Fidel Castrol alifanya makosa makubwa sana kutumia rasili mali zake kusaidia Bara la Africa Aibu ili

undefine

JF-Expert Member
Nov 17, 2016
442
1,010
Hakika nimesikitika sana kwa namna nchi za Africa zilivyomtenga Fidel Castro.Fidel Castro alikuwa Freedom fighter ambaye alitumia rasili mali zake kuikomboa bara la Africa mikononi mwa madhalimu.Takwimu zinazoonyesha takriban wanajeshi 381,432
wa cuba walishiriki katika mapambano ya kusaidia nchi za Africa waweze kujitawala.Wanajeshi hawa walitumia jasho na damu zao kusaida nchi za Africa japo hawakuwa wazawa.

katika misafara iliyoenda Cuba kwaajili ya maombolezo nchi za Africa ni nchi 2 tu ambazo zimepeleka wajumbe.Rais wa Africa kusini na Rais wa Zimbabwe ni viongozi pekee wa bara la Africa waliohudhuria mazishi ya Fidel Castro

makamu wa rais wa china,Waziri wa India, wajumbe wa Iran,urusi na viongozi wote wa nchi za America kusini wamehudhuria mazishi ya Fidel Castro huku Jumuiya ya umoja wa ulaya ni nchi pekee tu ya Ugiriki ambayo imemtuma mwakilishi katika mazishi ambaye ni waziri mkuu.

1.Fidel Castro aliwatoa madaktari wake waende kutibu ugonjwa wa Ebola uliokuwa umeikumba nchi za Africa Magharibi.

2.Fidel alitoa scholarships za kwenda kusomea udaktari kwa nchi nyingi za Africa

3.Fidel alitumia Rasili mali watu ''wanajeshi'' kwenda kusaidia mapambano dhidi ya wakoloni,moja ya nchi iliyosaidiwa ni Angola lakini kwa kusikitika Angola hawajapeleka mjumbe katika mazishi ya Fidel zaidi ya veterani mmoja aliyeshiriki vita kujitolea kwenda kuhudhuria mazishi ya Fidel.Takwimu zinasema idadi ya wanajeshi 2000 wa cuba walifariki katika mapambano katika nchi ya Angola.

4.Fidel alijenga shule nyingi katika maeneo mbali mbali Africa mfano Tanzania shule za Ruvu,ifakara nk zilijengwa na Cuba.

5.Cuba imekuwa ikitoa mafunzo ya kijeshi na Intelligensia kwa nchi mbali mbali za Africa.

Ni aibu ni nchi 2 tu kutoka Africa ambazo zimetuma wawakilishi katika msiba wa Fidel, Robert Mugabe na Jacob zuma tu ndio wamehudhuria.

Na ni masikitiko makubwa nchi ya Angola haijatuma mwakilishi kwenda kuhudhuria msiba wa Fidel wakati zaidi ya wanajeshi 2000 wa cuba walikufa katika mapambano nchini Angola katika harakati ya kuikomboa Angola na wanafunzi 14,000 waipata kusomeshwa nchini cuba.

mozambique,Congo waliosaidiwa kijeshi na Fidel Castro kupigania ukombozi leo hii wamesusa kuhudhuria mazishi ya Fidel.

Cuba walikuja Africa kama madaktari,walimu,wanajeshi,wakufunzi ,watafiti lakini siyo kuja kwa lengo la ukoloni.

Hata msiba wa Ronald Reegan ma rais wa nchi 6 Africa walihudhuria wakati Ronald Reegan na serikali yake walikuwa wana sapoti apartheid kule Africa kusini na walimuorodhesha Mandela kama Gaidi na alikuwa kwenye watchlist ya magaidi.Huku Fidel freedom fighter aliyeenda kumsaidia Mandela tukimsusa

Hakika Fidel Castro hajatendewa haki na nchi za ki Africa,jumuiya ya ulaya na Amerika wamemtenga na sisi wa Africa tumemtenga pia.

R.I.P Fidel rasili mali na nguvu ulizotumia kusaidia Africa ungetumia kuliendeleza taifa lako
 
Hakika nimesikitika sana kwa namna nchi za Africa zilivyomtenga Fidel Castro.Fidel Castro alikuwa Freedom fighter ambaye alitumia rasili mali zake kuikomboa bara la Africa mikononi mwa madhalimu.Takwimu zinazoonyesha takriban wanajeshi 381,432
wa cuba walishiriki katika mapambano ya kusaidia nchi za Africa waweze kujitawala.Wanajeshi hawa walitumia jasho na damu zao kusaida nchi za Africa japo hawakuwa wazawa.

katika misafara iliyoenda Cuba kwaajili ya maombolezo nchi za Africa ni nchi 2 tu ambazo zimepeleka wajumbe.Rais wa Africa kusini na Rais wa Zimbabwe ni viongozi pekee wa bara la Africa waliohudhuria mazishi ya Fidel Castro

makamu wa rais wa china,Waziri wa India, wajumbe wa Iran,urusi na viongozi wote wa nchi za America kusini wamehudhuria mazishi ya Fidel Castro huku Jumuiya ya umoja wa ulaya ni nchi pekee tu ya Ugiriki ambayo imemtuma mwakilishi katika mazishi ambaye ni waziri mkuu.

1.Fidel Castro aliwatoa madaktari wake waende kutibu ugonjwa wa Ebola uliokuwa umeikumba nchi za Africa Magharibi.

2.Fidel alitoa scholarships za kwenda kusomea udaktari kwa nchi nyingi za Africa

3.Fidel alitumia Rasili mali watu ''wanajeshi'' kwenda kusaidia mapambano dhidi ya wakoloni,moja ya nchi iliyosaidiwa ni Angola lakini kwa kusikitika Angola hawajapeleka mjumbe katika mazishi ya Fidel zaidi ya veterani mmoja aliyeshiriki vita kujitolea kwenda kuhudhuria mazishi ya Fidel.Takwimu zinasema idadi ya wanajeshi 10,000 wa cuba walifariki katika mapambano katika nchi ya Angola.

4.Fidel alijenga shule nyingi katika maeneo mbali mbali Africa mfano Tanzania shule za Ruvu,ifakara nk zilijengwa na Cuba.

5.Cuba imekuwa ikitoa mafunzo ya kijeshi na Intelligensia kwa nchi mbali mbali za Africa.

Ni aibu ni nchi 2 tu kutoka Africa ambazo zimetuma wawakilishi katika msiba wa Fidel, Robert Mugabe na Jacob zuma tu ndio wamehudhuria.

Na ni masikitiko makubwa nchi ya Angola haijatuma mwakilishi kwenda kuhudhuria msiba wa Fidel wakati zaidi ya wanajeshi 2000 wa cuba walikufa katika mapambano nchini Angola katika harakati ya kuikomboa Angola na wanafunzi 14,000 waipata kusomeshwa nchini cuba.

Cuba walikuja Africa kama madaktari,walimu,wanajeshi,wakufunzi ,watafiti lakini siyo kuja kwa lengo la ukoloni.

Hakika Fidel Castro hajatendewa haki na nchi za ki Africa,jumuiya ya ulaya na Amerika wamemtenga na sisi wa Africa tumemtenga pia.

Hata msiba wa Ronald Reegan ma rais wa nchi 6 Africa walihudhuria

R.I.P Fidel rasili mali na nguvu ulizotumia kusaidia Africa ungetumia kuliendeleza taifa lako
Nadhani umekula makande mengi mchana ukavimbewa!
Nani kakuambie ni mbili zimetuma wawakilishi huko Cuba? Hivi unajua KAZI za mabalozi? Hivi unajua kazi za mawaziri wa mambo ya nchi?
Siyo kila tukio kwenye fulani ahudhurie rais .
 
ndio maana nikasema iran ,india wametuma mawaziri wa mambo ya nje na china makamu wa rais kaenda ,urusi japo wana balozi Cuba lakini wamepeleka wajumbe..kama kuna ya Africa ilituma waziri hakika ningeitaja hapa .

uwakilishi wa balozi tofauti kabisa na delegation ikitumwa ya wajumbe au waziri.
 
Angalia takwimu zako. Ni idadi gani sahihi ya wanajeshi wa Cuba waliofia kwenye mapambano nchini Angola, 2,000 au 10,000?
 
Africa ina aibisha sana, ni bara ambalo halijawahi kuchangia chochote kwenye maendeleo ya hii Dunia.

Ni bara mzigo, linasaidiwa na wengine karibia kila kitu,

Hata kama Africa isingekuwepo Dunia isingepungukiwa hata kidogo
 
Nakubaliana na wewe kwa 100% dunia isingepungukiwa kitu chochote kwa kukosekana bara ka africa. Na pengine dunia ingekuwa pahala fulani pazuri zaidi. Inasemekana asilimia kubwa ya viongozi wa ngazi mbalimbali za juu wa kiafrica ndo wanaongoza kupora na kuweka pesa ulaya na sasa asia na wengine hata ndugu zao hawajui. Je kuna wafrica wangapi wanateseka na kutegemea misaada ya watu wa marekani, watu wa ulaya na uchina?.....
Hata kama Africa isingekuwepo Dunia isingepungukiwa hata kidogo!
 
Wakati wengine wakijikita kwenye vumbuzi za kimaendeleo, waafrika wamejikita kwenye ndoa za mitaala, ufisadi, vita vya wenyewe kwa wenyewe, wizi, na kila aina ya ovu unaloweza kulifikiri.

Ubaya ni kwamba waafrika wakiambiwa mapungufu yao wanawaka kama moto wa petrol, hawataki kuambiwa ukweli.
 
28 Reactions
Reply
Back
Top Bottom