Fiesta dar shakani

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,503
2,980
"Chawa" maarufu wa Mkoa wa Dar , Bwana "Lemtumboz" alitoa ujumbe kupitia Instagram juu ya onyesho OMARION lililofanyika Elements na kumalizwa kiubabe kabla ya muda uliopangwa. Unadhani hili limekuja bahati mbaya. Post hiyo imeweka reference juu ya onyesho la [HASHTAG]#CastleLite[/HASHTAG] lililomalizika saa sita kamili usiku. Wandugu wa Clouds Mjiandae na hilo li Fiesta lenu

Lemtumboz ambaye hana cheo chochote Serikalini, ameweka tumbo lake mbele na kufungua kitovu chake kiropoke kama kawaida akidai kwamba Sheria inataka matamasha yaishe saa 6 usiku. Waswahili wanasema message sent.

Kwa wenye uelewa wameelewa kwamba huu ni ujumbe kwa Fiesta ambayo inatarajiwa kufanyika Dar tarehe 18 Novemba. Miaka yote Fiesta inaisha Asubuhi ( Sheria zilikuwepo) Ni tangu miaka 16 iliyopita ambapo Lemtumboz na Bosi wake Bashite hawakuwa na hili wala lile, Fiesta iliisha asubuhi. Hata mwakajana Bossi wa Lemtumboz alipokuwa karibu na waandaji wa Fiesta tamasha lililisha Asubuhi.

Tunaelewa kuwa Birthday ya Diamond iliisha usiku wa manane na Mkuu wa Mkoa kama Mlezi wa WCB alihudhuria na mara nyingi tu anafika Elements kula Bata lakini hakuwahi kuwaambia wafunge saa sita. Inasemekana Bwana Platnumz aligoma kumpost jamaa kwenye Insta yake na hapo kisingizo kikapatikana

Clouds wenyewe wanafukuza mwizi Kimyakimya na juzi Prezidaa kawapigia simu kwa mara nyingine tena Live kwenye Fursa yao huko Tanga. Ngoja tuone Prezidaa atasimama na nani, RG au Bashi
 
Back
Top Bottom