Fikra za Kisasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fikra za Kisasa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mahmood, Feb 3, 2011.

 1. Mahmood

  Mahmood JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2011
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 7,851
  Likes Received: 1,336
  Trophy Points: 280
  Leo, wapo wanazuoni wengi wa kisasa katika ukristo wanaochukulia kuwa Yesu Kristo hakuwa Mungu. Katika mwaka 1977, kikundi cha wanazuoni saba wa biblia, wakiwemo wanateolojia mashuhuri wa Kianglikani na wanazuoni wengine wa Agano Jpya walichapisha kitabu The Myth of God Incarnate (Uwongo wa Mungu kuwa Mtu), ambacho kilileta vurumai kubwa katika Sinodi[1] ya Kijumla ya Kanisa la Uingereza. Katika dibaji yao, mhariri John Hick, aliandika yafuatayo: “Waandishi wa kitabu hiki wamekinai kuwa ukuuzi mkuu na muhimu wa teolojia unahitajika katika sehemu hii ya mwisho wa karne ya ishirini. Mahitaji yameibuka kutokana na kuongezeka kwa elimu ya asili za Kikristo, na inajumlisha utambuzi kuwa Yesu ni (kama alivyoelezwa katika Matendo 2: 22) ‘mtu aliyethibitishwa na Mwenyezi Mungu’ kwa jukumu maalumu ndani ya lengo la Mungu. Hakika ni kuwa ile dhana iliyokuja baadaye yeye ni Mungu mwanaadamu katika mwili, Mtu wa Pili katika Utatu Mtakatifu aliyeishi maisha ya kibinadamu, ni ya kubuniwa au njia ya kimashairi ya kueleza umuhimu wake kwetu”[2].

  Yapo makubaliano mapana miongoni mwa wanazuoni wa agano Jipya kuwa Yesu wa kihistoria hakudai uungu ambayo ni fikra ya Kikristo ya baadaye ilimfanya; hakujifahamu mwenyewe kuwa ni Mungu, Mungu Mwana, mwanaadamu (katika mwili)[3].

  Marehemu Askofu Mkuu Michael Ramsey, ambaye alikuwa mwanachuoni wa Agano Jipya, aliandika: “Yesu hakudai uungu kwake mwenyewe”[4]. Mwanachuoni wa zama zake wa Agano Jipya C. F. D. Moule, alisema: “Kwa hali yoyote ukristo wa ‘juu’ ambao ulitegemea usahihi wa madai ya Yesu kuhusu yeye mwenyewe, hasa katika Injili ya Nne, kwa hakika itakuwa ni mashaka na hatari”[5].

  Katika utafiti mkuu kuhusu asili ya itikadi za Mungu kuwa mwili, James Dunn, aliyeshikilia imani halisi ya Kikristo, alihitimisha kuwa, “Hakuna dalili halisi na ya kweli katika hadithi kabisa za Yesu za mwanzo ambazo kwa usawa na uadilifu zinaweza kuitwa utambuzi wa uungu”[6]. Tena, Brian Hebblethwaite, mfuasi thabiti wa Ukristo wa Nicene-Kalsedoni wa kiada, anakiri kuwa, “Haiwezekani tena kuutetea uungu wa Yesu kwa kutoa kumbukumbu za madai ya Yesu”[7]. Dunn na Hebblethwaite, na wanazuoni wengine kama wao ambao bado wanaamini uungu wa Yesu, badala yake wanatao hoja kuwa Yesu hakujua kwamba alikuwa Mungu katika umbile la binaadamu. Hili lilijulikana tu baada ya ufufuo wake.

  Aliye mashuhuri zaidi miongoni mwa makasisi wa Kanisa la Uingereza, aliyeshuku uungu wa Yesu, ni Padri asiyeogopa kusema ukweli Profesa David Jenkins, Askofu wa Durham, Uingereza, ambaye hadharani alisema kuwa Yesu hakuwa Mungu[8].

  Makala yafutayo, yalitokea katikaThe Daily News miaka kadhaa iliyopita[9], yaonyesha wazi kabisa kiwango cha shaka miongoni mwa makasisi kuhusu uungu wa Yesu.

  Uchunguzi wa Kushtua wa Maaskofu wa Kianglikani

  LONDON: Zaidi ya Maaskofu nusu wa Kianglikani wa Uingereza wanasema kuwa Wakristo hawalazimiki kuamini kuwa Yesu Kristo ni Mungu, kulingana na uchunguzi uliochapishwa.

  Kupiga kura kwa Maaskofu 31 kati ya 39 wa Uingereza inaonyesha kuwa wengi wao wanafikiria kwamba miujiza ya Yesu, kuzaliwa kwake na bikira na kufufuka kwake hayangalitokea kama vile yalivyoelezwa katika Biblia.

  Ni Maaskofu 11 pekee ndio waliosisitiza kuwa Wakristo ni lazima wamchukulie Kristo kama Mungu na mwanaadamu, ilhali 19 walisema inatosha kumchukulia Yesu kama “mwakilishi (au ajenti) mkuu wa Mwenyezi Mungu”. Mmoja kati yao alikataa kutoa rai yake.

  Kura hiyo ilifanywa na London Weekend Television (Runinga ya London ya Wikiendi[10]) katika kipindi cha dini cha kila wiki, kinachoitwa Credo.

  “DAILY NEWS” 25/6/84

   
 2. Mahmood

  Mahmood JF-Expert Member

  #2
  Feb 4, 2011
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 7,851
  Likes Received: 1,336
  Trophy Points: 280

  Thank you very much Bro. for this very useful thread.

  Mungu akubariki, Amin.
   
 3. Mahmood

  Mahmood JF-Expert Member

  #3
  Feb 5, 2011
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 7,851
  Likes Received: 1,336
  Trophy Points: 280
  Asante
   
 4. M

  Mandago JF-Expert Member

  #4
  Feb 5, 2011
  Joined: Feb 8, 2008
  Messages: 238
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Baada ya uchunguzi huo Maaskofu hao wa Kianglikani wa Uingereza wanasema kuwa Wakristo hawalazimiki kuamini kuwa Yesu Kristo ni Mungu, kulingana na uchunguzi uliochapishwa.

  Maaskofu 19 wa Kianglikani walisema inatosha kumchukulia Yesu kama “mwakilishi (au ajenti) mkuu wa Mwenyezi Mungu”. Mmoja kati yao alikataa kutoa rai yake.
   
Loading...