FIFA kujenga uwanja wa michezo kwa kila nchi mwanachama barani Afrika. Je unapendekeza mkoa/bei gani?

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
42,856
49,540
Katika kukuza michezo barani Afrika,Rais wa FIFA ameanzisha kampeni ya kuhakikisha kwamba kila nchi mwanachama wa wake wa bara la Afrika inajengewa uwanja mpya wa kisasa ambao utakuwa mali ya shirikisho

Kwa mujibu wa Rais wa TFF yeye amependekeza uwanja kujengwa mkoani yaani nje ya Dar na amewataka wadau wapendekeze sehemu itakayofaa

Mimi binafsi napendekeza moja ya mikoa au miji ifuatayo

1.Mbeya,
Napendekeza Mbeya kwa sababu zifuatazo,kwanza ni moja ya mikoa ya wapenda soka sana na ina wanasoka wengi sana lakini pia ina timu 2 kila mwaka ligi kuu na pili ina timu 3 ligi daraja la kwanza

Pili ni mji mzuri kwa ajili ya kufanya figisu washindani wa kimataifa kwa kuwa hali yake ya hewa huwa inazingua sasa mkipata timu inatokea kanda ya joto mnapeleka huko lakini kama tunapata timu ya kwenda kanda ya baridi ile ni sehemu nzuri ya kuweka kambi

Na tatu ni kwamba mji uko strategic kwa kanda ya nyanda za juu kusini na jirani na nchi za sadc ko ni rahisi uwanja kukodiwa na nchi jirani na pia kufikika na mashabiki wa mikoa na nchi jirani

2.Morogoro
Moro ni moja ya mikoa ya kimichezo Tanzania kwa hiyo kupata mashabiki ni uhakika kwa kuwa mji uko jirani na Dar na Dodoma. Ujirani wake na Dar unatoa fursa nzuri ya kuandaa mashindano ya kimataifa kama Chan nk ukishirikiana na viwanja vya Dar, Zanzibar na dodoma

3.Mwanza
Mji wa Mwanza ni moja ya mikoa yenye mashabiki wa kutosha wa soka na kuna timu zaidi ya moja ligi kuu na daraja la kwanza kila mwaka. Pili mji uko strategic kwa kuweza kufikiwa kirahisi na mikoa ya kanda ya ziwa na nchi jirani
Na tatu ni uwepo wa miundombinu wezeshi na kuweza kuchagiza utalii kwenye kanda hiyo
Wewe unapendekeza uwanja mpya ujengwe mkoa/mji gani? Karibuni kwa maoni
 
Kama haujengwi dar wanapoteza hela zao.
Dar ndio kuna mashabiki wa kila kitu
 
Kwa Mbeya nitaongezea sifa moja kuu ya kiufundi... Kuna njia panda nzuri ya kuvunjia Nazi.... Nazi ikivunjiwa Njia Panda ya Uyole team pinzani huwa hazitoki...
Ha!Ha!Ha!Siku Hizi Usafiri Wa Basi Kuja Mbeya Ndo Unakufa Hvoo!Habari Ya Mujini Ni Bombadieee!Tunatua Songwe Then Mbalizi!Kama Hiyo Nazi Vunjieni City Centre Pale Meta Njia Panda Stend Kuu!
 
Back
Top Bottom