undefine
JF-Expert Member
- Nov 17, 2016
- 442
- 1,011
Hakika nimesikitika sana kwa namna nchi za Africa zilivyomtenga Fidel Castro.Fidel Castro alikuwa Freedom fighter ambaye alitumia rasili mali zake kuikomboa bara la Africa mikononi mwa madhalimu.Takwimu zinazoonyesha takriban wanajeshi 381,432
wa cuba walishiriki katika mapambano ya kusaidia nchi za Africa waweze kujitawala.Wanajeshi hawa walitumia jasho na damu zao kusaida nchi za Africa japo hawakuwa wazawa.
katika misafara iliyoenda Cuba kwaajili ya maombolezo nchi za Africa ni nchi 2 tu ambazo zimepeleka wajumbe.Rais wa Africa kusini na Rais wa Zimbabwe ni viongozi pekee wa bara la Africa waliohudhuria mazishi ya Fidel Castro
makamu wa rais wa china,Waziri wa India, wajumbe wa Iran,urusi na viongozi wote wa nchi za America kusini wamehudhuria mazishi ya Fidel Castro huku Jumuiya ya umoja wa ulaya ni nchi pekee tu ya Ugiriki ambayo imemtuma mwakilishi katika mazishi ambaye ni waziri mkuu.
1.Fidel Castro aliwatoa madaktari wake waende kutibu ugonjwa wa Ebola uliokuwa umeikumba nchi za Africa Magharibi.
2.Fidel alitoa scholarships za kwenda kusomea udaktari kwa nchi nyingi za Africa
3.Fidel alitumia Rasili mali watu ''wanajeshi'' kwenda kusaidia mapambano dhidi ya wakoloni,moja ya nchi iliyosaidiwa ni Angola lakini kwa kusikitika Angola hawajapeleka mjumbe katika mazishi ya Fidel zaidi ya veterani mmoja aliyeshiriki vita kujitolea kwenda kuhudhuria mazishi ya Fidel.Takwimu zinasema idadi ya wanajeshi 2000 wa cuba walifariki katika mapambano katika nchi ya Angola.
4.Fidel alijenga shule nyingi katika maeneo mbali mbali Africa mfano Tanzania shule za Ruvu,ifakara nk zilijengwa na Cuba.
5.Cuba imekuwa ikitoa mafunzo ya kijeshi na Intelligensia kwa nchi mbali mbali za Africa.
Ni aibu ni nchi 2 tu kutoka Africa ambazo zimetuma wawakilishi katika msiba wa Fidel, Robert Mugabe na Jacob zuma tu ndio wamehudhuria.
Na ni masikitiko makubwa nchi ya Angola haijatuma mwakilishi kwenda kuhudhuria msiba wa Fidel wakati zaidi ya wanajeshi 2000 wa cuba walikufa katika mapambano nchini Angola katika harakati ya kuikomboa Angola na wanafunzi 14,000 waipata kusomeshwa nchini cuba.
mozambique,Congo waliosaidiwa kijeshi na Fidel Castro kupigania ukombozi leo hii wamesusa kuhudhuria mazishi ya Fidel.
Cuba walikuja Africa kama madaktari,walimu,wanajeshi,wakufunzi ,watafiti lakini siyo kuja kwa lengo la ukoloni.
Hata msiba wa Ronald Reegan ma rais wa nchi 6 Africa walihudhuria wakati Ronald Reegan na serikali yake walikuwa wana sapoti apartheid kule Africa kusini na walimuorodhesha Mandela kama Gaidi na alikuwa kwenye watchlist ya magaidi.Huku Fidel freedom fighter aliyeenda kumsaidia Mandela tukimsusa
Hakika Fidel Castro hajatendewa haki na nchi za ki Africa,jumuiya ya ulaya na Amerika wamemtenga na sisi wa Africa tumemtenga pia.
R.I.P Fidel rasili mali na nguvu ulizotumia kusaidia Africa ungetumia kuliendeleza taifa lako