Fikiri Kuwa Sayari Tunayoishi ( Dunia) Ni Jehanamu Ya Sayari Nyingine...!

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Ndugu zangu,

Kwamba kuna viumbe kwenye sayari nyingine wenye kukesha wakiomba kwenye nyumba zao za ibada, kuwa Mungu wao awaepushe na balaa la kuwaleta kwenye sayari dunia.

Dunia iliyo zaidi ya tambala bovu. Dunia iliyojaa wanadamu wenye roho za wivu, kinyongo, inda, husda na nyinginezo. Wanadamu wenye kutakiana mabaya badala ya mema.

Na mfano ni huyu aliyeomba sana kwa Mungu ashushiwe rehma. Siku moja akashukiwa na malaika. Akaambiwa, kuwa Mungu amepokea maombi yake. Kwamba anamtaka mwanadamu huyu achague jambo moja ili ashushiwe. Na akishachagua moja, basi, Mungu atampa jirani yake mara mbili ya kitu alichochagua.

Mwanadamu yule akamwambia malaika; " Basi, niache kwanza nitafakari".

Baada ya kutafakari kwa muda,mwanadamu yule akatamka; " Namwomba Mungu anipe chongo!"

Kwamba kwa vile alimwonea kinyongo jirani yake apate mara mbili ya atakachokipata, mwanadamu yule aliona ni heri Mungu amtoboe jicho lake moja, awe chongo, na jirani yake atobolewe mawili, awe kipofu!

Naam, fikiri kuwa sayari tunayoishi yaweza ni jehenamu ya sayari nyingine.

Kumbuka, nimesema fikiri, hivyo basi fikiri kwa bidii...yaweza kukusaidia kupata jibu la kwanini nchi yetu ni masikini, na watu wake pia.

Na hilo ni Neno La Leo.

Maggid Mjengwa
 
hivi mpaka leo tunahitaji kufikiri tena kwa bidii kufahamu kwanini nchi yetu na watu wake ni maskini,sidhani kama kuna mtanzania ambaye hajui kwanini yeye na nchi yake ni maskini.
 
Kinyume chake pia ni sahihi maggid.
Kuna maisha wanayoishi watu hapa duniani kiasi cha kuweza kua ni pepo kwa sayari ingine.

Kama kuna viumbe wanaish kwenye hizo sayari, basi wanaoomba Mungu mchana na usiku waishi kama kina "nanii" tulio nao leo hapa duniani.

Usishangae kusikia hapa Tanzania kuna mtu anaishi maisha ambayo ni pepo ya mtu alioko labda America au Ulaya.
 
Last edited by a moderator:
Sidhani dunia kama sayari ni jehanamu, ila mfumo wa walimwengu (cosmos) ndio jehanamu yenyewe haswa.
.
 
Kwakuwa ni Magid Mjengwa kapost, mnajadili tu! Je angekuwa mtu mwingine si mngesema hii post ipelekwe kwenye ile segment ya Jokes au religion! Hahahaaaa anyway fikirini kwa bidii!
 
na siku za mwisho watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe,wenye kupenda fedha,wenye kujisifu,wenye kiburi,watukanaji,wasiotii wazazi wao,wasio na shukrani,...wasiopenda wa kwao...wenye mfano wa utauwa(utakatifu)lakini wakizikana nguvu zake(Mungu)...wasiopenda mema...wapendao anasa kuliko Mungu...na mengineyo(2 timotheo sura ya 3).hebu tutafakari kwa bidii kila sifa iliyotajwa hapo juu,halafu tutafakari swali la Maggid!
 
hii post ni ya siasa,acheni vichwa vya nazi, mfano ni watu wanasikia gas imegunduliwa mtwara, wanakimbia ulaya kusaini mkataba feki, wanapewa say 234bn wanaficha uswisi, gesi ile inaishia kufaidisha nchi za ulaya, na yeye anasihi hapa kama peponi! huyu ni kama yule aliyemwomba Mungu awe chongo ilijirani yake awe kipofu...someni between the line, ndo maana ya great thinkers
 
hii post ni ya siasa,acheni vichwa vya nazi, mfano ni watu wanasikia gas imegunduliwa mtwara, wanakimbia ulaya kusaini mkataba feki, wanapewa say 234bn wanaficha uswisi, gesi ile inaishia kufaidisha nchi za ulaya, na yeye anasihi hapa kama peponi! huyu ni kama yule aliyemwomba Mungu awe chongo ilijirani yake awe kipofu...someni between the line, ndo maana ya great thinkers
Ni kweli mkuu. Kuna kiongozi mmoja wa masuala ya gas nilimsikia akisema gas ata ikichimbwa,manufaa yake mtanaania atayaona baada ya miaka sita!nilimshangaa..au ndio hao ambao wammeshapewa pesa wameweka uswiss. Gas ikitoka tu i tayari kwa matumizi,miaka sita ya kazi gani...?!
 
Kwakuwa ni Magid Mjengwa kapost, mnajadili tu! Je angekuwa mtu mwingine si mngesema hii post ipelekwe kwenye ile segment ya Jokes au religion! Hahahaaaa anyway fikirini kwa bidii!

Umeona eeh!!
Na mods wako so biased,kwani ingekuwa mwingine kapost hapa,ingesha kuwa moved kwenda jukwaa lingine,au kufutwa kabisa.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom