Fikra za waafrika "wanaojiita" wasomi ndizo zinazolidumaza bara letu

Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,684
2,157
Ndugu zangu, mliowengi mtakuwa mliisikia kauli ya Spika wa bunge kuhusu kuwaamini wenye vyeti vyenye GPA nzuri za first class kwamba ndio "pekee" wanatakiwa kuaminiwa na serikali na kutumwa kwenye "negosiesheni" panakuwepo na majadiliano yanayohusu maslahi ya Taifa lake.

Hakika sipingani na mawazo yake ila namkumbusha tu kwamba cheti pekee sio kipimo halisi cha kupima uwezo binafsi wa mtu kwenye kujadili hoja yoyote

Leo pia nimeona post inayomzungumzia Dr. Mwakyembe akisema yeye ana digrii nne hivyo haiingii akilini mtu kama huyo akosolewe na msanii tu ambaye hana hizo shahada nne.

Naomba tusaidiane hili swali, hivi ni kweli asiyemsomi hawezi kumkosoa msomi?

Ni kweli wasomi wanafahamu kila kitu kiasi cha kutokosolewa na hawa wasiokuwa wasomi wa ngazi za juu?

Screenshot_20191115-194251.jpeg
 
Ipo siku watakuja watu wenye akili na watawaonesha jinsi wazungu walivyofanikiwa kuiangusha Afrika kwa jina la wasomi wakati ukweli ni kwamba kuna tofauti kubwa sana kati ya "usomi na akili"

Wasomi wengi sana hawana akili ijapo wana GPA kubwa na degrii nyingi.Hili halitaeleweka sasa hivi kwa vile mifumo inayokandamiza watu wenye akili inalindwa sana kwa hoja za nguvu na nguvu za dola.

Uwezo wa mtu kukumbuka aliyofundishwa siyo kipimo cha akili.Watu wenye uwezo huo ni wengi sana mfano mmoja wapo ni Dr.Shika.

Naamini ipo siku nchi itapata kiongozi mwenye akili.Atakuwa dikteta.Kwa sababu hawa wanaojiita "wasomi" wataanza kuleta hoja zao za kimajungu zilizojaa mashairi matamu yasiyo na msaada wala tija.Atawalazimisha kufuta ujinga mwingi unaopoteza muda wa watoto wetu mashuleni ili wapate mnachoita degree.

Watu wanaishia kuelezea jinsi panzi anavyopumua,mende anavyokula kinyesi,Mbu anavyonyonya damu,halafu dawa za kuua mende zinaletwa na wachina,dawa za kutibu malaria zinaletwa na wachina!Huu ni usomi au upu.mbavu?

Wasomi?Tungekuwa tunadaiwa madeni makubwa kiasi hiki Afrika?

Naamini wasomi wako China siyo ujinga ujinga wetu huku mivyeti rundo ila hakuna lolote unaweza kuwaonesha watu umefanya.

Nchi haiihitaji watu wenye vyeti na GPA kubwa,nchi inahitaji wabunifu,wagunduzi,na watu wanaoleta masuluhisho ya changamoto tulizo nazo kama vile,umaskini,ujinga na maradhi,njaa na ugomvi wetu wenyewe kwa wenyewe kugombea madaraka
 
Ndugu zangu, mliowengi mtakuwa mliisikia kauli ya Spika wa bunge kuhusu kuwaamini wenye vyeti vyenye GPA nzuri za first class kwamba ndio "pekee" wanatakiwa kuaminiwa na serikali na kutumwa kwenye "negosiesheni" panakuwepo na majadiliano yanayohusu maslahi ya Taifa lake.

Hakika sipingani na mawazo yake ila namkumbusha tu kwamba cheti pekee sio kipimo halisi cha kupima uwezo binafsi wa mtu kwenye kujadili hoja yoyote

Leo pia nimeona post inayomzungumzia Dr. Mwakyembe akisema yeye ana digrii nne hivyo haiingii akilini mtu kama huyo akosolewe na msanii tu ambaye hana hizo shahada nne.

Naomba tusaidiane hili swali, hivi ni kweli asiyemsomi hawezi kumkosoa msomi?

Ni kweli wasomi wanafahamu kila kitu kiasi cha kutokosolewa na hawa wasiokuwa wasomi wa ngazi za juu?

View attachment 1263906
Wanaojiita Wasomi ndio wametufikisha hapa kwa kufanya mambo ya hovyo sana,bora hata darasa la 7 msukuma kasheku ambaye ametengeneza ajira nyingi kupitia kampuni zake kuliko hata huyo mwakyembe mwenye digrii zake nne zisizokuwa na msaada wowote kwenye jamii zaidi tu msaada kwa familia yake kwa kujikombakomba kwa meko.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom