. Kingine ni vizuri kujizuia kuweka Ambient Occlusion na Global Illumination unless ni lazima sana. Shadows pia zina tabia ya kuongeza rendering time. Pia suala la wewe kutoka kwenye 3DS max hadi Premiere bila kupita kwenye composting software ni lenye kuumiza sana. Kwa sababu essentially Premiere ni editing software ambayo mimi huitumia kwa kazi ya mwisho sana, unless sikukuelewa. Ungekuwa unatumia Cinema 4D ningesema upate support ya "Object buffer" ambapo ungeweza kuplay around na shadows, colours, motion blur etc more easily kwenye AfterFx. Sijatumia Apple Shake, Nuke, Combustion etc.

  Actually sikuipenda 3Ds Max japo bado naitumia kidogo na ndiyo niliyotumia muda mrefu zaidi kujifunza. Niko comfortable zaidi na Maxon Cinema 4D, iko more logically arranged. Nilirusha miguu kwenye Maya nikaishia kutoka na majeraha!!! Ntajifunza tena baadaye nikipata muda.

  Nafanyia kazi suala la texturing. Actually niko interested sana na kutengeneza photorealistic environments (hata abstract environments) kwa ajili ya sinema nayofikiria kuiandaa kwa ajili ya Dec 2012 - June 2013 release. Hivyo nafanyia kazi sana suala la texturing na matte painting/camera mapping. My full animated film is planned to be released in June 2014.

  However, fanyia kazi maoni ya wadau. Nadhani nikiiona sinema nzima nitakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kuichambua technically kwa kuzingatia pia ugumu wa mazingira ya utengenezaji. After 6 months naweza kuanza kupost character animations chache.
   
 16. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #16
  Apr 27, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mngeanza na kutengeneza clips za dakika 1 mpaka 3 au 5 kwanza kabla ya kurukia kutengeneza video yenye dakika 90.
   
 17. D

  Dr Mhella Member

  #17
  Apr 27, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
 18. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #18
  Apr 28, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mkuu hizo clip si kutoka kwenye hiyo hiyo filam yako, au...!?
   
 19. IrDA

  IrDA JF-Expert Member

  #19
  Nov 4, 2011
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 638
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 60
  Jaman kusema ukweli hii filamu inahitaji marekebisho makubwa hasahasa katika spidi and haina uhalisia.Mfano kwenye hiyo clip mtu anapigwa alafu reaction yake inachelewa kutokea.Vilevile marekebisho katika characters namaanisha sura zao
   
 20. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #20
  Dec 15, 2011
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  nimependa analysis yako vile vile muandaaje wa hii cartoon ajue target yake ni watz ambao wengi wao hawana hiyo anayoiita HD

  thanks XP
   
Loading...