Fidia kwa wanaozunguka Buzwagi kupitiwa upya

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,794
287,947
Fidia kwa wanaozunguka Buzwagi kupitiwa upya
Halima Mlacha, Dodoma
Daily News; Friday,June 13, 2008 @00:05

WIZARA ya Nishati na Madini inatarajia kupitia upya kwa kushirikiana na wadau, masuala ya fidia kwa wananchi wanaoishi kuzunguka eneo la mgodi wa dhahabu wa Buzwagi kubaini kama kuna ukiukwaji.

Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Zulekha Haji (CCM) ambaye alihoji nini kiini cha tatizo la migogoro katika mgodi huo, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima alisema kupitia upya fidia hizo kunatokana na Serikali kuona madai ya wananchi hayo yana msingi.

Mradi wa mgodi huo umekuwa na mgogoro kati ya wananchi na wawekezaji ambao chanzo chake ni tofauti za maoni na viwango vya fidia na utaratibu uliotumika kuwahamishia wananchi hao kwenye makazi mbadala, alisema.

Alisema mchakato wa tathmini ya kuwafidia na kuwahamisha wananchi hao ulianza mwaka 2005 na baada ya hatua za tathmini kukamilika wananchi wa vijiji vya Mwime, Mwendakulima na Chapulwa walilipwa fidia pamoja na kujengewa nyumba za makazi mbadala 205 kama mpango wa kufidia makazi yao ya zamani.
Malima alisema katika mchakato huo, wachimbaji wadogo waliokuwa wanachimba kwenye leseni ndogo ya kijiji cha Mwime, eneo la Zanzibar na Majimaji wamefidiwa mashimo 52 kila moja lilifidiwa Sh 200,000.

"Pamoja na malipo hayo, migogoro iliendelea na Aprili mwaka huu yalitokea matukio ambayo yaliashiria kuhatarisha amani katika eleo hilo," alisema.

Alisema Waziri Mkuu alimwagiza Waziri wa Nishati na Madini kushughulikia mgogoro huo ili kuutatua na Apili 25, mwaka huu, Naibu Kamishna wa Madini alitumwa kufanya uchunguzi wa awali ili kumwezesha Waziri kushughulikia mgogoro huo na baada ya kumpatia waziri taarifa yake Naibu Waziri pamoja na Kamishna wa Madini walikwenda Buzwagi kutatua mgogoro huo.

Walikutana na wahusika wote wakiwamo wawakilishi wa wananchi wa vijiji vyote vitatu, Mbunge wa Kahama Daudi Lembeli, uongozi wa wilaya na uongozi wa mgodi ambao ni Barrick kujadili kwa kina kiini cha mgogoro, alisema.

Alisema baada kushauriana na wahusika wa pande zote, walikubaliana kupitia upya masuala ya fidia kwa wananchi hao na wamejipa hadi Septemba mosi, mwaka huu wawe wamepata majibu ya utaratibu mzima wa ulipwaji wa fidia kwa wananchi hao.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom