Mkuu wangu, kama hujapata picha ni kwamba, Tume hyo inakazi maalumu kuonyesha uhusika wa CDM katika "mauaji" hayo, ili itoe mapendekezo yake na hatimaye ndoto za Tendwa na wanaomtuma zitekelezwe na baadae waje kutunga hyo sheria ya kubana shughuli za siasa katika mda usio wa uchaguzi....
Kazi za shetani hufanyakazi kwa uwazi sana huku wao wakidhani ni siri mno.
nape anajua kila kitu toka mwanzo,walishapanga na wakakabizi kazi kwa polis.maana taarifa yake kwa vyombo vya habari alitabiri haya kwani toka lini akawa nabii????na kama polis wangekuwa hawafanyi kazi kwa kupendelea chama tawala,nape alipaswa awe mhojiwa wa kwanza wa mauaji ya morogoro,lakini hakuna kitu kama hicho.tendwa aache upuuzi,asimamie haki na wala sio kutishia kufuta chama.ukweli anaujua wote na anafanya kazi kwa kuongozwa na magamba.whatever they do,hawawezi kushindana na uma.Kama wauaji au muuaji ameshapatikana na hamna CHADEMA inakuwaje CHADEMA ikahusishwa na mauaji. Nape aseme sasa kwamba CHADEMA imehusika toka Morogoro hadi Iringa ila hakuna kiongozi wa CDM aliyekamatwa, hii ni kuchafuana. Ifike mahali CHADEMA wachukue hatua za kisheria pale wanaposingiziwa wameua ili kukomesha CCM kuichafulia CDM.
Askari alikuwa na bomu kwa ajili ya shughuli za kufungua tawi!!?? Askari aliiba bomu hilo wapi??? Na aliyesahinisha hilo bomu ali akatekeleze amri ya wakubwa ni nani!! Ilikuwa alitumie kwa kiongozi gani ambaye ni adui wa CCM na serikali kwa ujumla???
Kuanzia kesho utaanza kusikia "Suala hilo liko mahakamani msilijadili".. Tanzania inaongozwa kama movie ya Kihindi.
Ingizo jipya sokoni: Episode 2
Asante mkuu umeanza kuandika nilicho taka nami nikihoji sasa hizo tume zivunjwe tu zisiendelee kumaliza pesa za walipa kodi na mh Tundu lisu kasema zimeundwa kinyume cha sheria yani wameishiwa mpaka wana fanya maamuzi mabovu na ya hovyo kabisa pia mh.Mnyika aliwashauri tume ya nini wakati ushahidi upo? kamateni mhusika weka ndaniSasa kama askari aliyetekeleza mauaji anafahamika na wanajiandaa kumfikisha mahakamani, huo msururu wa tume za uchunguzi wa kazi gani? Hata hivyo natarajia kuona washitakiwa katika kesi hii ya mauaji ni pamoja na RPC wa Iringa.
Au tume zinalazimika kuwa nyingi ili kufanya cover up ya wahusika wakuu waliotoa amri ya kuzuia mikutano ya Chadema na kuua raia asiyekuwa na hatia.
POLISI ambaye alifyatua bomu kwa karibu na kusababisha kifo cha Mwandishi wa habari wa Channel Ten, Daudi Mwangosi, anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote, Fikra Pevu limefahamishwa.
alikuwa chini ya amr ya IGP na RPC.
Taarifa za kutoka Iringa zimeeleza kwamba kushitakiwa kwa askari huyo, kunafuatia kukamilika kwa uchunguzi wa awali ambao unathibitisha pasi shaka kwamba bomu alilofyatua ndilo lililosababisha kifo cha mwandishi huyo wa habari.
Imethibitishwa kwamba kilichousambaza mwili wa mwandishi huyo ni bomu maalumu linalorushwa kwa kutumia bunduki kwa nia ya kusambaza watu waliokusanyika kwa nia ya kutenda uhalifu na lilirushwa kwa karibu mno kinyume cha masharti na kanuni za matumizi yake.
Bomu hilo hutakiwa kurushwa kutoka umbali wa mita kati ya60 na 80, wakati askari huyo alilirusha kwa karibu mno na akimlenga mwandishi Mwangosi.
Katika tukio hilo, bomu hilo liliusambaratisha mwili wa Mwangosi na kumjeruhi ofisa mmoja wa polisi ambaye anaelezwa kutaka kumsaidia mwandishi huyo ambaye alikua akipigwa na polisi wenzake.
Marehemu Mwangosi aliuawa Jumapili iliyopita katika kijijini cha Nyololo, wilayani Mufindi, mkoani Iringa katika tukio ambalo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walikuwa wakifungua tawi la chama chao, huku Polisi wakitumia nguvu kubwa kuzuia uzinduzi wa tawi hilo.
Source: Fikra Pevu | Kisima cha busara!
Huu upumbavu uko Tanzania tu! Nikikumbuka ile kesi maarufu ya mauaji iliyomkabili O.J. Simpson huko Marekani na jinsi ilivyojadiliwa duniani kote wakati huo huo ikiwa Mahakama Kuu na hatimaye Mahakama ya Rufaa sina hamu. Naiona nchi yetu kama kuzimu fulani hivi.
Ha ha ha ha ha! Makalio Productions - Part II
Mkuu ukiiangalia Tanzania kwa jicho la tatu unaweza kuwanasa vibao watawala... Huwa nikiangalia Bunge naona kama kijiwe cha kuilinda na kuitetea serikali (Hasa spika na naibu wake)