Fiancee mmbea

M-bongotz

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
1,734
405
Wadau naomna tumsaidie huyu jamaa..
"Mimi ni kijana wa makamo ambaye nimebahatika kupata mchumba ambae tumefahamiana kwa takribani miaka 2 sasa, she is perfect in many ways kasoro tabia moja tu aliyonayo inayonikera sana, yaani ni mmbea na mchonganishi kupita maelezo,ameshakorofishana na mashoga zake kibao kwa ajili ya tabia hiyo,nimejaribu kumkanya lakini naona haelekei maana kila mara napata malalamiko mapya, tafadhali kama kuna mtu ameshawahi kukumbana na kitu kama hicho anisaidie kunijuza alitatua vipi"
 
huh.............hlo tatzo mkuu,hbu jaribu kumtishia hutamuoa ka ataendelea natabia hyo
 
kuna uhusiano mkubwa sana kati ya kuwa na tabia za umbea na kuchonganisha watu
na kukosa furaha maishani.....
 
Wadau naomna tumsaidie huyu jamaa..
"Mimi ni kijana wa makamo ambaye nimebahatika kupata mchumba ambae tumefahamiana kwa takribani miaka 2 sasa, she is perfect in many ways kasoro tabia moja tu aliyonayo inayonikera sana, yaani ni mmbea na mchonganishi kupita maelezo,ameshakorofishana na mashoga zake kibao kwa ajili ya tabia hiyo,nimejaribu kumkanya lakini naona haelekei maana kila mara napata malalamiko mapya, tafadhali kama kuna mtu ameshawahi kukumbana na kitu kama hicho anisaidie kunijuza alitatua vipi"

Samahani mkuu sikulengi wewe..lakini hivi unawezaje kujua fulani ni mmbea au mchonganishi bila ya wewe kuwa mdau wa group hiyo. Kama ukisema fulani ni mgomvi ni sawa kwani unaweza ona jamaa aliyempiga anatoka damu...
 
labda wanamsingizia. Au anajiami. kosa la mchumba wako sio lako. Muoe hivo hivo kama umempenda na msapoti tu basi. Mie nilikuwa na wifi mwenye tabia ya umbea ushangingi na ugombanishi.

Kaka yetu mkimya sana, watu wakiogopa kumuambia. Na hata wakimuambia yeye wala hamulizi mkewe, kaka yetu alikuwa haweki akilini mambo kama hayo.

Kuna siku ugomvi ukaja hadi nyumbani kwa kaka, ngumi mtu, heheh. ile kaka anatoka nje tu wanawake wakakimbia na kumuambia yule wifi mumewe akitoka tu watakuja kumkomesha. Wifi akasema njoeni tu hawaogopi. wakarushiana maneno. kaka alipouliza, akasema mijitu mingine mishenzi.

wifi alipopata mimba ndio akatulia, akawa mpole. Alipo zaa marafiki zake wakamuambia anuka mikojo na kapitwa na wakati. akamuambia kaka wamie sehem ingine kuepusha shari. Sasa wifi yetu sasa sio yule wa zamani, sasa kakomaa akili na wanaendelea kuishi pamoja na mumewe vizuri tu.

mchumba ako, ujana unamuangaisha, ila kuna siku hiyo tabia ataiacha. Jifanye kama haujui, na jifanye haikuhusu wewe. Hao watu wanao kulalamikia waambie ni bora wamalizane wenyewe na huyu dada. Husifuatilie sana mambo ya wanawake, na inawezekana pengine wanamzushia tu mwana wa watu, na analipiza kisasi kwa kuwachonganisha. mtu hawezi tu kuwachonganisha watu bila sababu, mie naona labda mchumba wako anajiami kwa jambo fulani hapo. Muulize mwenyewe kwanini anafanya hivo, atakuambia.
 
Wadau naomna tumsaidie huyu jamaa..
"Mimi ni kijana wa makamo ambaye nimebahatika kupata mchumba ambae tumefahamiana kwa takribani miaka 2 sasa, she is perfect in many ways kasoro tabia moja tu aliyonayo inayonikera sana, yaani ni mmbea na mchonganishi kupita maelezo,ameshakorofishana na mashoga zake kibao kwa ajili ya tabia hiyo,nimejaribu kumkanya lakini naona haelekei maana kila mara napata malalamiko mapya, tafadhali kama kuna mtu ameshawahi kukumbana na kitu kama hicho anisaidie kunijuza alitatua vipi"

hivi hadi ukawa kijana wa makamo kapera......................kisa nini ukachelewa hivyo kujipatia jiko?????????????????????

kwenye hilo sijui na wewe yaelekea unapenda umbeya ..........................hivi na ya mashoga yanatoka wapi wakati mnayapendana ni yeye tu...................

pilii kama una kipaji cha kuwabadilisha watu usimwache.............wakati huu anahitaji sana msaada wako badala na wewe kuwa mlalalamishi.............kumbuka kama umekiri ni mkamilifu..............in many ways................................hilo ni dogo...............................just put up or simply shut up..................................
 
Samahani mkuu sikulengi wewe..lakini hivi unawezaje kujua fulani ni mmbea au mchonganishi bila ya wewe kuwa mdau wa group hiyo. Kama ukisema fulani ni mgomvi ni sawa kwani unaweza ona jamaa aliyempiga anatoka damu...

AM fully in concord with this analysis...................
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom