kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,404
- 7,188
Nimesikitika sana leo kumuona Raisi Magufuli akiongelea TTCL kijamaa. Mawazo yake ambayo anafikiri ni mazuri kwa nchi si mazuri na ni mabaya sana kwa uchumi wa mtaji. Simshangai maana watu wengi sana Tanzania bado wanajua uchumi kwa kujifurahisha na kushabiki lakini uchumi wa mtaji una utaalamu wake ambao usikoufuta utapata shida kama nchi.
1. Ni kujua kwanini TTCL iko nyuma mpaka leo pamoja na kuwa na yote. Ni kwasababu simu ni technology na huwezi kubaki tu Tanzania ukafikiri utafaniliwa hivyo hata tutoe pesa hatuwezi kutoa pesa kwa TTCL kiweza kushindana na Voda phone kwenye technology.
2. Kampuni ambayo inahitaji mgao haitakiwi kutoa dividends kama TTCL kwa serikali. Kampuni ambayo inakuwa inabakiza mtaji kukuza kampuni au kitaalaumu wanaita retained earnings. Yaani kampuni ikishapata net profit inaamua igawe au ibakie na faida ili iwekeze kwenye kampuni. Cha kushangaza wakati huohuo TTCL inaomba mtaji😂 yaani ni kichekesho.
3. Ukichukulia kodi za wote waajiriwa, kodi za kampuni na maendeleo kampuni za simu zina faida kubwa sana nchini lakini cha ajabu serikali imeanza kuwapa shida wakurugenzi na kesi za bandia ili tu kusaidia TTCL. Serikali mjue hakuna kampuni itafanikiwa Tanzania kijamaa na ni vizuri mruhusu ushindani zaidi badala ya kukumbatia kampuni ambayo itakuwa hasara kwa taifa. Yaani tupewa ths billion 2 halafu wanaomba billioni 60 kama mtaji.
Wasiwasi wangu mkubwa ni fikra ambazo si za kweli na hazijawahi kufanikiwa kwamba kampuni za serikali ni nzuri kwa jamii hasa kwa nchi ambayo hatuna uwekezaji wa kutosha. Haya ndiyo yaleyale ya korosho.
Wala hujui unapotosha tu. Kampuni inayohitaji mtaji kutoka kwa wenye kampuni haizui kutoa gawio kwa mwenye au wenye kampuni. Ni uamuzi wa wakurugenzi na inategemea mtaji unaohitajika ni kiasi gani na lengo lake ni kufanya nini.
Halafu hujui ujamaa ila umedhurika na propaganda tu. Kampuni za umma kwa ajili ya kutekeleza majukumu maalum hata katika nchi za kibepari zipo. Tatizo hapa kampuni shindani binafsi zinaweza kuhujumu kirahisi kampuni za serikal ili ziweze kuhodhi soko kutokana na ufisadi miongoni mwa watumishi wa umma. Awamu hii imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupambana na ufisadi.