Fid Q: Rado ni msanii pekee aliye ni-diss kwa mistari mikali kuliko msanii yeyote

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
Fareed%20Kubanda2.jpg

Baada ya lile bifu la siku nyingi kati ya rapa kutoka mwanza Fareed kubanda a.k.a Fid Q na msanii mwenzake Rado kutoka lebel ya Kiraka Rado,hatimaye Fid Q amekiri kuwa Rado ni msanii pekee aliyemdiss kwa mistari mikali kuliko wasanii wote waliowahi kumdiss.

Akizungumza na Enewz Fid Q alisema kuwa Rado ni rafiki aliyemfunza kitu katika maisha pasipo kufafanua amemaanisha nini katika sentensi yake hiyo ikiwa hivi karibuni tu ametoa ngoma ''Sihitaji Marafiki'' yenye mistari inayoonesha kuwa hana imani na tabia za washikaji.

Rado na Fid Q waliingia kwenye mgogoro kuhusu mashairi ya wimbo wa Mwanza mwanza wa Fid Q ambao Rado alidai aliibiwa mashairi na baadaye akatoa wimbo ulioitwa 'Usiulize' ukiwa na mashairi yaliyomdiss FID Q,hata hivyo wakati hili linatokea Fid q alikanusha kuiba mashahiri ya Rado.

Hata hivyo kulikuwa na story kuwa chanzo hasa cha ugomvi huo kilianzia kwenye wimbo wa Fid Q 'Chagua moja' ambao unadaiwa mwanzo ulifanyika studio za Baucha records ukiwa na verse ya Rado ,fid Q,Adili na TID kwenye chorus lakini baadaye fid Q alihamisha wimbo huo kwenda kwenye studio ya Bongo records na kufuta mashairi ya Rado.
 
Kuna watoto wa ILALA kama sikosei wanajiita WATANABE,ndani kunamchekeshaji Tinwhite walipata kuimba nyimbo ya moja ina verse inasema"Tulianza rap kabla hawajatoka Mwanza,Pia ipo ya Bigboy stereo "Tunawasukuma wasukuma warudi Mwanza,nadhani zote zilikua zinamlenga kubanda,hiyo ya Rado inasemaje mkuu?
 
ule wimbo wa usiulize verse ya kwanza mpaka ya mwisho nidiss kwa Fareed utafute usikilize
 
Usiulize bado nimo, rado namwaga wino, uwezo nini sijui, kamwe haviusiani na wimo
Duh, kitambo kidogo naukumbuka, nlikua nafuatilia haya mambo ila tumekua saivi, hivi rado yuko wapi? Ilikuwaje akapotea kimziki? Nlikua namkubali dogo
 
Yani zaman ilikua raha unasikiliza kitu hapohapo umepata elimu,mi mwenye bi kushungi lakini ulikua hunambii kitu kwa hiphop,kubanda ndo alinifanya nifuatilie mziki wao,katika ile ngoma ya story za mtaa kuna verse anasema"Siku zote Adam akosi Eva kumshawishi,hajalishi maji ni ya moto lazma ataurudia ubaridi,kwenye video anaonekana jamaa kakaa na mwanamke wake halafu anapita mwanamke mwingine jamaa anageuka kumtizama halafu kidogo anarudisha shingo kuendelea na mwanamke wake.SIYO SIRI ILINIFANYA NIPUNGUZE WIVU.
 
Wewe ni Ke?
 
...ati!?..jina la asili ya wapi na linatamkwaje?...au ndo female version ya odhiambo!?
Ni makeke yangu tu,nina rafiki yangu anaitwa OTHAIGO binti wa kikurya huyu,kipindi tunasoma nilikua napenda sana kumtania kwa kulinyambua jina lake mana hata mimi jina hili ndo kwanza nilimsikia yeye,si unajua dar kumejaa akina Asha na Amina,ndo nikawa nanyambua jina lake tu mara othambo,otwango, ondiango,hili ondiango tumemuita sana mi na mabest zangu school, kwa kufuatisha hii Odhiambo ya kikenya,basi ndo nikakwamia hapa pa othiambo ndo nikaamua nilitumie.
 
....teh teh teh..na una hakika sio matusi kwa lugha ya wenyewe? huyo kwenye avatar ndo wewe na sie tuanze "makeke yetu!?"
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom