Figisu Figisu za wasimamizi wa uchaguzi mdogo wa marudio wa Madiwani kata ya Boma Mbuzi Jimbo la Moshi Mjini

So far away

Member
Jan 7, 2017
58
121
Tarehe 26 mwezi huu ndo uchaguzi wa marudio kwa madiwani na wabunge unafanyika nchi nzima. Ila hali inaonekana si shwali jinsi ya kuwapata wasimamizi wakuu; wasimizi wadogo na Makarani pia ambao wataendesha zoezi zima la uchaguzi katika kata ya Boma Mbuzi jimbo la Moshi mjini.

Nikweli wametangaza nafasi za usimamizi ili watu waombe nafasi hizo. Kwa sasa ni kama wiki imepita. Wanaoonesha nia ya kuomba nafasi hiyo inawabidi waandike barua na waambatanishe na CV na waipitisge kwa mwajiri wao.

Kumbe hayo yote ni kiini macho Aisee!! Hapa kuna figisu figisu za makada wa CCM ambao wameshapanga nafasi hizo (80) za wasimamizi. Na kwa sasa kuna taarifa kuwa kila kitu kimeshakamilika. wasimamizi tayali wanajijua na vituo vya kusimamia wanavijua. Kila mmoja anajua kuwa ni msimamizi mkuu
; msaidizi au karani ilihali hata dead line (tarehe 11) ya kutuma barua haijafika.

WanaCCM wamejipanga vya kutosha kurejesha hiyo kata. Wasimamizi wameshasukwa kwa kila mbinu ili warete ushindi kwa mgombea wa CCM. Hiyo inawezekana tena kwa urahisi kwani hata Msimamizi wa uchaguzi ikada mwaminifu tu wa CCM.

My take:
Kama hali ndo hiyo; je CHADEMA hawaoni kuwa wataangikia pua kwenye uchaguzi huu nchi nzima!
CHADEMA na nyinyi mmelala mno sana. Hatuoni harakati za ushindi kwenye uchaguzi huu mdogo. Mtaaibika saa aisee!!!
 
Sawa mwalimu. Wamekusikia.
Ila kusimamia uchaguzi na kulalamika ni kawaida kwa walimu, mpaka mtakapojitambua!
Unaona CHADEMA wamelala wakati wewe umekosa nafasi?
 
Tarehe 26 mwezi huu ndo uchaguzi wa marudio kwa madiwani na wabunge unafanyika nchi nzima. Ila hali inaonekana si shwali jinsi ya kuwapata wasimamizi wakuu; wasimizi wadogo na Makarani pia ambao wataendesha zoezi zima la uchaguzi katika kata ya Boma Mbuzi jimbo la Moshi mjini.

Nikweli wametangaza nafasi za usimamizi ili watu waombe nafasi hizo. Kwa sasa ni kama wiki imepita. Wanaoonesha nia ya kuomba nafasi hiyo inawabidi waandike barua na waambatanishe na CV na waipitisge kwa mwajiri wao.

Kumbe hayo yote ni kiini macho Aisee!! Hapa kuna figisu figisu za makada wa CCM ambao wameshapanga nafasi hizo (80) za wasimamizi. Na kwa sasa kuna taarifa kuwa kila kitu kimeshakamilika. wasimamizi tayali wanajijua na vituo vya kusimamia wanavijua. Kila mmoja anajua kuwa ni msimamizi mkuu
; msaidizi au karani ilihali hata dead line (tarehe 11) ya kutuma barua haijafika.

WanaCCM wamejipanga vya kutosha kurejesha hiyo kata. Wasimamizi wameshasukwa kwa kila mbinu ili warete ushindi kwa mgombea wa CCM. Hiyo inawezekana tena kwa urahisi kwani hata Msimamizi wa uchaguzi ikada mwaminifu tu wa CCM.

My take:
Kama hali ndo hiyo; je CHADEMA hawaoni kuwa wataangikia pua kwenye uchaguzi huu nchi nzima!
CHADEMA na nyinyi mmelala mno sana. Hatuoni harakati za ushindi kwenye uchaguzi huu mdogo. Mtaaibika saa aisee!!!
Mbona dakika tisini hazijaisha unaweweseka?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom