FikraPevu: Polisi aliyefyatua bomu lililoua mwandishi akamatwa, kushitakiwa kwa mauaji

Haya mabadiliko kwenye nchi yanasimamiwa na Mungu mwenyewe, watapanga mambo yao sirini lakini yatawekwa hadharani! Wataendelea kunasa kwenye mitego walio tega wao, Mungu hadhhakiwi! Uwezo wao wa kudanganya tume u outsmart!
I highly appreciate your view, no one can deceive all the time.
 
Vema...wamfikishe mahakani pia askari alioyueuwa kule morogoro na hata Ramadhani Ighondu, aliyehusika katika sakata la Dr Uli.
 
Sasa kama askari aliyetekeleza mauaji anafahamika na wanajiandaa kumfikisha mahakamani, huo msururu wa tume za uchunguzi wa kazi gani? Hata hivyo natarajia kuona washitakiwa katika kesi hii ya mauaji ni pamoja na RPC wa Iringa.
Au tume zinalazimika kuwa nyingi ili kufanya cover up ya wahusika wakuu waliotoa amri ya kuzuia mikutano ya Chadema na kuua raia asiyekuwa na hatia.

Ndugu Mwita kesi za Mauaji haziendi hivyo. RPC labda wamuwajibishe lakini siyo kushitakiwa Kwa mauaji Kama vile unavyosema. Tume hapa ni kutafuta ukweli wa nini hasa kililijiri mpaka Huyo askari akafyatua bomu hilo. All in all atakujapatikana na hatiya ya kuua bila ya kukusudia. Mfano itakuwa katika pulukushani mkono ukagusa trigger kwa bahati mbaya na kusababisha mlipuko we bomu. Askari wa Tanzania wajifunze ukiwa na Siraha Kama aliylkuwa nayo mtuhumiwa wa mauaji, wajiepushe na ushabiki wa kupiga waandamanaji, Kwa sababu silaha inahitaji kuzingatia mashariti yote ya usalama.
 
Sasa Tume za nini wakati watuhumiwa wapo mahakamani?

Serikali yako ya magamba inatafuta namna ya kuwazuia wananchi kuendelea kuufichua ukweli wa mauaji ya Mwangosi.
Muda si mrefu utasikia suala hili liko mahakamani kwahiyo hakuna mtu wala chombo chochote kinachoruhusiwa kulijadili suala hili kwani kwa kufanya hivyo ni kuingilia uhuru wa maghakama.

Hii sinema inapoelekea itafanana na sinema ya kutekwa kwa Dr. Ulimboka, Kova kamuibua mkenya kutoka anakojua mwenyewe ili kuficha aibu ya polisi kumteka na ktaka kumuua Dr. Ulimboka.
 
KUSHO/KULIA sioni malumbano ya Police na wananchi ambao hata fimbo hawana. Nchimbi alishatapita kwa kusuma ni kitu kilichorushwa kwa nia ya kujeruhi Police. Hii leo kakamatwa askari alieua. Na bomu lile hurushwa ikiwa kuna wananchi wanaotaka fanya fujo, Je CHADEMA walienda kufanya fujo au kuzindua Tawi?

TANZANIA TANZANIA
 
Nimesikia kuna ffu walitoka dom,hatujajua anatoka wapi.
nafikiri ni muda muafaka sasa wa hawa walinda amani na utulivu wetu kuanza kuficha sura zao hasa wanapokuwa kwenye majukumu yao hasa yalio na sura za kisiasa kwa usalama wa familia na mali zao.......
 
Nape hachelewi kusema "huyu askari ni CHADEMA"

By the way, Tundu was very right. Mshika mtutu anajulikana, siasa za nini?
 
Ndugu Mwita kesi za Mauaji haziendi hivyo. RPC labda wamuwajibishe lakini siyo kushitakiwa Kwa mauaji Kama vile unavyosema. Tume hapa ni kutafuta ukweli wa nini hasa kililijiri mpaka Huyo askari akafyatua bomu hilo. All in all atakujapatikana na hatiya ya kuua bila ya kukusudia. Mfano itakuwa katika pulukushani mkono ukagusa trigger kwa bahati mbaya na kusababisha mlipuko we bomu. Askari wa Tanzania wajifunze ukiwa na Siraha Kama aliylkuwa nayo mtuhumiwa wa mauaji, wajiepushe na ushabiki wa kupiga waandamanaji, Kwa sababu silaha inahitaji kuzingatia mashariti yote ya usalama.

Nimekusoma mkuu, lakini sasa hebu angalia tena hii picha ili unishawishi kwamba huyo askari aligusa trigger kwa bahati mbaya. Inaonekana dhahiri shahiri kwamba jamaa alikusudia kumlipua na ndicho alichofanya.

Mkuu Pasco,

Kuna kisa kimoja kilitokea wakati wa vita vya marekani na vietnam.
Kuna Luteni mmoja alipewa amri ya kuteketeza kijiji chote. Yeye alichofanya aliua hadi kuku, na kila chenye uhai. Alikamatwa na kufunguliwa mashitaka na katika utetezi wake alisema aliagizwa afanye hivyo. Mahakama ilimdharau na kukataa utetezi wake kuwa alitakiwa atumie busara zaidi.
Huyo polisi anakila sababu ya kuhukumiwa kwa mujibu wa sheria bila kujitetea kuwa alikuwa anatekeleza amri, kwani angeona huyo anayetakiwa kumfyatulia bomu angefanya hivyo?
Japo ni kweli huyo askari mpuuzi asiyetumia akili anatolewa kafara ili kuficha walomtuma akiwemo huyo rpc aliyesema anaipenda kazi yake na anataka kustaafu kwa amani.
Hadi tuwatoe hawa maadui wa nchi hii ambao ni pamoja na CCM, polisi na huyu anayekuja sasa mshiri john tendwa ndo wahusika kamili watakuja patikana.

Yap. MESTOD - Ni kweli, hata wale marubani wa fighter jet za Libya walipewa amri ya kwenda kuangamiza waandamanaji huko Benghazi lakini wakatumia busara kutokutii hio amri na kutuliza hizo jet visiwa vya Malta...
 
Kwa jinsi picha za utekelezaji wa mauaji yale zilivyosambaa kwenye mitandao, polisi na serikali yake hawana namna yoyote ya kujinasua na unyama huu walioufanya. Kinachofanyika hapa ni juhudi za kujaribu kuwanusuru wahusika wakuu wa mauaji yale ambao ni Waziri Nchimbi(aliyetoa amri kwa IGP), IGP Mwema(aliyetoa amri kwa RPC) na RPC Kamuhanda(aliyetoa amri kwa askari wake).

Halafu katika watu wajinga Dr. Nchimbi anaongoza, eti anajikosha kwa kusema anashangaa kwa nini Dr. Slaa mpaka leo yupo nje wakati alitishia. Swali la msingi mbona hashangai mpaka leo hii kuwepo nje kwa muuaji wa Mwangosi wakati ushahidi upo wazi????

Kweli ukishangaa ya Mussa utayaona ya Farao!!!!
 
Huyo Askari aulizwe nani aliye mtuma katika tukio hilo la mauaji sababu inavyoonekana Askari huyu alikuwa na lengo lake.
 
Kushitakiwa kwa huyo Askari kuna mtia hatiani Chagonja ambaye aliudanganya umma kuwa Kifo cha Marehemu Daudi Mwangosi kilisababishwa na kitu kilichorushwa kutoka mbali.Huu ni Ushahidi tosha kwa wafuatao kuwajibika:
  1. Nchimbi
  2. Mwema
  3. Chagonja
  4. Kamuhanda
  5. The like
 
Ndugu Mwita kesi za Mauaji haziendi hivyo. RPC labda wamuwajibishe lakini siyo kushitakiwa Kwa mauaji Kama vile unavyosema. Tume hapa ni kutafuta ukweli wa nini hasa kililijiri mpaka Huyo askari akafyatua bomu hilo. All in all atakujapatikana na hatiya ya kuua bila ya kukusudia. Mfano itakuwa katika pulukushani mkono ukagusa trigger kwa bahati mbaya na kusababisha mlipuko we bomu. Askari wa Tanzania wajifunze ukiwa na Siraha Kama aliylkuwa nayo mtuhumiwa wa mauaji, wajiepushe na ushabiki wa kupiga waandamanaji, Kwa sababu silaha inahitaji kuzingatia mashariti yote ya usalama.
Realy!!??....

img.php
 
Nadhani si busara jambo hili kuendeshwa kisiasa... tutakurupuka halafu baadaye tuta'chemka'....waacheni wataalam wafanye kazi zao..ashtakiwe kwa uzembe kazini au mauaji ... haya ndio mambo ambayo wataalam watayajua...tujifunze kuwaheshimu wataalam.....mambo ya kitaalam tuwaachie wataalamu.....anyway tusiumize sana vichwa kwani hata chanzo chenyewe hakijakaa sawasawa

Tuwaachie wataalamu, wataalamu my foot.
Wataalamu hawa si ndio waliotuambia Ulimboka alitekwa na mkenya?! Yule askari Moro aljinyonga huku miguu imejikunja?! Muuza magazeti Moro alipigwa na kitu cha ncha kali?
Hii nchi tuna wataalamu gani ambao hata kuandaa kesi hawawezi hadi wamefanya Zombe kaachiwa huru!!
I hate this word Wataalamu,
By the way they rely for more than 45% on the evidence provided here in JF.
 
Back
Top Bottom