Fikra pevu kwa kijana wa mwaka 2017. Mtazamo wako, mafanikio yako

Babafetty

Senior Member
Nov 11, 2013
102
250
Mwaka 2016 unaisha tukiwa na mtazamo mpya wa Tanzania tokana na aina mpya ya utawala. Kuna waliofanikiwa na cha kujivunia kwa mwaka 2016 na kuna waliopoteza matumaini na kisha kulaumu waliowazunguka kama ndio chanzo kwa kufeli kwao.

Kulalamika ni chanzo cha kuifunga akili yako juu ya mafanikio. Umeumbwa kupambana, ukilaumu umri hausubiri. Relax, take it easy, don't copy and paste, don imitate plz, be creative tokana na mazingira yako, utafanikiwa.

Usikubali mwaka 2017 ukaisha huku ukilalamika huku wenzako wakifanikiwa, kufanikiwa is just a spirit and not imagination. Jiamini na focus unataka kufanya nini mwakani. Have a vision and how you will accomplish your target.

Orodhesha malengo yako katika karatasi, yasiwe mengi mpaka yakakuchanganya. yapangie muda ya kuyatekeleza na kisha angalia ulifeli wapi. Lazma upambane ili uwe wewe.

Nakutakia kheri ya mwaka mpya, wenye mabadiliko chanya. Thubutu, jiamini, weka malengo chanya.

Karibu 2017.
 

La Nuit

JF-Expert Member
Dec 16, 2015
472
500
Nisiwe mchoyo wa shukrani. Maana naamini JF na wana Jamii forum, wamenifanya nipige hatua kubwa kama ya Goliath ndani ya mwaka huh 2016.
 

Maboso

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
5,009
2,000
Kwa uwezo wake Mungu, na kwa kipawa alichonipa, na kwa nguvu alizonipendelea, na kwa akili alizonijalia, pamoja na changamoto nyingine za kusomesha wadogo zangu, na kusaidia wazazi wangu ambao mimindiye nguzo yao kuu, mwaka 2017 kufikia Desemba naamini nitakuwa nimemaliza ujenzi wa nyumba ya kisasa yenye vyumba vinne, jiko, store, sebule, dinning, chumba cha mazoezi, cumba cha kujisomea na fence. Panapo majaaliwa ya Mwenyezi muguu niweze kuwasaidia wazazi wangu kupata hata ka Raum ka kutembelea. Malengo yangu ni hayo, ila Mungu ndiye msimamizi wa yote hivyo nitazidi kumuomba anisimamie na kunibariki.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom