Fikra

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,653
Hata mbwa anaweza kufundishwa na kufanya baadhi ya mambo, binadamu anapaswa kuwa juu ya kufundishwa.

ANAWAJIBIKA kwa kutumia akili yake mwenyewe kuzalisha maarifa sio kupokea tu maarifa.

Anayepokea tu maarifa pasipo kuzalisha maarifa bado ni mfungwa.

Ana ufungwa ule ule ambao anao mbwa aliyefundishwa kutenda jambo fulani na kuwa analifanya hilo kila siku.

Maarifa yote ni zao la fikra kwahiyo usidharau fikra wala usiache kufikiri na kutegemea fikra za watu. Dare to use your own mind. utegemezi wa fikra ni mbaya sana na unazuia ukuaji wa binadamu na mataifa.

Ukweli ni kwamba tumekuwa taifa la kupokea maarifa na sio kuzalisha maarifa. Maarifa yote tuliyonayo na tunayofundishwa shuleni mengi ya hayo chanzo chake sio sisi. Ni fikra na mawazo ya watu wengine.Tumeyapokea tu na kuwa trained kufanya jambo hili na lile.

Kuna shida gani kwenye akili zetu hadi tunashindwa kuzalisha maarifa ya kutosha? Hatujiamini?

Na hii ndio sababu inayotufanya kuwa maskini kila kukicha.

Tunapokea pasipo kutoa. Mataifa yanayozalisha maarifa they will always be superior to those who do not.
 
Asante sana mleta mada. Nimeshangazwa na ufundi wako wa kuandaa bandiko kiasi kwamba ukianza kulisoma toka juu kushuka chini na kutoka chini kwenda juu bado bandiko linakuwa na mtiririko wa kimantiki.
===
Jambo la msingi sana, na ambalo huwa nalipigania sana kuhakikisha tunajitegemea na ndicho kisa cha ID hii ya TUJITEGEMEE.
 
18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom