FIFA kuja na mabadiliko kadhaa kwenye soka ikiwemo kupunguza muda mpaka dakika 60

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,251
FIFA yapendekeza dakika 60 za mechi

Shirikisho la soka duniani (FIFA) lina mpango wa kupunguza muda wa mchezo wa mpira wa miguu kuwa dakika 30 kila kipindi. Bodi ya kimataifa ya soka duniani inatarajia kujadili pendekezo hilo linalolenga kuondoa upotezaji muda kwa makusudi, tabia inayofanywa wachezaji uwanjani.

Pendekezo lingine ni wachezaji kutoruhusiwa kupiga mpira mara ya pili baada ya kipa kuupangua wakati wa penalti na iwapo penalti haikupigwa inavyostahili, mchezo utasitishwa na mpira wa adhabu kutolewa.

Mapendekezo mengine ni kama kuweka saa katika uwanja ambayo italingana na ile ya refa mbali pamoja na sheria mpya itakayoruhusu mchezaji kujipigia mpira au hata kutamba na mpira wakati anapopiga mpira wa adhabu.

RFA
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Dakika 90 za sasa zinapotezwa na kuchezwa labda 80 tu! Wakipunguza muda wa mchezo mpaka dakika 60 sijui zitachezwa dakika ngapi? Wangetafuta namna ya kuwabana wachezaji wenye tabia ya kupoteza muda wakati wa mchezo! Kama vipi wakipunguza muda wa mchezo wapunguze pia na viingilio.
 
Hawa jamaa wanataka kutupunguzia ladha ya soka. Sasa dk 60 kweli nikalipie hela yangu ya kiingilio pale Taifa ? Sasa nitakuwa nimepata ladha gani kwa hizo dk 60?

Bora wangeongeza dk 120 ili muda uwe wa kutosha jamani.
 
mi nadhani ingekuwa busara akaongeza kila kipindi ndio iwe dakia 60,yani kipindi cha kwanza dakika 60 kipindi cha pili dakika 60,extra time iwe dakika 40 penalti ziwe 10 kwa 10,kusiwepo na offsaid na kadi nyekundu iondolewe iwe kadi ya njano,na nyeusi,yani mchezaji akifanya kosa anapwa kadi ya njano,akirudia anapigwa tena kadi ya njano,akirudia mara ya tatu anapigwa tena kadi ya njano,mara nne anapigwa kadi nyeusi ya kumsimamaisha kucheza mpira kwa muda wa miezi mitatu
 
Hawa jamaa wanataka kutupunguzia ladha ya soka. Sasa dk 60 kweli nikalipie hela yangu ya kiingilio pale Taifa ? Sasa nitakuwa nimepata ladha gani kwa hizo dk 60?

Bora wangeongeza dk 120 ili muda uwe wa kutosha jamani.

90=huendii
60=utaendaje hioo taifa
 
Kuna kirusi kwenye kambi inayofanya mapendekezo na maamuzi, nahisi watu wamehongwa ili waharibu radha ya mpira na washabiki tuje kwenye Basket Ball, American Football, Baseball, na michezo mingine.

Maana soccer imedominate kwa muda mrefu na haionekani kuanguka.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom