Fikiria we ndo mtangazaji kati ya mechi ya mkoa Mbeya na Kagera | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fikiria we ndo mtangazaji kati ya mechi ya mkoa Mbeya na Kagera

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Viol, Jul 4, 2012.

 1. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #1
  Jul 4, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  Fikiria wewe ni mtangazaji wa mpira.Mechi inayochezwa ni kati ya timu ya mkoa wa Mbeya na timu ya mkoa wa Kagera....hivi ndivyo utakavyoutangaza mpira.
  ...Anakwenda pale Andendenisye Mwakisomola...anapiga kwake Nsajigwa Malafyale...naye kwake Asangalwisye Mwasabwite....anapiga pasi kwake Anongisye Mwakatebela...anatokea pale Salvatory Rugemalira ananyang'anya mpira...anatoa pasi kwa Bagambilaine Ntuyabaliwe....anacheza vizuri kabisa kwake Kokushobura Rugaimukamu...naye anampa pale Rwekaza Rweyemamu...anacheza vizuri...asalalee namna gani pale ananyang'anywa na Anyosisye Mwakifwamba...anagonga mbili tatu pale anapiga pasi ndeeefu kabisa inakuwa njiwa.... Mpira ni wa kurushwa sasa kuelekea lango la timu ya mkoa wa Mbeya...anakwenda kurusha nani pale...jezi nambari saba pale...haya sasa Rweyongeza Rutashubanyuma anarusha mpira kwake Lutatinisibwa Mutahyabarwa...ancheza daglizi pale...kwake nani sasa...kwake Nyamuhanga Lutabasibwa...anatokea pale Alinanuswe Mwakatapanya anachukua mpira...anatokea Kamugoza Rwegoshora anapigwa tobo pale na Mwakatapanya...anacheza vizuri pale kwake Andendekisye Mwamasangula...anaruka kichwa..hatari pale...gooooooooooooo......bao safi kabisa lile....golikipaChristosom Rwehumbiza alikwenda kushoto....Andendekisye Mwamasangula akapiga kichwa maridadi kabisa kulia...beki wa kati Mutakyawa Mukyanuzi akabaki kushangaa... Mbeya moja na Kagera hawajapata kitu......

  Mpira ukiisha lazima unywe dawa ya kutuliza maumivu ya koo.
   
 2. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #2
  Jul 4, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,156
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  nimeipenda hii mechi, nimejaribu kutangaza hapa kdogo tu mara koo limebuma, ngoja kwanza nipate asali kidogo
   
 3. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #3
  Jul 4, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  unatakiwa utangaze ukiwa na soft drink pembeni
   
 4. s

  sapaka Member

  #4
  Jul 4, 2012
  Joined: Jun 23, 2012
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii mechi nuksi kweli.kama zote zngekuwa hv mi naacha kazi.
   
 5. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #5
  Jul 4, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,833
  Trophy Points: 280
  Haaaaaaaaaaaaa
   
 6. d

  daby mouser JF-Expert Member

  #6
  Jul 4, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 207
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  hahahahahaha unaweza ukatema ulimi bila kupenda
   
 7. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #7
  Jul 4, 2012
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,101
  Likes Received: 1,425
  Trophy Points: 280
  Duh, nilikuwa natangaza kimya kimya lakini koo linaniuma...
   
 8. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #8
  Jul 4, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,127
  Trophy Points: 280
  Mechi tamu sana hiyo, yaani hata kama gemu haitanoga, ila hayo majina yatanogesha gemu.
  Kila neno lisilo maana watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu yake katika siku ya hukumu.
   
 9. B

  Bosco massawe Member

  #9
  Jul 5, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani! jamani MUNGU hana utani,hana mazoea, wala hana mzaha. Tuwe tunafikiri kabla ya kuonge. Mathayo 12-36
   
 10. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #10
  Jul 5, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  hahaaaaaaaaaaa.............
   
 11. God knows

  God knows JF-Expert Member

  #11
  Jul 6, 2012
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 266
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Kazi ipo!
   
 12. G_crisis

  G_crisis JF-Expert Member

  #12
  Jul 6, 2012
  Joined: Jun 19, 2011
  Messages: 715
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Hahahahahahah Mbona hao kagera wamezi 11 uwanjani
   
 13. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #13
  Jul 6, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,148
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  Kazi ndogo kwa Enock bwigane au ezekeli malongo
   
 14. K

  KIDOSHO Member

  #14
  Jul 9, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  wakikushinda unafupisha majina tu..Ruta, muta, ande, ndio mpango mzima
   
 15. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #15
  Jul 9, 2012
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,577
  Likes Received: 846
  Trophy Points: 280
  ..ulimboka alikuwa reserve au?
   
 16. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #16
  Jul 9, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  ukitoka hapo umeshachoka

  we cheka tu mkuu
   
 17. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #17
  Jul 9, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  tena kubwa sana

  kwanza hayo majina utejuaje huyu wa kagera na huyu wa mbeya?
   
 18. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #18
  Jul 9, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  dah umenikumbusha mbali hivi Ezekiel Malongo kapotelea wapi

  utakuwa umeuza mechi bhana
   
 19. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #19
  Jul 9, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  huyu ni majeruhi
   
 20. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #20
  Jul 9, 2012
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,577
  Likes Received: 846
  Trophy Points: 280
  Kumbe mechi ya juzi tu wiki haina.
   
Loading...