FikraPevu: Polisi aliyefyatua bomu lililoua mwandishi akamatwa, kushitakiwa kwa mauaji

Mkuu wangu, kama hujapata picha ni kwamba, Tume hyo inakazi maalumu kuonyesha uhusika wa CDM katika "mauaji" hayo, ili itoe mapendekezo yake na hatimaye ndoto za Tendwa na wanaomtuma zitekelezwe na baadae waje kutunga hyo sheria ya kubana shughuli za siasa katika mda usio wa uchaguzi....
Kazi za shetani hufanyakazi kwa uwazi sana huku wao wakidhani ni siri mno.

Kama huo ndio mpango wao basi wamechemsha kabla ya utekelezaji wa mpango huo.
Pressure imekuwa kubwa kwa serikali hadi inaamua kujichanganya, kitendo cha kumshitaki muuaji tayari ni ushahidi tosha kwamba wahusika wakuu wa vurugu pamoja na mauaji ni jeshi la polisin likishirikiana na ccm na serikali yake.
 
Kwa kawaida askari anatimiza wajibu wake kwa amri, wa kwanza kushitakiwa sie aliyefyatua bomu bali aliyetoa amri!. Huyo mfyatuaji yeye ni mtekelezaji tuu!.

Askari polisi hawezi kushitakiwa kwa kutekeleza amri halali ya mkuu wake!.

Kwenye ile kesi ya mauaji Mwanza, baada ya kutokea vifo vya watuhumiwa wawili wa mauaji ya vikongwe, Bw. Masanja Mazengenuka na Isaack Mwana Mkoboko, Waziri wa mambo ya Ndani wakati huo Ali Hasan Mwinyi alijiuzulu, mkuu wa Polisi, Pundugu alistaafishwa kwa manufaa ya umma. Mkuu wa Usalama wa Taifa, Mzena alistaafishwa kwa manufaa ya umma. Walioshitakiwa ni RPC wa Mwanza, Cassian Mkwawa, RS wa Mwanza, Andrew M na DSO, Jemes Ihuya!.

Kama ni kweli polisi mfyatuaji risasi atapandishwa kizimbani, then RPC wake nae ndie amtangulie, huku waziri Nchimbi na IGP Mwema, bado wanasubiri nini?.

Pasco!.
 
Mmh, kuna kitu hawa jamaa wanakimbiza kukificha hapa. Iwaje hata kabla tume haijakamilisha riport tayari wanapeleka watu mahakamani? Hizo tume za nini sasa?

Katika nchi hii, adui yetu mkubwa ni CCM akitumia idara zake za polisi na msajili mshiri john tendwa kudumaza haki zetu.

Maelekezo:
1. Polisi vurugeni mikutano ya cdm na ikiwezekana ueni kabisa.
2. Msajili tangaza kukifuta cdm kwa madai kuwa kinasababisha vurugu.
 
Duuuuh polisi inahaha sana maana walizoea kubebwa na waandishi wa habari. Hakuna lolote katika hilo.
 
Kama wauaji au muuaji ameshapatikana na hamna CHADEMA inakuwaje CHADEMA ikahusishwa na mauaji. Nape aseme sasa kwamba CHADEMA imehusika toka Morogoro hadi Iringa ila hakuna kiongozi wa CDM aliyekamatwa, hii ni kuchafuana. Ifike mahali CHADEMA wachukue hatua za kisheria pale wanaposingiziwa wameua ili kukomesha CCM kuichafulia CDM.
 
Sasa kama askari aliyetekeleza mauaji anafahamika na wanajiandaa kumfikisha mahakamani, huo msururu wa tume za uchunguzi wa kazi gani? Hata hivyo natarajia kuona washitakiwa katika kesi hii ya mauaji ni pamoja na RPC wa Iringa.
Au tume zinalazimika kuwa nyingi ili kufanya cover up ya wahusika wakuu waliotoa amri ya kuzuia mikutano ya Chadema na kuua raia asiyekuwa na hatia.
Hizo tume ziliundwa kuficha kitu fulani. Ni baada ya kugundua kuwa hakifichiki ndiyo wamechukua mkondo mwingine. Hata hivyo, unajua kuwa wauuaji wa Kombe waliachiwa na kupewa mtaji na serikali?
 
Kama sio kiini macho ni sawa, lakini kuna wale askari waliomzunguka na kumpiga (kabla hajafariki) nao wakamatwe na kushitakiwa, kwa sababu walikuwa wanampiga bila kosa lolote na kisheria hawatakiwi kupiga. Kiongozi wao alikuwa anawakataza lakini wakakaidi amri hiyo na kuendelea kutembeza kipondo. nao wakamatwe iwe funzo kwa hawa wengine.
 
Sasa kama askari aliyetekeleza mauaji anafahamika na wanajiandaa kumfikisha mahakamani, huo msururu wa tume za uchunguzi wa kazi gani? Hata hivyo natarajia kuona washitakiwa katika kesi hii ya mauaji ni pamoja na RPC wa Iringa.
Au tume zinalazimika kuwa nyingi ili kufanya cover up ya wahusika wakuu waliotoa amri ya kuzuia mikutano ya Chadema na kuua raia asiyekuwa na hatia.

Tume ni muhimu kujua yaliyopelekea kutokea kwa tukio hilo na kufahamu kama wapo wengine ambao hawaku pull trigger lakini walisababisha kutokea kwa hili tukio.
 
Nadhani akili za wafuatao sasa zitafunguka...

...Nape Nnauye,.....Shigela wa uvccm,....John Tendwa,.....Mzee Wassira.....

Hawa wamekuwa ni "...wagumu kuelewa na wepesi kusahau..."
 
Kwa kawaida askari anatimiza wajibu wake kwa amri, wa kwanza kushitakiwa sie aliyefyatua bomu bali aliyetoa amri!. Huyo mfyatuaji yeye ni mtekelezaji tuu!.

Askari polisi hawezi kushitakiwa kwa kutekeleza amri halali ya mkuu wake!.

Kwenye ile kesi ya mauaji Mwanza, baada ya kutokea vifo vya watuhumiwa wawili wa mauaji ya vikongwe, Bw. Masanja Mazengenuka na Isaack Mwana Mkoboko, Waziri wa mambo ya Ndani wakati huo Ali Hasan Mwinyi alijiuzulu, mkuu wa Polisi, Pundugu alistaafishwa kwa manufaa ya umma. Mkuu wa Usalama wa Taifa, Mzena alistaafishwa kwa manufaa ya umma. Walioshitakiwa ni RPC wa Mwanza, Cassian Mkwawa, RS wa Mwanza, Andrew M na DSO, Jemes Ihuya!.

Kama ni kweli polisi mfyatuaji risasi atapandishwa kizimbani, then RPC wake nae ndie amtangulie, huku waziri Nchimbi na IGP Mwema, bado wanasubiri nini?.

Pasco!.

Mkuu Pasco,

Kuna kisa kimoja kilitokea wakati wa vita vya marekani na vietnam.
Kuna Luteni mmoja alipewa amri ya kuteketeza kijiji chote. Yeye alichofanya aliua hadi kuku, na kila chenye uhai. Alikamatwa na kufunguliwa mashitaka na katika utetezi wake alisema aliagizwa afanye hivyo. Mahakama ilimdharau na kukataa utetezi wake kuwa alitakiwa atumie busara zaidi.
Huyo polisi anakila sababu ya kuhukumiwa kwa mujibu wa sheria bila kujitetea kuwa alikuwa anatekeleza amri, kwani angeona huyo anayetakiwa kumfyatulia bomu angefanya hivyo?
Japo ni kweli huyo askari mpuuzi asiyetumia akili anatolewa kafara ili kuficha walomtuma akiwemo huyo rpc aliyesema anaipenda kazi yake na anataka kustaafu kwa amani.
Hadi tuwatoe hawa maadui wa nchi hii ambao ni pamoja na CCM, polisi na huyu anayekuja sasa mshiri john tendwa ndo wahusika kamili watakuja patikana.
 
Kwahiyo hili suala ndio linafikia mwisho wa kujadiliwa!!! Likishaenda mahakamani haliruhusiwi kujadiliwa tena!
 
Mkuu wangu, kama hujapata picha ni kwamba, Tume hyo inakazi maalumu kuonyesha uhusika wa CDM katika "mauaji" hayo, ili itoe mapendekezo yake na hatimaye ndoto za Tendwa na wanaomtuma zitekelezwe na baadae waje kutunga hyo sheria ya kubana shughuli za siasa katika mda usio wa uchaguzi....
Kazi za shetani hufanyakazi kwa uwazi sana huku wao wakidhani ni siri mno.

hiyo tume ikitoa mapendekezo hayo na muswada kupelekwa bungeni basi iambatane na muswada wa kupiga marufuku shughuli zote za polisi baada ya uchaguzi..TAFAKARI
 
Kwa kawaida askari anatimiza wajibu wake kwa amri, wa kwanza kushitakiwa sie aliyefyatua bomu bali aliyetoa amri!. Huyo mfyatuaji yeye ni mtekelezaji tuu!.

Askari polisi hawezi kushitakiwa kwa kutekeleza amri halali ya mkuu wake!.

Kwenye ile kesi ya mauaji Mwanza, baada ya kutokea vifo vya watuhumiwa wawili wa mauaji ya vikongwe, Bw. Masanja Mazengenuka na Isaack Mwana Mkoboko, Waziri wa mambo ya Ndani wakati huo Ali Hasan Mwinyi alijiuzulu, mkuu wa Polisi, Pundugu alistaafishwa kwa manufaa ya umma. Mkuu wa Usalama wa Taifa, Mzena alistaafishwa kwa manufaa ya umma. Walioshitakiwa ni RPC wa Mwanza, Cassian Mkwawa, RS wa Mwanza, Andrew M na DSO, Jemes Ihuya!.

Kama ni kweli polisi mfyatuaji risasi atapandishwa kizimbani, then RPC wake nae ndie amtangulie, huku waziri Nchimbi na IGP Mwema, bado wanasubiri nini?.

Pasco!.

kifupi amri ya kufyatua bomu la aina hiyo ni mita 60 hadi 80, hivyo mtoa amri hana hatia hapo kwani bomu lilifyatuliwa usawa wa mt 1 hivi
 
Mkuu wangu, kama hujapata picha ni kwamba, Tume hyo inakazi maalumu kuonyesha uhusika wa CDM katika "mauaji" hayo, ili itoe mapendekezo yake na hatimaye ndoto za Tendwa na wanaomtuma zitekelezwe na baadae waje kutunga hyo sheria ya kubana shughuli za siasa katika mda usio wa uchaguzi....
Kazi za shetani hufanyakazi kwa uwazi sana huku wao wakidhani ni siri mno.
wapeleke bungeni wakati huo huo muswada wa kusitisha shughuli za polisi after election!
 
Kuanzia kesho utaanza kusikia "Suala hilo liko mahakamani msilijadili".. Tanzania inaongozwa kama movie ya Kihindi.
 
Duuuuh polisi inahaha sana maana walizoea kubebwa na waandishi wa habari. Hakuna lolote katika hilo.

Kwa jinsi picha za utekelezaji wa mauaji yale zilivyosambaa kwenye mitandao, polisi na serikali yake hawana namna yoyote ya kujinasua na unyama huu walioufanya. Kinachofanyika hapa ni juhudi za kujaribu kuwanusuru wahusika wakuu wa mauaji yale ambao ni Waziri Nchimbi(aliyetoa amri kwa IGP), IGP Mwema(aliyetoa amri kwa RPC) na RPC Kamuhanda(aliyetoa amri kwa askari wake).
 
Hapo pana tatizo maana wangekamatwa wote 8 wajieleza tukisema yule wa bomu ndio akamatwe ni uonevu na hata mahakama itamwachia huru tu kama akina zombe. Maana atajitetea kuwa mwangosi alisakufa baada ya kupigwa virungu vya kichwani ama mateke mbavuni.yeye alifyatua tu kama kumtisha.mi vizuri wale wote waliohusika wakakamatwa kwanzia igp,waziri kushuka ngazi ya chini hili halikua jambo la askari mmoja tena inasemekana ni askari wa dodoma ndio waliofanya hizo vurugu.
 
Back
Top Bottom