Fikra za Magufuli kwenye TTCL hazina tija

pombe anaamini mashirika yote na taasisi zote binafsi na kibiashara zikifa ni faida kwa taasisi za serikali maana zitakosa mpinzani..
kkkk
bado serikali inahitaji wawekezaji na kodi !
TANESCO lini kutoa dividend ?
Huko ni kujitekenya tu, unawapa rudhuku wanakupa dividend hapo hapo wanakuomba mtaji. Hayo ni mawazo mgando waache makampuni yajiendeshe kibiashara.
 
Serikali iachs biashara na iwekeze kwenye sera za kodi, uwekezaji. Land, banking na elimu kwa vijana pamoja na ujenzi. Serikali ifanye vitu ambavyo watu hawaweI kufanya wenyewe na sio biashara ambazo hazina tija
Mkuu thumb up, umeongea mambo ya msingi kabisa, tena apa kwenye last lines. Serikali iwezeshe biashara sio ijiingize kwenye biashara ambazo hata watu binafsi au mashirika binafsi yanaweza kuzifanya.
 
Chief hili bandiko lako linaonyesha jinsi gani haupo aware na jinsi dunia ya leo inavyoendeshwa yaan karne hii ya ishirini na moja bado una mawazo ya kutoa huduma bila faida? Na km ttcl wana mawazo km hya basi they are doomed to fail!
Ndo hapa usishangae serikali ipo busy kutoa rudhuku kwenye mashirika yake na bado wanaendelea kufanya vibaya sana.
 
Mkuu Kamundu, I'd like to differ, rais Magufuli hajazungumzia ujamaa, amezungumzia uzalendo. Hii inaitwa affirmative action, hiki ndicho nchi zote zinazotaka maendeleo ya kweli zilianza, unajenga chako, unapenda chako, unatumia chako. Huo ndio uzalendo wa kweli wa nchi yako.

Kwa hili hongera sana Rais Magufuli.
P
Anko Paschal nawezaje kupenda changu wakati hakina ubora unaotakiwa?
 
Mh. Rais angejifunza mawazoya Deng Xiao Ping alipoona ujamaa unazorotesha Faida za makampuni ya umma, alitoa kauli mwongozo kuwa (it doesn't matter whether a cat is black or white,provided it cathes a mouse) .Akaruhusu biashara mchanganyiko na kukumbatia ubepari. Na huyo ndi

o father of China's economic miracle. Alipandisha uchumi Wa China hadi tunavyouona Leo. Sasa rais wetu bado ana hangover ya ujamaa Wa kina Mao na Nyerere hadi leo? TTCL hata afanyeje haiwezi kuwa mfano bora huko mbele hata afanyeje. Labda Mh.
kama ameamua kuwa rais wa majaribio, na kila jaribio ni failure kwake. Korosho zingempa funzo ambako aliachia majeshi yalisimamia kikamilifu lakini Leo tunaambiwa hujuma kubwa imetawala huko na wanajeshi wapo tu. Kwanza jeshi limesomea kupigana vita ya silaha sio uchumi. Sana jeshi litapakwa matope nalo,which is very sad. Mimi nadhani miaka iliyobaki angetulia akawa anasikia watalamu tu. Akiendelea na staili ya amri basi anataka watanzanja tuogope rais Wa aina hadi miaka 50 ijayo.
 


Nimesikitika sana leo kumuona Raisi Magufuli akiongelea TTCL kijamaa. Mawazo yake ambayo anafikiri ni mazuri kwa nchi si mazuri na ni mabaya sana kwa uchumi wa mtaji. Simshangai maana watu wengi sana Tanzania bado wanajua uchumi kwa kujifurahisha na kushabiki lakini uchumi wa mtaji una utaalamu wake ambao usikoufuta utapata shida kama nchi.

1. Ni kujua kwanini TTCL iko nyuma mpaka leo pamoja na kuwa na yote. Ni kwasababu simu ni technology na huwezi kubaki tu Tanzania ukafikiri utafaniliwa hivyo hata tutoe pesa hatuwezi kutoa pesa kwa TTCL kiweza kushindana na Voda phone kwenye technology.

2. Kampuni ambayo inahitaji mgao haitakiwi kutoa dividends kama TTCL kwa serikali. Kampuni ambayo inakuwa inabakiza mtaji kukuza kampuni au kitaalaumu wanaita retained earnings. Yaani kampuni ikishapata net profit inaamua igawe au ibakie na faida ili iwekeze kwenye kampuni. Cha kushangaza wakati huohuo TTCL inaomba mtaji😂 yaani ni kichekesho.

3. Ukichukulia kodi za wote waajiriwa, kodi za kampuni na maendeleo kampuni za simu zina faida kubwa sana nchini lakini cha ajabu serikali imeanza kuwapa shida wakurugenzi na kesi za bandia ili tu kusaidia TTCL. Serikali mjue hakuna kampuni itafanikiwa Tanzania kijamaa na ni vizuri mruhusu ushindani zaidi badala ya kukumbatia kampuni ambayo itakuwa hasara kwa taifa. Yaani tupewa ths billion 2 halafu wanaomba billioni 60 kama mtaji.

Wasiwasi wangu mkubwa ni fikra ambazo si za kweli na hazijawahi kufanikiwa kwamba kampuni za serikali ni nzuri kwa jamii hasa kwa nchi ambayo hatuna uwekezaji wa kutosha. Haya ndiyo yaleyale ya korosho.

"Business is competition" where there is no competition there is no business. they have to create strategies how to beat competition the problem here is the working team for TTCL they have to work on USP unique selling point.
 
Haya mashirika ya umma yaliishafeli long time nakumbuka tulikuwa nayo zaidi ya 400 wakati wa Nyerere na yenyewe ndio yaliyochangia tukakosana na IMF na WB kipindi kile.

Hakuna haja ya kuwa na haya mashirika ktk dunia ya leo kwani leo watatudanganya wanapata kafaida kumbe ni hesabu za kuchakachua tu make hata Financial Statement tu haionekani.

Haya mashirika ni hasara kubwa kwa taifa. Serikali iachane nayo na ihimize more private investment, unless wawe wanavizia kuchumapo pesa ili kuisaidia ccm wakati wa kampeni.
 
Kinachokutatiza ni kitendo cha kugawa bilion 2.5 wakati inaomba bilioni 60.

Kimsingi unakubali kwamba TTCL sasa haiendeshwi kwa hasara. Hivyo, ni wazi unajua kuwa hili si tatizo la TTCL kwani wakipewa hizo bilioni 60 watagawa dividend kubwa zaidi unayotaka wewe.

Kumbuka hata kampuni kubwa binafsi unazodhani zinafaulu, nyuma yake wanafanya kama TTCL. Wanatengenezewa budget kutoka nje, wao wanaita "Group" sema tu wakiomba bilioni 60 wanazipewa wakati management ya TTCL haipewi.

it is that simple.


Yaani kampuni ikishapata net profit inaamua igawe au ibakie na faida ili iwekeze kwenye kampuni. Cha kushangaza wakati huohuo TTCL inaomba mtaji😂 yaani ni kichekesho.
 
wasitoe gawio kabisa kwa maana hata mtaji hawana wanaomba!! kuna maana gani ya kutoa gawio ikiwa ukishalitoa unarudi kua omba omba, ni sawa na kupangisha nyumba yako yote afu huna pa kuweka hata ubavu.
Mkuu biashara ndiyo ilivyo unatoa gawio kwa wamiliki then unaongeza mtaji kwa kuomba mkopo Benki ili ukuze mtaji
 
Mkuu biashara ndiyo ilivyo unatoa gawio kwa wamiliki then unaongeza mtaji kwa kuomba mkopo Benki ili ukuze mtaji

Sio kweli hakuna biashara ya hivi kama unahitaji mtaji kukuza biashara hutoi gawio. Ukishapata faida unabaki na faida retained earnings badala ya kitu ambacho wanaita dividend payout. Mara nyingine dividend zinalipwa na kampuni ambazo hazikui. Kazi kubwa ya kampuni sio kupata faida bali ni kuongeza thamani ya kampuni.

Soma hapa chini

Why Some Companies Choose Not to Pay Dividends With Their Profits
A company that is still growing rapidly usually won't pay dividends, because it wants to invest as much as possible into further growth.
Even a mature firm that believes it will do a better job of increasing its value (and therefore a better job of increasing its share price) by reinvesting its earnings will choose not to pay dividends. Companies that don't pay dividends might use the money to start a new project, acquire new assets, repurchase some of their shares or even buy out another company.
The choice to not pay dividends may be more beneficial to investors from a tax perspective. Non-qualified dividends are taxable to investors as ordinary income, which means an investor's tax rate on dividends is the same as his marginal tax rate. Marginal tax rates can be as high as 37% (as of 2018). For qualified dividends, the tax rate is either 0%, 15%, or 20%, depending on the marginal income tax bracket that the investor falls under. The capital gains on the sale of appreciated stock can have a lower, long-term capital gains tax rate (typically up to 20% as of 2018) if the investor has held the stock for more than a year.
 
Mawazo ya wengine hapa hayana facts zozote Pascal Mayalla tuanze kupeana ukweli hapa

1. Sera za Nyerere za uchumi zilishidwa kuleta maendeleo kwa nchi yetu. Uzalendo sio chakula hivyo uzalendo wa kweli ni pamoja na kuleta maendelo watu waweze kula. Wakati Nyerere anaondoka Watanzania walikuwa na mgao wa Chakula, wanakula unga wa yanga na nchi ilikuwa haina pesa. Isitoshe kwa uzalendo wake Nyerere alistaafu kwa manufaa ya uma na akaita kustaafu kungatuka. Sababu kubwa ni alishidwa kukubali ukweli kwamba uchumi ni wa mtaji ndiyo unaleta maendeo na prove kwamba wakina Mtei walikuwa sawa kwenye uchumi.
2. Hii mitandao tunayotumia hapa, WhatApp, Word na Excel za Microsoft, ndege zote, magari yote, technologia ya umeme, technologia ya madawa, vifaa vya hospitali, dawa za mswaki za kila siku, betri zote, vinywaji kama coca na pepsi, kampuni za bia, technologia ya simu. Hivi vyote vimeletwa na hao mnaowaita mabeberu sasa visingekuwepo tungekuwa wapi!.

Ni kwanini mnaishia kwenye simu ? Kwanini tusiwe na kampuni ya pombe zetu za kienyeji tukaacha kunywa bia za mabeberu, kwanini tusiwe na kampuni yetu ya kutengeneza ndege badala ya kununua ndege Billioni 400?, kwanini tusiwe na kampuni yetu ya chai watu wasitumia coca na pepsi, kwanini tusipige miswaki kama zamani na miti badala ya kutumia colgate. Mimi naona Watanzania wengi 67% wana miaka chini ya 24 yaani wamezaliwa 1995 na kuendelea mnawachanganya na siasa zenu za uzalendo ambazo hazina msingi wala tija kwa taifa la siku hizi.

Mwisho niwape somo uzalendo wa siku hizi ni upi
Uzalendo siku hizi sio kuwa na kampuni ya kitaifa bali kuwawezesha Watanzania. Mengi mfano alikuwa na kampuni ya coca cola ambayo alipata kibali kutoka kampuni ya coca cola ya Atalanta USA. Kampuni yake ililipa kodi, kutoa kazi na wamesaidia Watanzania kuliko kampuni ya pombe ya Tanzania ya kibuku. Hatuwezi kusema kwa uzalendo tupendelee kampuni ya kibuku kwasababu tupende chako. Pamoja na ukweli kwamba Mengi alikuwa anapata share ndogo sana kwenye coca cola huu ni uzalendo ingawa tumewatajirisha mnaowaita mabeberu is win win. Hivyo hata voda ni yetu inaajiri pale, inalipa kodi, inasaidia jamii , imeleta Mpesa na tumeona faida yake. Voda imefanya makubwa sana kuliko TTCL hatuwezi kusema kwamba wafanyakazi pale sio wazalendo kuliko wafanyakazi wa TTCL sio sawa. Saa tunaona minyanyaso na kusahau hizi kampuni za nje ambazo zimetuletea kila kitu na tunawaita mabeberu. Tujiulize ni kampuni gani zinaajiri Tanzania kuliko kampuni za bia, simu na ujenzi? pesa za kodi za hizi kampuni ndiyo zinaenda kusaidia kampuni ya kizalendo ya TTCL ambayo tena inarudi kushindana na walewale waliompa mtaji badala ya kuwasaidia wafanikiwe zaidi. Hii ni kujipiga risasi mwenyewe mguuni
 
1. lengo la makampuni ya umma ni kutoa huduma( service) zaidi ya faida. Huduma inayotolewa na makampuni ya umma ni muhimu kuliko nia na lengo la kupata faida. Huduma hiyo inatakiwa kuwa na ubora na viwango kama kampuni binafsi. makampuni ambayo yanatumia faida iliyobaki yaani retained earning kukuza mtaji na faida ni binafsi. ni haki ya msingi kwa TTCL kuomba mtaji kwa sababu lengo lake kubwa ni kutoa huduma na si faida.

2. itakuwa ni ujinga mkubwa kulinganisha makampuni yenye malengo makuu tofauti, moja inalengo la kutoa hudama na nyingine lengo lake kuu ni kupata faida. hakuna sehemu serikali inapotaka kushindanisha TTCL na kampuni binafsi kwa sababu moja inapeleka huduma mpaka vijijini na nyingine inatafuta wateja mijini tu kwa lengo la kupata faida.

3.kampuni ni zaidi ya wakurugenzi waliopo, hivyo kuhusisha wakurugenzi wa hayo makampuni mengine waliofunguliwa mashtaka na kampuni zao ni kukosa weledi. kama serikali ingekuwa na nia ya kuua kampuni nyingine ibaki TTCL tu, ingeweza na taasisi moja kwa moja na sio mkurugenzi mmoja ambaye ni mfanyakazi tu na si mwanahisa.

Hiyo namba 2 katafute wajinga uwaambie huo upuuzi. Katafute mwanakijiji mwenye line ya TTCL kisa wamepelekewa hiyo huduma kila kijiji na TTCL.
 
Mkuu biashara ndiyo ilivyo unatoa gawio kwa wamiliki then unaongeza mtaji kwa kuomba mkopo Benki ili ukuze mtaji

Mawazo kama haya yanapatikana kwa watu wenye mawazo ya kizee au kijamaa tu.
 
Kampuni za ndani lazima uzilinde bila hivyo zitakufa,huwezi kusema TTCL ishindane na Vodacom,ambayo ni ya UK/south Afrika,wanatuzidi mtaji na Tekinoloja.
Halotel ni kampuni ya Nchi ya Vietnam,haikufika hapo kwa kupambanishwa na makampuni makubwa ya kimagharibi.ilisaidiwa.
Hatuwezi kusema TTCL haina kitu,Airtel/celtel imezaliwa kutoka TTCL kwa wizi wa kutisha uliofanywa na wabongo wenzetu,
Majizi,mafisadi yafungwe,tutafute Tekinolojia,mbona CRDB,TCC,NHC wameweza?tuondoe ukiritimba,siasa katika mambo ya kitaalamu,
Kuna kampuni kibao zawatu binafsi,zinaanzishwa,na zinaendeshwa vzr,na zinakuwa na mafanikio,kwanini serikali inashindwa kusimamia kampuni za umma,
Ikibidi kutafuta ma CEO kutoka sekta binafsi,tufanye hivyo,ila walioifikisha TTCL hapo ilipo,ni sisi wenyewe,

Sifa ya kuwa CEO kwenye kampuni ya umma ni kuwa kada wa ccm tena uwe ni mzee wa ndio mzee. Mambo ya competency Ni huko kwa watu wenye mitazamo mbali.
 
Kwanza
Gawio lenyewe mwaka mzima ni idd usd one million, TTCL wangeendelea kukodisha services zao kwa makampuni binafsi wangepata zaidi ya hiyo na hayo makampuni yangetengeneza faida maradufu, tunaingizwa chaka kwa kuamini TTCL inaweza kushindana na sector binafis hii ndoto inatoka kuzimu, vodacom tanzania mwaka 2018 walitengeneza faida ya 134 billioni, na leseni hiyo waliinunua kutoka TCRA kwa usd zaidi ya 20 mil. Nashindwa kuelewa tunataka nini, watoto kazi hawana uchumi bado tunaupigia punyeto
Yes. We need wa baba kama wewe. Ambao wakiwa kwenye mawazo yao wanawaza wajukuu wa ndugu wao. Hawa wanawaza kupigiwa makofi na wasioelewa lakini wanatuharibia nchi.
 
Mkuu Mag 3, safari ni hatua, kwenye UZALENDO wa kupenda chako, we are long overdue, tumechelewa sana kwanza, uzalendo kama huu ulikufa na Nyerere sasa umefufuliwa na Magufuli, tunaanza mdogo mdogo katika madogo yaliyo ndani ya uwezo wetu, tunaanzia kwenye huduma, services provisions, ambapo hata mimi na kikampuni changu kile ki PPR, ni muhanga, taasisi za serikali zimeelekezwa kutangaza na TBC na magazeti ya serikali hivyo PPR, chali.

Tukimaliza kwenye huduma tunakuja
Kwenye bidhaa, Watanzania tupende kutumia bidhaa za nyumbani. Lushoto apples zinasitawi sana, hizi apples mabarabarani, zinatoka South. Nenda Mlimani City utakuta hadi viazi mbatata ni imported, KFC wanatumia imported chickens. What we need is tupende bidhaa zetu ili tukidhi demands ambayo inajazwa na imported products.

Kiukweli tunahitaji elimu ya uzalendo na uhamasishaji uzalendo ili kujenga Tanzania ya wazalendo.
P

Mkuu Paskali sasa hivi ni ngumu kutofautisha uzalendo na ujinga.
 
Shida Raisi wa nchi akishasema mimi dio mwenyekiti wa chama basi siasa inaanza.Tukifanya kazi kwa utaifa na sio chama au serikali ya Fulani nahisi mambo yatakwenda vizuri kwa kuweka wataalam sahihi kunusuru mashirika yetu na sio kama tunachokiona.

Nchi ikiongozwa na rais mwenye mitazamo ya kijamaa, sifa ya kwanza sio utaalamu bali ni itikadi yako.
 
Hizo fikra haziwezi kufanya kazi. Huko Rufiji na Mafia hata vodashop au tigoshop hakuna. Mitandao inayoshika ndio hio.
Ni kuwasumbua tu viongozi wa huko kuwa na line za ttcl.

Na hizo pesa wanazoomba TTCL utakuta 70% ni gharama za upembuzi yakinifu.

Amekataza watu kwenda nje, wameona fursa kutengeneza matukio kama hilo la gawio ili waandike dodoso la posho.

Mfumo wa utendaji wa mashirika haya hauna tija kwa taifa.
 
mimi natumia TTCL wapo vziri hasa vifirushi

Utakuwa ni mzee lazima. Ni nadra kumkuta mtu aliye below 40 anatumia Line ya TTCL. Voucher zenyewe zinapatikana sehemu chache kama dawa za kulevya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom