Uterine Fibroids (Myoma): Preventing, Shrinking and Avoiding Surgery

JamiiForums

Official JF Response
Nov 9, 2006
6,200
4,984
FIBROIDS NI NINI?

Ni vimbe ambazo hutokea katika sehemu za uzazi wa mwanamke. Ni vimbe zinazotokea katika kizazi (uterus). Vimbe hizi hazimaanishi kuwa ni kansa. Zinatengenezwa na kambakamba zilizofungamana (muscle fibre) Fibroids huanza kwa ukubwa kama wa njegere, lakini huweza kukua kwa ukubwa wa tikiti maji. Inakadiriwa kwamba asilimia kati ya 20-50% ya wanawake wana hili tatizo au watakuwa na hili tatizo katika kipindi Fulani cha maisha yao. Fibroids hupatikana zaidi kwa wanawake wenye umri kati ya miaka 30-40 na hupungua ukubwa mara baada ya umri wa utu uzima. Uchunguzi uliofanyika huko Marekani unaonesha kwamba Fibroids huwapata wanawake wa Kiafrika mara tisa zaidi ya wanawake wa kizungu.

Nini kinachosababisha Fibroids?

Ingawa sababu/chanzo hasa cha Fibroids hakijulikani, utafiti unaonesha kwamba fibroids huchochewa na oestrogen mwilini. Mara nyingi fibroids hukua kwa mwanamke pale ambapo kiwango cha oestrogen kimeongezeka mwilini, na pia fibroids hupungua pale ambapo kiwango cha oestrogen nacho kikipungua.

Oestrojen ni nini?

Ni mkusanyiko wa homoni ambazo ndizo zinazoukuza mwili wa mwanamke kijinsia, mfano ukuaji wa viungo kama matiti na kupata hedhi.

Pia wanawake ambao wana uzito zaidi ya kg.70 wana hatari kubwa zaidi ya kupata fibroids, pia hii ni kutokana na kiwango kikubwa cha oestrogen katika umri huu. Wakati wa zamani fibroids ingeweza kusababishwa na matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango. Hii ni kwa sababu vidonge hivi vilikua na kiwango kikubwa cha oestrogen. Lakini kwa hivi sasa vidonge hivi vya uzazi wa mpango havina kiwango kikubwa cha oestrogen kama ilivyokuwa hapo awali.

Aina za Fibroids

Fibroids zinatofautishwa kutokana na sehemu ambapo imetokea. Yapo makundi mawili yanayoweza kugawanya aina za fibroids.

1) Fibroids zinazotokea ndani ya mji wa mimba,
2) Fibroids zinazotokea kwenye kuta za nje ya mji wa mimba.

Dalili za Fibroids

Inakadiriwa kwamba, asilimia 75% ya wanawake wenye fibroids hawana dalili zozote na wala hawajui kama wana fibroids. Kuweza kujua dalili za fibroids, inategemea na ukubwa wa fibroid na wapi zilipo kwenye kizazi. Hii pia inachangia aina ya dalili atakazopata mtu. Mfano: Fibroid ndogo ambayo ipo kwenye kuta za kizazi haitakuwa na dalili sawa na Fibroid kubwa inayoota kuelekea nje ya kizazi. Dalili kubwa inayofahamika ni ile ya kutokwa na damu nyingi sana wakati wa hedhi. Dalili nyingine ni kama maumivu ya tumbo, inaathiri mfumo wa haja (kubwa na ndogo), kuhisi mkojo mara kwa mara, mkojo kutoka kidogokidogo/kuvuja, mkojo kushindwa kutoka kirahisi, kukosa choo (constipation), kuwa tasa (kutoshika ujauzito), maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Fibroids na Ujauzito

Fibroids zinaweza kusababisha matatizo yafuatayo kwenye ujauzito:
1. Kuharibika kwa mimba/ujauzito
2. Inachangia kwa mwanamke kutoshika mimba kutokana na kubanwa kwa mirija ya uzazi.
3. Pia kutokana na msukumo unaosababishwa na fibroids, mirija ya uzazi hubanwa na hivyo kushindwa kupitisha mayai kuelekea kwenye kizazi (uterus)
4. Mwanamke anapokuwa mjamzito na pia akawa na fibroids kwa wakati huo, mwili unaweza ukasitisha kupeleka damu kwenye fibroids na kuifanya fibroid kusinyaa. Kama hili likitokea husababisha maumivu makali ya tumbo, na pia kufanya kizazi kutanuka na kusinyaa, baadae mimba huweza kutoka kabla ya wakati wake.
5. Wakati wa kujifungua, kama fibroid itakuwa kwenye njia ya kutolea mtoto inaweza kusababisha damu nyingi kutoka, au ikishindikana mama hufanyiwa upasuaji ili kumtoa mtoto.

Utaweza vipi kugundua kama una Fibroids?

Kama hakuna dalili inawezakana tu kwa kufanya vipimo. Dalili zikiwepo na kuhisi unalo tatizo la fibroids, mwone daktari kwa ajili ya kupata vipimo ili kujua kama una fibroids au la.

Vipimo vya Fibroids

Daktari huweza kufanya uchunguzi kwa vipimo kati ya hivi vifuatavyo:-
  • Ultrasound scan (Mionzi)
  • Hysteroscopy (kifaa kidogo ambacho huingizwa kwenye kizazi kupitia sehemu ya uke (vagina)
  • Laparoscopy (upasuaji wa sehemu ndogo ya tumbo pamoja na kuwekewa kifaa kidogo sehemu ya uke (vagina)

Kuishi na Fibroids (wanavyoshauri hospitali)

Njia iliyozoeleka ya kuishi na fibroids zinazotoa damu nyingi ni kuzilinda na si kuzitibu. Utashauriwa kupata uangalizi/uchunguzi wa mara kwa mara lakini bado utahisi unahitaji msaada zaidi kwa jinsi unavyojisikia

Matibabu ya Fibroids (Hospitali)

Zipo njia kuu mbili za kihospitali za kutibu fibroids:-

1. Kutumia dawa (drug treatment)
2. Kufanyiwa upasuaji (surgical procedures)

1. Kutumia Dawa

Mkusanyiko wa dawa zijulikanazo kama GnRH analogues hupunguza kiwango cha oestrogen mwilini na hivyo kusababisha fibroid kusinyaa. Uchunguzi unaonesha kwamba dawa hizi zikitumika kwa miezi sita hupunguza ukubwa wa fibroid kwa asilimia 50%. Pia dawa hizi husitisha mzunguko wa mwezi (hedhi). Inashauriwa kwamba matumizi ya dawa hizi (GnRH analogues) yasitumike zaidi ya miezi sita kwani dawa hizi huweza kuleta madhara makubwa. Pia mara baada ya kuacha kutumia dawa hizi, wiki chache baadae fibroids huanza kukua tena, na mwanamke huanza kupata hedhi tena kama awali, ikiambatana na maumivu makali. Kwa baadhi ya wanawake huwa hawapati tena hedhi hadi kifo.

2. Kufanyiwa upasuaji

Upasuaji unahusisha mambo yafuatayo:-
  • Kuiondoa fibroid yenyewe na kuacha kizazi(Myomectomy)
  • Kukiondoa kizazi kabisa (Hysterectomy)
  • Kuzuia damu kwenda kwenye fibroids (Uterine artery embolisation)

Ipo njia ambayo haijazoeleka sana, ambayo mtu huchomwa sindano nne tumboni zikielekea ilipo fibroids kwa ajili ya kuiua kwa kemikali maalum.

Hii ni elimu kwa ajili ya afya yako pia usiwe mchoyo uipatapo mshirikishe na mwingine aweze kupata uelewa. Kwa msaada pia kuepuka hali hiyo kukupata kuna food supplements ambazo zipo.

SOMA PIA: TAHADHARI: Dawa za nywele zinasababisha uvimbe wa kizazi kwa wanawake

========

Natural remedies:

Not too long ago, a 35-year-old housewife walked into a hospital in Festac Town, Lagos. The once lively lady had suddenly become a bundle of worries. After giving birth to two beautiful daughters, she was finding it difficult to be pregnant again.

The family had gone through thick and thin and now the problem was threatening the marriage.Apart from painful menstruation, she regularly had symptoms of pregnancy: missed periods, swollen breasts and protruding stomach.

She had come to this clinic hoping to find a cure.After physical examination, the doctor recommended that she should go through scan. And then the bubble burst. She had a growth right inside her womb. She had fibroid.

Fibroid is not a new disease, but it is a development that is bringing tears into the lives of many women and it is wrecking marriages. Even when surgery is recommended, very few ever get pregnant again. In fact, according to experts, surgery for fibroid could involve the removal of the patient's womb. It is that bad and the number of carriers is growing.

It had no known cure, that is, until now.So, it was a call to arms when, while responding to complaints from its independent distributors on the prevalence of this condition, Forever Living Products (Nigeria) Limited, engaged a man versed in the field of clinical sexology, a medical doctor with knowledge in herbal medicine and a marriage counselor, Dr. Taiwo Fadeyi - to throw light into this dreaded disease, its causes, its management and eventual cure.

For three hours, the Faculty of Medicine, University of Cairo, Egypt - trained medical director of F&G Clinic & Laboratory Services, Lekki, Lagos, Dr Fadeyi, held a Lagos audience that had defied the early morning rains of Saturday, September 17, to listen to him, at the FLP Eagle Hall, spell bound.

Dr. Fadeyi described fibroid as a non-cancerous tissue that is found in the womb of women. "It is a mass which creates a lot of problems for women in terms of fertility, menstrual problems and frequent abdominal pains." According to him, fibroid has become rampant in the Nigerian society due to modern lifestyle. "The causes of fibroid can be traced to the type of lifestyle that our people now live.

Such lifestyles cannot be compared with the natural lifestyles of the people of old," he said.He added: "There are so many things that are bringing in a lot of oestrogen into the body systems now, like plastics, pesticides and even the foods and the processes under which we breed animals for consumption".

He continued: "Most of these things, including fishes, are bred artificially. So they store those hormones that we are imbibing and that is what is causing some of these problems".The Eagle Hall was silent. "What to do?" It was like he was responding to FLP history statement: "to offer the finest and healthiest products to the public that are proven to promote lasting health and wellness, and do it in a personal way""You need supplements; they do help and they will continue to help", Fadeyi assured.

"Normally, Forever Living Products and other herbal supplements are holistic things, they go into the body and try to reverse whatever bad that had been done inside the body and they want to do that holistically. That is the way they help," he said, displaying to the audience, two live specimen of fibroid extracted from the womb of patients from his clinic recently.

Dr Fadeyi said FLP range of supplements was capable of not only managing the ailment, but they provide permanent cure, recommending supplements like Aloe Vera Gel, Arctic Sea, Aloe Berry Nectar as foundation supplements that could take care of fibroid and even help to restore and check re-growth for those who had undergone surgery for the disease."Definitely, a surgery for fibroid is recommended for cases which cannot be managed.

In cases of surgery, where you have a patient that is bleeding uncontrollably, or you have a patient who has a big fibroid mass, I will personally suggest surgery for such cases and thereafter they can go back and use these supplements to prevent reoccurrence.".Fadeyi stressed that Forever supplements are natural products which have been accepted all over the world as a check to contamination that today's living has brought.

To those with fibroid, he advised, "For each particular case, I would just normally say, herbal supplements."



Source: Nigerian Tribune - Fibroids: Supplements provide permanent cure -Dr. Fadeyi

Very fortunate this herbal supplements are available in Tanzania!
 
kuwa specific please fibroids zikoznyingi kwa aina zake tupe ya fibroids yako kama ulivyo ambiwa na daktari
 
KOKUTONA Hi!

Fibroid ni uvimbe unaotokea kwenye misuli ya kizazi (uterus), inaweza kutokea kwenye body, fundus, kwenye isthmus mpaka kwenye cervix.

Popote ilipo fibroid inakuwa na kuongezeka ukubwa with time. Huwapata sana watu ambao hawajazaa kabisa au wamechelewa kuzaa mpaka kufikiaa umri wa miaka 35 na kuendelea au waliozaa watoto wachache (low parity), ndio maana masister wa kanisani wanasumbuliwa sana na tatizo hili.

Dalili kubwa ya fibroid ni kutoka damu nyingi wakati wa hedhi (menorrhagia), pia uvimbe tumboni kama imekuwa kubwa, maumivu tumboni hasa ikipata mabadiliko yanayoitwa 'red degeneration' au uvimbe ukikandamiza nearby structures. Uvimbe pia husababisha matatizo ya uzazi ambapo mgonjwa anacomplain failure of conception lakini si wote wapo wanaoconceive wakiwa na uvimbe. nk. asilimia kama 0.1 ya vivimbe hugeuka cancer (sarcoma), very rare.

Yapo matibabu ya dawa lakini yote ni kwa ajili ya kupunguza kiasi cha damu kinachotoka, au kupunguza maumivu lakini kamwe hakuna dawa ya kuondoa uvimbe. Uvimbe unatibiwa kwa upasuaji tu ambao huusisha kuondoa uvimbe peke yake au kuondoa kizazi kutegemeana na uvimbe ni mkubwa kiasi gani au kama mtu bado anataka kuendelea kuzaa.
 
Matibabu inategemea na profile yako, i mean umri, umeshapata watoto, bt in short kuna dawa (Gnrh agonist) km gosereline zinapunguza size ya fibroid. Tiba kamili ni operation myomectomy wanafungua uterus kuondoa huo uvimbe, kw wamama waliokamilisha familia hysterectomy kuondoa kizazi.
 
Ahsante sana ndugu kwa majibu mazuri. Mwenye tatizo ana miaka 34 na hakuwah kuzaa, aliambiwa na daktari apate mtoto kawnza ndo aende akafanyiwe operation ya kuondoa uvimbe. Akaambiwa sehemu ulipo according to ultrasound hauwezi kumzuia kuzaa. Wakamwambia unavoongezeka ni hatari pia. Na wakamwambia kuna dawa za kushrink fibroids, ila wakamwambia wao, hawana. Km zipo kweli ni zipi? Niweze kumsaidia hyu ndugu yangu?
 
My closest friend had the same problem. Hii ilikuwa kama miaka 7 ilopita. Alikuwa anataka mtoto na alipobeba mimba ikawa shida kidogo ikabidi apewe bed rest kwa miezi takriban 6 hv. Ila baadaye alianza kuumwa sana kichwa na kupoteza damu nyingi. Pia tumbo lilikuwa kubwa kiasi unaweza kufikiri ana ujauzito. Njia pekee ilikuwa operation na amefanyiwa july saa hizi ni mzima na hana tatizo tena ingawa ndo hivyo tena hatoweza kuzaa. Niliongea na DK pale KCMC anasema ni kuchelewesha operation tu lakini finally lazima uvimbe uondolewe na ikibidi kizazi pia. See doctors in referral hospitals watakupa ushauri zaidi. Good luck pal!
 
Nilisahau kukuuliza km ana tatizo la kutokwa na damu. Km fibroid ipo lkn haitoki damu anaweza kusubiri, akaweka malengo ya kupata mtoto kabla ya operation. Bt kikubwa ni kwamba atahitaji kuuondoa huo uvimbe si mapema sana bt wkt itakapokuwa salama zaidi kufanya hvyo. Mpe pole zangu
 
Nashukuru sana kwa ushauri mzuri.
Yeye hatokwi damu na anapata mensration yake kama kawaida. 28 days for 3-4 days na damu ni ya kawaida kabisa, si nyingi.Tatizo ni maumivu upande wa kulia, wakati mwingine anashindwa hata kufanya shughuli zake.
 
Dada yangu ana miaka 31..aliolewa mwaka juzi na sasa ana mtoto wa mwaka mmoja.
Amegunduliwa kuwa na uvimbe tumboni-nadhani unaitwa mayoma fibroid, iko mitatu na wanadai ni mikubwa.Mmoja uko kwenye kizazi ni mkubwa sana.

Kawaida huwa inaondolewa kwa operesheni.Ila ye ameambiwa iko sehemu mbaya kiasi kwamba wakifanya operesheni lazima waondoe kizazi..sasa yeye yuko depressed sababu ndio ana mtoto mmoja tu na alitaka kuzaa watatu jumla..kinachomsumbua ni kwamba je hakuna namna yoyote ya kutibu bila kuondoa kizazi?
Na mimi napenda kujua,hizo fibroid mayoma zinasababishwa na nini? Na je zinawapata wanawake tu au hadi wanaume?
 
Learned sijajua dini yako lkn believe you me! by the name JESUS! dada yako atazaa na fibroid zitatoka. Mwambie atafute annointed water toka kwa Pastor TB Joshua. Afanye maombi ya nguvu awe na imani, hakika wengi wamezaa. My wife aliambia hivyo hivyo ana fibroid nyuma ya kizazi tukatafuta annointed water, tukafanya maombi sasa ni seven month pregnant. mwambie Imani yaweza hamisha milima sembuse fibroid...
 
Learned sijajua dini yako lkn believe you me! by the name JESUS! dada yako atazaa na fibroid zitatoka. Mwambie atafute annointed water toka kwa Pastor TB Joshua. Afanye maombi ya nguvu awe na imani, hakika wengi wamezaa. My wife aliambia hivyo hivyo ana fibroid nyuma ya kizazi tukatafuta annointed water, tukafanya maombi sasa ni seven month pregnant. mwambie Imani yaweza hamisha milima sembuse fibroid...

Na uvimbe unatoweka?Yanapatikana wapi hayo mafuta na yanauzwaje sh ngapi?
 
Dada yangu ana miaka 31..aliolewa mwaka juzi na sasa ana mtoto wa mwaka mmoja.
Amegunduliwa kuwa na uvimbe tumboni-nadhani unaitwa mayoma fibroid, iko mitatu na wanadai ni mikubwa.Mmoja uko kwenye kizazi ni mkubwa sana.

Kawaida huwa inaondolewa kwa operesheni.Ila ye ameambiwa iko sehemu mbaya kiasi kwamba wakifanya operesheni lazima waondoe kizazi..sasa yeye yuko depressed sababu ndio ana mtoto mmoja tu na alitaka kuzaa watatu jumla..kinachomsumbua ni kwamba je hakuna namna yoyote ya kutibu bila kuondoa kizazi?
Na mimi napenda kujua,hizo fibroid mayoma zinasababishwa na nini? Na je zinawapata wanawake tu au hadi wanaume?

Uterine Myoma/Fibromyoma/Uterine Fibroid ni uvimbe ambao asili yake unakuwa kwenye misuli ya kizazi (Uterus)...inaweza ukawa mmoja mdogo au mkubwa...au ikawa mingi midogo au mikubwa. Tiba yake ni operation, na kuna aina 2 za operation: 1. Myomectomy - Hii ikiwa kuna uvimbe mmoja na si mkubwa sana, na mwanamke ni kijana akihitaji kuendelea kuzaa. Operation hii hutoa uvimbe tuu na kuacha kizazi. Uwezekano wa vivimbe kujirudia ni mkubwa sana: 2. Hysterectomy - Hii kizazi chote kinatolewa kama alivyoambiwa dada yako. Hufanyika ikiwa kizazi kina uvimbe mmoja mkubwa sana au vivimbe vingi (kama ilivyokuwa kwa dada yako).

Kwa jinsi ulivyoelezea, zipo vimbe tatu tena kubwa...plus dada angalau ameshazaa mtoto mmoja, daktari yuko sahihi kumfanyia Hysterectomy. Cha muhimu ni kumuandaa kisaikolojia dada akubaliane na hali hiyo, na pia ninyi kama familia na mwenza wake mumpe ushirikiano wa karibu sana katika kipindi hiki kigumu kwake.

NB: Kwa sababu Myoma asili yake ni misuli ya kizazi...nadhani umeshafahamu kuwa wanaume hawawezi kupata Myoma!
 
Chimungguru asante kwa ushuhuda,kweli Yesu ni muweza.

Swali: hayo maji kuna vile yanaweza kukufikia hapa bongo au ni lazima mtu afike Lagos?

Learned sijajua dini yako lkn believe you me! by the name JESUS! dada yako atazaa na fibroid zitatoka. Mwambie atafute annointed water toka kwa Pastor TB Joshua. Afanye maombi ya nguvu awe na imani, hakika wengi wamezaa. My wife aliambia hivyo hivyo ana fibroid nyuma ya kizazi tukatafuta annointed water, tukafanya maombi sasa ni seven month pregnant. mwambie Imani yaweza hamisha milima sembuse fibroid...
 
Uterine Myoma/Fibromyoma/Uterine Fibroid ni uvimbe ambao asili yake unakuwa kwenye misuli ya kizazi (Uterus)...inaweza ukawa mmoja mdogo au mkubwa...au ikawa mingi midogo au mikubwa. Tiba yake ni operation, na kuna aina 2 za operation: 1. Myomectomy - Hii ikiwa kuna uvimbe mmoja na si mkubwa sana, na mwanamke ni kijana akihitaji kuendelea kuzaa. Operation hii hutoa uvimbe tuu na kuacha kizazi. Uwezekano wa vivimbe kujirudia ni mkubwa sana: 2. Hysterectomy - Hii kizazi chote kinatolewa kama alivyoambiwa dada yako. Hufanyika ikiwa kizazi kina uvimbe mmoja mkubwa sana au vivimbe vingi (kama ilivyokuwa kwa dada yako).

Kwa jinsi ulivyoelezea, zipo vimbe tatu tena kubwa...plus dada angalau ameshazaa mtoto mmoja, daktari yuko sahihi kumfanyia Hysterectomy. Cha muhimu ni kumuandaa kisaikolojia dada akubaliane na hali hiyo, na pia ninyi kama familia na mwenza wake mumpe ushirikiano wa karibu sana katika kipindi hiki kigumu kwake.

NB: Kwa sababu Myoma asili yake ni misuli ya kizazi...nadhani umeshafahamu kuwa wanaume hawawezi kupata Myoma!

Doh ahsante kwa kunfahamisha dah inatia huruma..
Na jee inasababishwa na nn exactly hii kitu just so that watu wajue wajikinge koz apparently wanawake wengi lately wanapata hii kitu..
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom