Fikiria Sumaye angekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Kama kushindwa uenyekiti wa Kanda tu kapanic hivi hadi kaitisha press conference, kama angefanikiwa kuwa Mwenyekiti wa chama na kupata usumbufu kama anaopata Mbowe si kuna siku angerusha ngumi kabisa.

Ingekuwaje kwa mfano bahati mbaya kawa mkiti na siku hiyo hiyo anaitwa central police kwa tuhuma za uchochezi ambao yeye hakuhusika bali wanachama wake, si mkiti angezimia kabisa.

Kwa bahati mbaya angekuwa mkiti kesho yake anasikia spika kawafukuza wabunge wake 50, na siku hiyo hiyo anasikia madiwani wake 400 nchi nzima wamefukuzwa uanachama na kupoteza nafasi zao, huyu hangechanganyikiwa? Kwa mfano Mkiti Sumaye akae rumande hata mwezi mmoja tu kwa tuhuma za uchochezi wa kusingiziwa, nafikiri siku anaachiwa angeomba aletewe kabisa shati lake la kijani kwenye mlango wa gereza ili aunge juhudi.

Najaribu kuwaza tu....unajua uongozi unahitaji uvumilivu, kwangu Sumaye ameprove failure.

"Nilichukuwa fomu ili kusaidia kukisafisha Chama juu ya tuhuma kuwa nafasi ya Mwenyekiti haiguswi" Tafsiri ya sentensi hii inaonyesha hakuwa serious kuongoza chama bali kuondoa tuhuma tu.

Hongera inteligensia ya Chadema kwa kuliona hilo mapema, bila hivyo chama kizima kingeuzwa kwa bei rahisi sana. Chadema ilikuwa inakwenda kuwa kama CUF na NCCR au TLP ya Mrema.

Sumaye was too soft to handle Main Opposition Party like CHADEMA.
 
Najaribu kuwaza tu....unajua uongozi unahitaji uvumilivu, kwangu Sumaye ameprove failure.

Hongera inteligensia ya Chadema kwa kuliona hilo mapema, bila hivyo chama kizima kingeuzwa kwa bei rahisi sana.

Sumaye was too soft to handle Main Opposition Party like CHADEMA.
 
chadema nimewaelewa sana kwa hili... wavivu wa kufikiri wanaponda but hawajui gharama za kukijenga chama baada ya agent kama Sumaye kukibomoa....................CCM amkeni amkeni amkeni wenzenu CDM wameanza kuwashitukia..
Kwa sasa CCM inashughulika na ACT wazalendo hao Chadema ni zilipendwa!
 
Back
Top Bottom