Figisu Figisu CECAFA: Zanzibar Heroes wahofiwa kutumia madawa ya kusisimua misuli!

Wonderful

JF-Expert Member
Apr 8, 2015
7,348
5,977
C__Data_Users_DefApps_AppData_INTERNETEXPLORER_Temp_Saved Images_BAO-LA-3-SHEREHE-640x427.jpg

Kiwango kinachooneshwa na Zanzibar Heroes kwenye michuano ya kombe la Chalenji kimeendelea kushtuwa wengi, kubwa kuliko ni leo Dec. 9, 2017 baada ya mchezo dhidi ya wenyeji Kenya, baadhi ya wachezaji wa Zanzibar Heroes walitakiwa kupimwa wakishukiwa kutumia dawa za kusisimua misuli ambazo zimezuliwa kwenye michezo.

Mchezo huo ulimalizika kwa suluhu (Kenya 0-0 Zanzibar Heroes) lakini maafisa wa CECAFA waliwataka baadhi ya wachezaji wachukuliwe vipimo kwa ajili ya kufaniwa uchunguzi kama wanajihusisha na matumizi ya dawa zilizozuiliwa michezoni.

Baadae maafisa wa CECAFA wakiwa wameongozana na madaktari walifika hotel waliyofikia wachezaji wa Heroes (Garden Hotel) kisha kuchukua vipimo kwa wachezaji wanne.

Wachezaji waliochukuliwa vipimo ni Fesal Salum, IbrahimHamad, Suleiman Kassim ‘Selembe’, na Mohamed Issa ‘Banka’. Watatu kati ya wachezaji wameshinda tuzo ya man of the match katika mechi tatu tofauti (Mohamed Issa-Zanzibar vs Rwanda, Ibrahim Hamad-Tanzania vs Zanziba na Fesal Salum-Kenya vs Zanzibar)
 
Nyie watanganyika acheni unaaa mjue zenji tuko vizuri badala ya kutusifia kama sehemu ya jamhuri ya tz Na nyie mnaleta unafiki, mpira maandalizi sio porojo kwani hamuoni saivi wazanzibar walivyoiteka ligi yenu ya VPL Na mnabahati FIFA hawajatupa membership tungewApigeni kilasiku
 
Nyie watanganyika acheni unaaa mjue zenji tuko vizuri badala ya kutusifia kama sehemu ya jamhuri ya tz Na nyie mnaleta unafiki, mpira maandalizi sio porojo kwani hamuoni saivi wazanzibar walivyoiteka ligi yenu ya VPL Na mnabahati FIFA hawajatupa membership tungewApigeni kilasiku
Jamani kwani cc watanganyika ndio tuliowapima mkojo? Waulizeni CECAFA
 
wanataka kuiminya Zanzibar kila kona, huku jinamizi la Tanganyika na kule Cecafa wameanza choyo
 
Breaking news
Baada ya hapo jana cecafa kuitilia mashaka Zanzibar heroes kama wana tumia madawa ya kuongeza nguvu na kuwafanyia vipimo na waka gundua ni kweli wanatumia
Cecafa wamesema zanziba hero wana tumia dawa aina tatu nazo ni---
UROJO WA FORODHAN
BOFLO NA
UBUYU WA KIPONDA.....ONE LOVE ZANZIBAR HEROES
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom